Kikwete: Kuna mpasuko wa kisiasa Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete: Kuna mpasuko wa kisiasa Zanzibar

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zawadi Ngoda, Aug 31, 2010.

 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Mbio za muungano zilifikia kilele chake pale JK alipoamua kuuvulia njugaMuungano, na kuahidi kuupatia ufumbuzi wa kisiasa. Muungano ulijengwa na JK(Kambarage) na kusua sua bila mafanikio, na ukatafutiwa ufumbuzi na JK (Kikwete). Maraisi wote waliopita hawakuisha kuwaita wadai haki zao kuwa ni wahuni.

  Mwaka 2000 mara baada ya uchaguzi mkuu Wazanzibari zaidi ya 200 waliuliwa na bunduki na helkopta zilizonunuliwa kwa fedha ya walipa kodi, kwa amri ya Mkapa. Na wote waliouwawa aliwaita wahuni, huku akimtafuta muhuni mkuu, Sheikh Sharif na Prof Lipumba. Na baada ya muda si mrefu nao wakashikwa na kutiwa ndani. Kwa upande wangu huo ndio ulikuwa mwisho wa demokrasia, na mwanzo wa udikteta. Hata wale aliyewauwa Mwebechai nao walikuwa wahuni tu, na sheikh ponda ndio kiongozi wa wahuni. Ilionekana kana kwamba Mkapa alikuwa Rais wa wananchi wahuni nchi nzima.

  JK wakati huo akiwa katika serikali ya Mkapa, na kwa ujumla alikuwepo ktk serikali zote zilizopita, aliyaona mapungufu yaliyosababisha matatizo hususan, Zanzibar. Na ndio maana alipoingia madarakani miaka mitano iliyopita alikuwa ni Raisi wa kwanza kukiri kuwa Zanzibar kuna mpasuko wa kisiasa. Kauli hii ilifurahiwa na wengi, na kuandikwa karibu katika magazeti yote TZ. Kwani kuutatua mgogoro wa zaidi ya miaka 40, si lelemama.

  Baada ya miaka takriban mitano toka aingia madarakani, yaonyesha dalili nzuri ya kutimizwa kwa ahadi yake. Siri kubwa ya kufanikiwa katika kutatua tatizo hilo, ni kuwaachia Wazanzibar wenyewe kuwa wachezaji wakuu, naye ni kam,a mtazamaji na mshauri. Viongozi wa Zanzibar wakaamua Serikali ya mseto, na baadae suala likatupwa kwa wananchi kupitia kura ya maoni, 66% wakapitisha pendekezo. Na baada ya hapo ikahitajika kufanyiwa marekebisho katika katiba, nayo yakapitishwa kwa kishindo na Baraza la wawakilishi. Kwa kipindi hiki chote hakuuwawa hata mtu mmoja, kana kwamba wahuni waliondoka alipostaafu Mkapa.

  Kilichonishangaza mimi ni kuwaona wasomi, wanasheria, magazeti na hata hapa JamiiForums, kupiga kelele sana hasa pale Katiba ilipoguswa. Na wengine kukiita kitendi hicho kama ni cha Kihaini, na hoja hiyo ikaungwa mkono na Watanganyika wengi tu. Sasa najiuliza wataundaje serikali ya mseto bila kugusa katiba? Au JK alipoonyesha dhamira ya kutatua mgogoro wa kisiasa Zanzibar walielewa nini? Au kulikuwa na mpaka katika ufumbuzi huo? Kama kulikuwa na mpaka ni nani aliouweka huo mpaka? N i maswali ambayo kila siku najiuliza toka kura ya maoni ipigwe na katiba kupitishwa bila majibu. Na ninapokaribia kupata jibu, basi ni jibu gumu sana, kuwa hawa watu ni watu wa shari hawataki amani.

  Na kama hivyo ndivyo, basi kundi hili liwe NGO au la kidini ndilo lililokuwa likifaidika na Muungano kwa njia moja au nyingine. Ninasikitika kusema kuwa kundi hili halina nafasi katika Tanzania ya sasa, na si tu kuwa limepotea njia bali litakufa kifo kibaya. Sioni haja yeyote ile ya kuulinda Muungano au kipengele cha katiba hata kwa kuuwa wananchi kwa kutumia madaraka vibaya. Vikundi kama hivi havifai kabisa katika jamii, na popote tunapokutana navyo ni lazima tuvionye na kuvitokomeza.

  Ninapigwa na bumbuwazi zaidi pale ambapo hoja zinazotolewa ni za kulaumu tu. Ningefurahi kama wangekuja na maelezo makini juu ya mapendekezo ya utatuaji wa mgogoro huo. Bado mnayonafasi ya kutoa hoja zenu, ni vipi mlihitaji mgogoro huo utatuliwe ili wananchi wa pande zote mbili zinazohusika huko Zanzibar wakarithika nazo. Msipoweza kutoa hoja basi malalamiko yenu hayana msingi kabisa.

