Kikwete kuwa Gorbachev wetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete kuwa Gorbachev wetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 27, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Mojawapo ya hofu nilizonazo ni kuwa Kikwete hatimaye anaweza kuwa Gorbachev wetu. Yawezekana akaja na mawazo ya Perestroika anapotaka kugombea mara ya pili na watu wakakubali na matokeo yake itakuwa ni kuvunjika kwa Muungano wetu.

  Kama Gorbachev sidhani kama atakuwa na ujasiri wa kutumia nguvu kuzuia kumeguka kwa muungano au kama ana ujuzi wa kisiasa kuimarisha Muungano. Hadi hivi sasa ni wazi kuwa suala al Muungano analiona ni gumu mno kiasi cha kushindwa hata kujaribu kulirekebisha na matokeo yake yeye na CCM wanaamua kutafuta "the path of least resistance" a.k.a referendum.

  Kuna watu hata hivyo wanamuona Gorbachev shujaa na wanamshukuru kwa maamuzi yake; na kuna watu (kama kina Putin) ambao wamesimama na kurudisha ukutufu wa yule "Dubu" wa Ulaya Mashariki.

  Hili swali bado natafuta jibu lake kwani pande zote mbili naweza kuziona kinadharia.
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Muungano haulazimishwi na JK pekee, na si jambo la kumuangalia mtu moja moja na kutoa hukumu..muungano ni majumuisho ya historia, faida/hasara, wananchi, na wakati wake

  Kama muungano utavujika ni wakati wake umefika wala halitakuwa kosa la gorbachov wala JK, wanaolilia muungano watuambie kinagaubaga wanataka muungano kwasababu zipi? na wanapata faida zipi kwa kuangalia historia yake nk. please "msilete habari za alinacha eti nyerere kasema" this is an old crying song hatutaki kusikia..tuambiwe sasa hivi (wakati huu) muungano unatusaidia nini? na uwe muungano wa aina gani? kwa manufaa zaidi?

  Wanaokataa muugano vilevile watuambia hawataki kwasababu gani wanapata hasara gani na wanataka muugano wa aina gani?

  Hoja ziwekwe wazi..hii mambo imefichwa sana utafikiri karume na nyerere walikuwa malaika ni ujinga kwa nchi yenye wasomi kama nchi yangu
   
 3. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kikwete atakuwa shujaa wangu pale atakaporuhusu huu muungano kuvunjika.

  Muunguja anaweza kuweka bayana faida anazozipata kutokana na muungano huu. Zipi faida za muungano kwa mtanganyika wa Mtwara. Kama bahari Mtwara ipo, tena bahari ya Hindi. Kama ni reserves za mafuta, hata mtwara zipo, kama ni marine parks, hata Mtwara zipo, kama ni natural gas, hata Mtwara ipo. Kama ni watalii hata Arusha wapo. Kama ni ardhi, huku Tanganyika ndio usiseme, kama ni ng'ombe wa nyama, mbuzi, kuku wa kienyeji, ndizi, nyanya, vitunguu, matunda, mazao ya nafaka na ya jamii ya kunde tunayo.

  Je tunataka muungano ili tufaidike na karafuu?

  Hata mapacha inafika wakati kila mtu anachukua time na kuendelea na maisha, ije kuwa muungano wa kuchanganya kias kidogo cha mchanga! Huo mchanga uliochanganywa ulichukuliwa kila mkoa wa Tanganyika na Unguja?
   
 4. k

  kisikichampingo Senior Member

  #4
  Jan 27, 2010
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Muungano huu ulilazimishwa. Pamoja na mawazo mazuri ya Karume Senior na Nyerere wakati huo, tukiri kwamba wakati huu ni mwingine. Bila shaka, Karume Senior na Nyerere wangekuwa serious tangu wakati huo, wangeruhusu mchanganyiko halisi wa wazanzibari na wabara. Hili halikufanyika. Muungano feki sana ulikuwa, na Kikwete hana namna ya kuuokoa
   
