Kikwete: Kuna watu wana mitambo ya kufyatua uongo

Kikwete: Kuna watu wana mitambo ya kufyatua uongo

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Wakati akifungua kikao cha NEC kilichopokea mapendekezo ya Kamati Kuu kuhusu Rais John Magufuli kuwa Mwenyekiti mpya, Jakaya Kikwete alisema kuna propaganda za wafitini ambao walifikia hatua ya kuandika kwenye gazeti hivi karibuni habari inayosema “Uteuzi wa Magufuli kupingwa NEC”.

Alisema habari hiyo ni potofu, kwa sababu hakuna kitu kama hicho na hakikutokea na kwamba walioiandika, inaonesha wana mtambo wa kufyatua uongo.

“Kuna watu wana viwanda na mitambo ya kufyatua uongo. Hawa wanazalisha bidhaa mpya zenye uongo na uzushi kila siku,” alisema.

Aidha, alisema wapo watu hawalali na wana taabu mno, wanapoona CCM ina nguvu na inaendelea kuwa imara. Alisisitiza kuwa CCM haibabaishwi na uongo na uzushi wa watu hao; kwani mara zote kama kuna jambo ndani ya CCM, hupelekwa katika vikao husika, kisha hujadiliwa na kufikia maafikiano.
 
Kikwete kwa vijembe tu nampa pongezi.

Alinifurahisha aliposema kuna gazeti limeandika habari inayosema ‘JK hachomoi’, mie nimechomeka nini, sijachomeka chochote kwa hiyo sina cha kuchomoa.

Kuna watu watamkosa na kumkumbuka kwenye eneo la vijembe vya kisiasa.
 
Rais wangu bora na mtetezi wa wanyonge
Kikwete amemuua Lowassa kisiasa huku akitabasamu.

Nguvu ya Lowassa aliyoikusanya kuanzia mwaka 1992 ilisambaratishwa kwa gharama ya hii kalamu;
03-BICcristal2008-03-26.jpg
 
Haitotokea BAVICHA wakamsifia au kupongeza jema lolote la Rais Kikwete. Chuki yao inatokana na kushindwa uchaguzi kwa Mamvi ambaye walitegemea wangepata nafasi za kazi za uteuzi za kisiasa.

Ukweli usiopingika wengi wao hawapo vizuri upstairs na ushahidi upo katika uwasilishaji au uwezo wa kujibu hoja.

BAVICHA hawataa wampende, wakiwa na njaa ndio kabisa akili zinawaruka hadi kutoa matusi kwa watu wasiohusika.
 
Alituambia nanukuu pale Lumumba akimtambulisha Mgombea wetu wa CCM, "Mlisema mimi Mpole Nawaletea JPM yeye Mkali." Hakika Viongozi wetu CCM huwa hatukosei toka Awamu ya kwanza hadi hii ya Tano na CCM ndo kwanza Ina Imarika ikiwa Inadhihirisha ya kuwa ni Chama cha Mapinduzi chini ya Uongozi Imara Mahiri Makini wa Hekima na Busara wa Viongozi wake kwa Misingi ya Katiba yake,Imani,Madhumuni na Kanuni zake iliyojiwekea Hongereni CCM.
 
He he he mitambo na viwanda yva kufyatua uwongo. Tanzania ya viwanda imetimia.
 
Kikwete amemuua Lowassa kisiasa huku akitabasamu.

Nguvu ya Lowassa aliyoikusanya kuanzia mwaka 1992 ilisambaratishwa kwa gharama ya hii kalamu;
03-BICcristal2008-03-26.jpg
Kwa kitendo hiki cha kishujaa makosa yake yote akiwa rais yamefutwa. Tunamtakia mapumziko mema na maisha marefu.
 
Back
Top Bottom