  Lazima ikumbukwe kuwa polisi waliokuwa wanatumwa Zanzibar, ni makomandoo wa jeshi waliokuwa mafunzoni wakvishwa mavazi ya polisi. Watu hawa hawakujifunza kutuliza ghasia, bali kuuwa na hivyo ndivyo walivyofanya huko Zanzibar. Si hivyo tu bali vile vile wali wabaka watoto wa kike mbele ya wazazi wao. Kweli tuko tayari kuulunda muungano kwa dhamani hii? Hapana hii si Tanzania bali ni SOWETO. Hata mkinukuu maneno ya mwalimu ya mwaka 1964, bado si tiketi ya kuulinda muungano kwa dhamani hii.

  Hapa alipofikia Kikwete anahitaji pongezi, kwa hali yeyote ile si rahisi kuutatua mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 40 kwa amani kama tulivyoshuhudia. Hii ni sawa kama Rais Obama akafanikiwa kuutatua mgogoro wa Israel- Palestina. Ni nini anachoweza kupewa zaidi ya zawadi ya Nobel. Tumsifu JK kwa hapa alipotufikisha, na tuelewe kuwa ukuzaji wa uchumi unategemea sana amani ya nchi. Hongera Kikwete!!
   
 2. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  @Zawadi NGODA Asante sana kwa kutuwekea "article " hii nzuri.

  Kwa muda mrefu hapa katika JF kumekuwa na mawazo ya wengi kuiona Zanzibar ni kama kitu kinacho kera au kero. Watu wengi wanashindwa kuelewa historia ya Zanzibar na Muungano. Mawazo ya wengi hapa ni kuiona Zanzibar kama sehemu ya Tanzania kwa maana ya Tanganyika. Kwahiyo ,wanashangaa kuano Wazanzibari kulalamika na kuujadili Muungano. Kwa mtazamo wangu mimi tatizo la MAPASUKO wa kisiasa Zanzibar limesababishwa na CCM. kwa kuwanyima wazanzibari demkrasia ya kweli. kuwanyima haki ya kuchagua viongozi wanao wataka wenyewe.

  Hii imesababisha wengi wa Wazanzibari kuanza kuuchukia Muungano kwasababu ya kuona ni kama kipingamizi cha maendeleo yao. CUF ilishinda chaguzi zote zilizofanyika tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Kwanini CUF hawakupewa nafasi ya kuongoza? hofu ya CCM ilikua ni kwamba CUF walionekana kama ni chama cha kupinga Muungano. Kwanini watu waupinge Muungano? Sasa hapa ndio linakuja suala zima la utata wa siasa ndani ya Zanzibar.

  Kila Mtanzania anaamini au anakubali kuwa Muungano una kasoro, lakini wengi wetu hatuko tayari kukaa na kujadili kasoro na kutafutiwa ufumbuzi. Tuko tayari kulaumu na kuwaona wanaolalamika kama wanaleta kero,hata kama sababu wanayo.

  Utulivu wa kisiasa uliopa Zanzibar ni mchango mkubwa wa MH, Rais Kikwete.
   
 3. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hongera sana Mheshimiwa Kikwete

  [​IMG]
   
 4. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Si kweli! Pelekeni credit kunakohusika. Mwenyekiti wa CCM alishindwa kabisa kushughulikia suala la Zanzibar hadi Karume na Seif Shariff walipoamua kuketi na kukubaliana uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Hilo halikutokana na vikao vya CCM vilivyokuwa vikiongozwa na JK.
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  jee wakati wa mkapa aliweza kuwa karibu na wapinzani kama mwere? huyu jamaa kwa kweli mie nna mpa salute

  nnamkubali
   
 6. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sana sana kilichofanyika ni mafuta yanayochemka kuyatia maji. Mnategemea nini zaidi ya moto kulipuka na kuwaunguza wenyewe. Mie si Shekhe Yahaya Husein, Lakini mtu mwenye akili zake ahitaji manabii au waganguzi kuliona hilo. Katiba ya JMT imevunjwa ni ukweli.
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Aliye ndani ya box haoni nje mpaka atoke
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..matatizo ya kisiasa Zenj yanawahusu wa-Zenj wenyewe.

  ..hakuna Mtanganyika mwenye "muarubaini" wa kuyatatua matatizo hayo.

  ..nawapongeza wa-Zenj,kupitia viongozi wao, Karume na Maalim Seif,kwa kuachana na ile dhana kwamba Tanganyika itawafanyia kila kitu, ikiwemo kuwasuluhisha ktk migogoro yao ya kisiasa.