 5. C

  Chief Masanja Member

  #5
  Jan 27, 2010
  Joined: Feb 6, 2007
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hali zenu, wajukuu wangu,

  kwanza kabisa tutulie ikiwa sehemu ya kumuombea mjukuu wangu, wa jina la kipenzi changu chief swetu.swetu fundikira mwanangu nenda kapumzike kwa amani ....................maana ukifungua masikia ni mengi yanasemwa haswa juu ya chanzo cha kifo chako.mungu wa baba yao ramadhani na babu yako swetu ndio wanaojua.buriani mwanangu.

  pili, nimeguswa kuchangia mjadala aliuanzisha mjukuu wangu, mwanakijiji hapo juu.

  kwanza , ieleweke huo ni mtazamo wake na kwa kiswahili kifupi hayo ni maneno yake. nisingefikiri kama mwana kijiji anaweza kutofautiaa na yule wa juzi ambaye wakati wote akili yake imejaa kuamsha hisia ambazo yeye anafikiri zimefichwa.naomba niruhusu nikutoe wasiwasi.

  ni ukweli usiofichika kuwa mabadiliko yoyote yale uja na wakati. ninapozungumzia sababu nazungumzia pia viambata vyake.vitu kama uongozi uliopo na maafisa waandamizi wa uongozi huo ni sehemu pia ya mabadiliko hayo.

  lakini pamoja na yote. mabadiliko si jambo ambalo mtu mmoja anawerza sema fanya ikawa siku ya pili. ni jambo ambalo watu wote katika utawala wa muda ule ukubaliana na wakafanya. hapa nazungumzia uwepo wa vyombo vya kiusalama na wananchi kwa jumla yao.

  sasa sioni kama kuwa raisi kunakufanya wewe uwe chachu ya kuleta mabadiliko yote hayo peke yako isipokuwa kama mfumo mzima unaoishi utakubaliana na haya.

  kwa tanzania silioni hilo.mambo mengi sana yanafanyika na sidhani kwa mtu kama wewe ambaye unaangalia mambo kwa juujuuu tu unaweza yaona. angalia kati ya mistari.

  hivi unafikiri, inawezekana
  ......karume kuongezewa muda kwa kuwa wazanzibar wanataka.
  .....muungano wetu kuondoka sababu ya kitu kinaitwa referendum
  .....kuwa na chama kinaitwa ccj bila ya serikali kujua nani wamo ndani
  .....kufanya vita na serikali wakati maisha yako yanaangaliwa na hao.
  .....kufanya watu millioni 40 wahangaike na tabu kwa sababu ya watu wawili
  ....kuwa mnatuma sms huku big brother anakuangalia tu

  mjukuu wangu , kama unaweza pata majibu ya haya maswali machache basi pia unaweza jua nini ninachokizungumzia.

  mabadiliko ni jinsi mfumo unavyotaka. wakati tulionao ni wakati wa mpito na maisha yanaendelea.

  toa wasiwasi , mchi haiwezi kufikia huko na hata huyo bwana Jakaya hawezi kuwa hicho unachofikiria wewe ndicho.

  HABARI ZA ASUBUHI.
   
 6. W

  WildCard JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  JK wetu asipoisimamia na kuilinda KATIBA yetu ya JMT atakuwa Gorbachev wetu. Zanzibar sasa hivi wanatoa matamshi yao kama vile katiba hii haipo, haiwahusu. JK amewekwa pale kwa mujibu wa katiba hii lakini anakuwa kama anaionea haya vile!
   
 7. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  ni wazi kwamba muungano una matatizo makubwa......wote yanatuhtusu haya,nadhani ni vema tushauri namna ya kuuboresha au kuuvunja kwa heri..binafsi naamini Zenj itaendelea vzr sana ikiwa nchi huru..
   
 8. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
   
 9. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu Tumain,

  I second you on this...
  Its time hawa viongozi wetu waweke haya mambo wazi... We all know more problems huu muungano uko nayo, dawa si kuyakimbia but rather tudiscuss tukiangalia yapi yalikuwa makosa yapi ni mazuri, ili wote (bara/visiwani) tufaidike nao.

  Kweli imauma sana kuona nchi kama hii yenye wasomi na watu wenye upeo tunakalia ubabaishaji na kudhani waasisi walikuwa miungu!!!

  Amandla.
   
