Kikwete mgeni rasmi Tamasha la Pasaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete mgeni rasmi Tamasha la Pasaka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Apr 19, 2011.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 14th March 2011

  RAIS wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka litakalofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka, Aprili 24 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

  Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Msama Promotions waandaaji
  wa tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa Rais tayari amethibitisha kuhudhuria.

  Alisema Rais Kikwete amekubali kujumuika na wadau mbalimbali katika tamasha hilo la aina yake na kwamba litakuwa bora kuliko matamasha mengine yaliyopita.

  Alimshukuru Rais Kikwete kwa kukubali mwaliko wao na kuongeza kuwa hiyo ni furaja kwa waandaaji pamoja na Wakristo wote kwa vile siku hiyo ni sikukuu ya Pasaka.

  Kwa mujibu wa Msama kiasi cha fedha kitakachopatikana kwenye tamasha hilo kitatumika kuwasaidia waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto, Dar es Salaam.

  Hata hivyo Msama alisema kwamba lengo la awali la kuwasomesha yatima na kuwasaidia mitaji ya biashara wanawake wajane bado lipo pale pale.

  "Pamoja kwamba tutawasaidia waathirika wa mabomu pia, lile lengo letu kubwa la tamasha hili kuwasaidia kuwasomesha yatima na wajane lipo pale pale," alisema.


  Chanzo: Habari Leo
   
 2. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Yah Pasaka njema....
  Nadhani ya mwaka huu itakuwa kali zaidi...
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Ataambiwa anatumikia mfumo kristo.
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 7,780
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Naogopa, hivi hataanguka kweli?!, mi simo.
   
 5. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Thanks Dr. President
   
 6. i411

  i411 JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 795
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Hapo waisilamu watapiga mdomo wee wakati raisi anaenda hapo ni kikazi manake ameobwa kuwepo hapo
   
 7. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 1,936
  Likes Received: 808
  Trophy Points: 280
  Hii namsifu kafanya kitu cha kistaarab hajaonyesha udini wala nn safi sana mheshimiwa....
   
 8. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,190
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Mmmmh, utaona sasa wanasiasa na watu maarufu watakavyojaa kwenye hilo tamasha hadi waislamu kama vile wanaenda kumsifu Mungu, kumbe wanatafuta chance ya kuwa karibu na Mkuu wa kujivua gamba ili awaone wanajichanganya sana katika masuala ya dini,

  Me wananiudhi wanafiki hawa wa kujivua gamba hadi nataka kupasuka sasa.........
   
 9. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,465
  Likes Received: 1,150
  Trophy Points: 280
  siendi tena..
   
 10. CHIMPANZEE

  CHIMPANZEE Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Hapo wamepatia, sasa tamasha litakua zuri. Hongera sana
   
 11. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,485
  Likes Received: 806
  Trophy Points: 280
  Hilo lawezekana kabisa
   
 12. M

  Makupa JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,741
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Hili tamasha Pengo na Malasusa watakhudhuria?
   
Loading...