  ..wa-Zenj wajiandae kuhakikisha kwamba serikali ya mseto waliyoazimia kuiunda inafanya kazi bila matatizo kwa manufaa ya wananchi wa visiwa hivyo.
   
 9. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mie nilidhani kuwa hivi sasa kuna mgogoro baada ya maridhiano na tegemeo la kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa GNU

  Nnaamini kwa sasa wazanzibari wako makini sana na wamejipanga. nnataraji baada ya uchaguzi tanzania kutakuwa na mambo mazito.

  Nnataraji muundo wa muungano utabadilika, maana wazanzibari kwa ujumla sasa wameelekeza macho yao kwenye muungano, wanaamini kuwa wamepoteza dola yao na kuwa wilaya na wao hawako tayari kwa hilo

  Zanzibar inahitaji nguvu zake kamili na hawakao tayari kuona hali hii inayoendelea ya kugandamizwa na kuonewa au kufananishwa na mkoa au wilaya inakoma.

  Wao wako tayari kwa mazungumzo tena ya wazi juu ya muund wa muungano na hata ikibidi tanganyika wawe na serikali yao au muuungano uwe basi

  Japo la muuungano kuwa basi mimi siliungi mkono maaana nna mtoto wa kinyamwezi na tushazaa sasa sitaki damu yangu ipotee
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Aug 31, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Inachekesha sana naposikia watu wakitumia CCM kama ni chama cha Bara na CUF ni chama cha visiwani. Ni aibu iliyoje kwa Mzanzibar kusema kwamba Zanzibar hawana uwezo wa kuchagua viongozi wao hali viongozi wote wanaoshiriki ktk bunge, serikali na utawala wa Zanzibar ni Wazanzibar wenyewe. Yawezekana kuwa hawakuchaguliwa na wananchi lakini bado ni Wazanzibar wakiongozwa na baraza la Mapinduzi..

  Wachezaji wakuu wa serikali ya Zanzibar ni Wazanzibar wenyewe, hilo lifahamike kwani baraza la Mapinduzi sio baraza liloundwa na bara wala watu wenye asili ya Bara isipokuwa ni Wazanzibar (watawala). Kwa jambo lolote lile linalotokea Zanzibar limetokana na baraza la Mapinduzi ambao muda wote wamekuwa wakifikiria maslahi ya Zaanzibar kwa manufaa ya baraza hilo.

  Hawa ndio waisopenda kuona CUF wakishika madaraka ya kuongoza Zanzibar lakini kwa ujinga wa baadhi wachache, lawama zote zinawafuata Bara hali ukitazama kwa makini tatizo lopo visiwani kwenyewe. Huwezi kumweka Salmin Amoor na Seif Shariff Hamad meza moja wakajadiliana kwa usalama na kwa manufaa ya Wazanzibar. Na ndio maana halisi ya maneno ya JK kwamba - Kuna mpasuko wa kisiasa Zanzibar.

  Huo mpasuiko hauhusiani na Bara kisiasa hata kidogo isipokuwa wananchi wamepandikizwa hofu ya bara kutoa maamuzi yanayohusiana na Visiwani pasipo kufahamishwa ukweli kwamba ni baraza la Mapinduzi ndilo linaloweka masharti ya maamuzi yote ya kitaifa kuhusiana na Zanzibar.

  Hata huu mufaka uliopita baina ya CUF na CCM umepitia hatua za suluhu kwa kuwahusisha Wazanzibar wenyewe. yaani ni Wazanzibzr wenyewe wamefikia maamuzi ya kuweka kando tofauti zao na kuunda umoja wao..Kwa mara ya kwanza Karume (CCM) na Seif wa (CUF) wamekaa meza moja na kufikia maamuzi ambayo hawakuwahi kuyafanya miaka ya nyuma, hatua ambayo inatakiwa kupongezwa wahusika wake yaani Karume na Seif na sii Kikwete au serikali ya Muungano.

  Bara hawakuhusika na wala haikuwepo sababu ya wao kuhusika isipokuwa tu ktk maamuzi yaliyofikiwa ambayo ni kinyume cha katiba ya nchi Zanzibar na serikali ya Muungano. Kama wananchi WaZanzibar watakichagua chama cha CUF kuongoza nchi yao basi hakuna sababu ya kuwa na serikali ya Mseto. CUF wameshinda wameshinda wapewe Uongozi wa nchi na sio kuwahadaa wananchi na hili neno - Serikali ya Mseto ambalo linawahakikishia CCM visiwani (baraza la Mapinduzi) kuendelea kuongozi Zanzibar hata kama wameshindwa uchaguzi mkuu.