 10. C

  Chief Masanja Member

  #10
  Jan 27, 2010
  Joined: Feb 6, 2007
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wajukuu zangu, mie naungana na nyie juu ya ulinzi wa katiba yetu na wazo la kuwa makini juu ya utawala wa kikatiba maana huu ndiyo msingi wa muungano wa nchi hizi mbili.

  manufaa ya muungano, hauwezi yagusa kwa mkono hasa ukiangalia juu ya nini ambacho wewe kama mtanzania unapata haswa kwa upande wa hewa au mambo yanavyokwenda. hapa nanzungumzia mwananchi anayeishi chunya au kule kibondo upande wa kigoma.

  lakini yapo mengine ambayo yataharibika baada ya muungano huu kuvunjika.ni dhahiri kwamba hali ya amani na utulivu iliyopo na tafsiri ya mshikamo iliyopo baina ya mataifa yetu ,kwa upande wa biasharana hata mahusiano binafsi yanatia moyo.kuvunjika kwa hili kutaathiri sana haya.

  lakini pamoja na haya yapo mambo mengine mengi ambayo kwa kweli tutayapoteza kama hali hii itatoweka.

  suala la kulinda muungano ni letu wote na nisingependa tulipuuze. watu wa kwanza kuchukiwa ni wale wanaopinga muungano huu.
   
 11. W

  WildCard JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
   
 12. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
   
 13. M

  Mchili JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Pamoja na kwamba ni muhimu kuilinda katiba na ni wajibu wa raisi na raiya wake, elewa kuwa katiba sio msaafu au bible. Kama ikidhihirika kwamba haikidhi mahitaji ya wananchi kwa wakati uliopo ni muhimu kuibadili kwa utaratibu unaofaa. Katiba tulio nayo ya JMT ina upungufu mkubwa sana hasa kwenye masuala ya muungano. Hivyo JK anatakiwa afungue macho aone hata kama itabidi awe Gorbachev kwa maslahi ya utaifa ni bora zaidi.
   
 14. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Natumai na wewe ni msomi mbona hueleweki where did u stand on? and why? TOA MTIZAMO WAKO.:mad::mad:
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Lakini, Ikulu au rais (kama taasisi) nimoja ya mihimili muhimu ya Muungano. Mtu anayeongoza taasisihiyo anapaswa kutoa uongozi utakaotyoa mwelekeo wa mambo muhimu kama nchi na kwa sisi, Muungano ni moja ya mambo muhimu kabisa. Kwa hiyo, JK hatoweza kukwepa lawama au sifa iwapo lolote litatokea kuuhusu Muungano wakati wa kipindi cha yeye kuongoza taasisi hiyo
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Jan 27, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
   
 17. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu,

  Msimamo wangu ni kwamba mambo ya siri za muungano ni ujima na ujinga

  Muungano ujadiliwe upya prons and cons uwekwe nje utolewa sirini mpaka hadharini (public)

  Pakubaliwe kama muungano uwepo au usiwepo! (referendum) na wa namna gani kwa faida ya watu walioungana!

  Kuogopa mizimu ya kina nyerere na karume ni dalili ya shirk yaani tunaamini wafu utafikiri hatuna elimu...bana!

  Wanachofanya wazanzibar nakiunga mkono kwakuwa watanganyika ni kanyaboya, hawajui kwanini wako kwenye muungano na faida zake.
   
 18. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
   
 19. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #19
  Jan 27, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Umuhimu wa muungano ni nini?

  Muungano ni muhimu kupita maji na umeme shinyanga?

  Muungano ni muhimu kupita kuondoa mafisadi serikalini?

  Muungano ni muhimu kupita kujadili tume huru, katiba mpya? kidding!
   
 20. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #20
  Jan 27, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kusigina katiba kuanzia kwenye SMZ kutaka Bendera yao, then Ukaja kupigwa kwa wimbo wao wa taifa kwenye baraza la wawakilishi, ikaja kodi , mafuta na hivi karibuni wabara wataambiwa kuanza kutumia pasi za kusafiria kuingia huko visiwani. Hadithi ya Mwarabu na Ngamia inakaribia kutimia. Nadharia yangu ni kwamba ata kama URT itavunjika then kuna hatari ya kuwa na serikali ya Pemba na Zanzibar { Makubaliano ya Maalimu na Karume nyuma ya Pazia}. Kikwete inaonekana ameridhia kufa kwa URT.
   
Loading...