  Kilichofanyika ni kwamba Wananchi wa Zanzibar wamepigwa changa la macho, ktk kuwahakikishia WaZanzibar kwamba CUF haitaweza kuongoza nchi hiyo hata siku moja pasipo kuangaliwa na baraza la Mapinduzi. Yawezekana ni njia bora zaidi kwa leo lakini tofauti na maamuzi kama haya, chama Chadema kinapendekeza zaidi utawala wa Zanzibar kuendeshwa na chama kilichoshinda. Chama kilichochaguliwa na wananchi wake kwa ushindi wa kura nyingi ndicho kitakacho ongoza Zanzibar na sii kuunda serikali ya mseto kabla hata ya uchaguzi mkuu kufanyika huku kukiwa na dalili kubwa ya CCM kushindwa vibaya uchaguzi huu. Maamuzi haya ya kuunda serikali ya mseto ni kuwahahakikishia CCM kuendelea kuongoza hata kama wameshindwa uchaguzi...
   
 11. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  :becky: Ya Ngoswe ataachiwa Ngoswe daima!!
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nenda kanywe naye chai na yale mambo yenu mengine!
   
 13. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  ww mjanja sana, hivi unataka kutufanya sisi hatuelewi kuwa bara ndio wanaosababisha migogoro kule zanzibar?

  wao si ndio wako nyuma ya baraza la mapinduzi? wao si ndio wanaolazimisha nani na nani awemo ndani ya baraza la mapinduzi, na nini kiamuliwe?

  wazanzibari chini ya rais Jumbe walipotaka serikali tatu waliopinga walikuwa wazanzibari? waliomuondosha madarakani kwenye kikao kilichafanyika CBE dodoma walikuwa wazanzibari?

  wanaowasaidia CCM zanzibar kuiba kura kwa kuleta mamluki walikuwa ni wazanzibari?

  mm naaamini hata huku wazanzibar kukamatana kwao, wabara wakiona itakuwa hatari sana watajiotahidi kupenya kufitinisha.


  nnachokiamini wazanzibari wakikamatana na kushikana wabara hawatakuwa na pa kupenyea, maana walikuwa wakitumia migogoro na kutokuwepo maelewano baina ya wazanzibari kama njia ya kuimeza na kuimaliza zanzibar


  sasa kumekucha tujiandae kumuona mzanzibar akiamka kutoka usingizini na kudai haki zake bila ya kumuonea mtanganyika

  nataka ile tu daraja yangu

  sitaki nyengine kama wenzangu

  siiinui mikono kushika mbingu
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Sep 1, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hapana mkuu wangu mimi siii mjanja kwa aina yeyote ile isipokuwa nazungumzia historia ya na Ukweli usopenda kuukubali.
  Umezungumzia wakati Jumbe akitaka serikali tatu kama ni Wazanzibar waliopinga.. Jibu ni Wazanzibar ndio kwani ktk kina cha mwisho wa matatizo haya rais aliyekuwa madarakani sii alikuwa Mwinyi? Na Mwinyi ndiye alimfuata Nyerere na kumwomba msaada wake kuhusiana na hoja ya serikali Tatu. Na nani aliyekwenda kuwatonya CCM kuhusu Jumbe kama sii mwingine ila huyo Seif Shariff Hamad - Mzanzibar! Kwa hiyo ukweli unabakia kwamba hizi habari za bara kuhusika ni mazingaombwe tu mnayolishwa ili viongozi hao wa Mapinduzi wabakie madarakani lakini pamoja na yote hayo hamjachelewa.

  La kufanya jaribuni kuwaondoa hao viongozi toka baraza la Mapinduzi ktk uongozi wa Zanzibar (kwa kura zenu) kisha utanambia mbaya wako nani! Au umesahau majuzi tu Karume alitaka kuwarudisha Wangazija woote warudi Comoro kwa sababu ndio wapinzani wa hili baraza la Mapinduzi na wengi wao ni wanachama wa CUF.

  Huu ndio ukweli mkuu wangu pamoja na matatizo yoote ya Bara, hata siku moja Bara haiwezi kuingilia maslahi ya Visiwani pasipo baraka la baraza hilo ambalo ndilo lilimkataa Salim A. Salim kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano.. Na ombi lao likatimia, Nyerere asifanye kitu.
   
 15. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wewe uliyowasikia hewani ni hao watu wawili....Maalim Seif na MH,Karume. Lakini kwa maelezo ya Maalim mwenyewe makubaliano yalianza mabali kabla ya hao watu wawili kukutana ikulu Zanzibar. Mkutano wa Ikulu Zanzibar ulikua ni kuhitimisha tu kilicho afikiwa. Karume alipewa go ahead na JK na hii haikutokana na vikao vya CCM. Kwani hiyo ilikua ni adhma ya JK kuhakikisha amani na utulivu inapatikana Zanzibar. Ndani ya CCM kuna watu ambao hawajapendezwa na maridhiano yaliyo fikiwa...Mh,Kikwete anastahili pengezi .
   
Loading...