Kikwete kilimo kwanza, Lowassa elimu kwanza!

Kwani hatuwezi kuweka priority kwenye sera zote mbili? My take is that they are both right! Tuweke elimu mbele kwa watoto wetu lakini kilimo bado kibakie uti wa mgongo wa Tanzania!

Ndo nilikuwa nawaza hili jambo......kwani ni lazima tuweke mayai yote kapu moja...mbona hizi wizara kila moja ina budget yake, waziri na full potentials to make them move???

Mbona tunakuwa kama mazuzu kila lisemwalo liwe headline???? Hayo ni mawazo yake in terms of priority na hakuna jipya ......nani asiyejua haya matatu ya elimu afya na kilimo yanategemeana kwa ukaribu?????

Hebu tuwe makini na kuweza kufanya upembuzi wa kauli sio kufuata tuuuuu
 
bot_tabimg.gif



Tuesday, 28 August 2012 20:59

lowassa-top-safi.jpg


ASEMA HATA CCM INAJUA MSIMAMO WAKE, WAZIRI KABAKA ASISITIZA KILIMO NI LAZIMA, PROFESA LIPUMBA, MBATIA WAMSHANGAA

Peter Edson

WAKATI Serikali ikielekeza nguvu nyingi kutekeleza mkakati wa kuendeleza sekta ya kilimo nchini uliopewa jina la Kilimo Kwanza, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ameibuka na kusema haungi mkono mkakati huo.Alisema mkakati huo wa Kilimo Kwanza umekosa mashiko hivyo ili auunge mkono, kuna haja ya kubadili dhana yake na kuwa, elimu kabla ya kilimo kwanza.

"Ni vyema nikaeleweka hapa. Ninachomaanisha ni kuongeza elimu katika Kilimo Kwanza ili wananchi wawe na elimu kwanza ndipo waweze kuboresha kilimo," alisema Lowassa.

Akizungumza katika Kipindi cha Dakika 45 kilichorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV juzi usiku, Lowassa alisema pamoja na Serikali kuwa na nia nzuri ya kumkomboa mwananchi kwa kuboresha mazingira ya kilimo, jambo hilo litakuwa si chochote kama hatapatiwa elimu itakayomwongoza kwenye mapinduzi hayo ya kijani.

"Mpango huu wa Kilimo Kwanza umekosa nguvu kwa sababu kuanzishwa kwake hakukuzingatia dhana ya ukombozi wa mwananchi wa kawaida. Tangu awali ndani ya chama (CCM) nilieleza kuwa sitaunga mkono hoja hiyo mpaka kuongezwe mashiko na kuwa Elimu Kabla ya Kilimo Kwanza," alisema Lowasa na kuongeza:

"Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alitoa uamuzi mgumu na wenye busara, ndiyo maana kilimo cha pamba, kahawa, mkonge na mazao mengine vikaanzishwa. Hivyo ipo haja ya kufanyika mchakato wa kuona mbali zaidi ili viongozi wetu waweze kutoa uamuzi sahihi katika hoja hii ya Kilimo Kwanza, kwani nguvu nyingi pasipo elimu inaweza kuligharimu taifa."

Alisema kuwa ili mwananchi wa kawaida aweze kunufaika na Kilimo Kwanza, anahitaji kupatiwa elimu ya kutosha ya namna ya kuandaa mazingira ya kilimo na uelewa wa vifaa na pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea na dawa.

Alisema pamoja na kuwa na mabwana shamba wachache, wananchi wamejikuta wakitumia mawazo yao kufanikisha miradi ya kilimo katika maeneo yao na matokeo yake wanapata mazao kidogo ambayo hayawakwamui kiuchumi.

Alitoa mfano wa nchi ya Indonesia akisema inaendesha uchumi wake kwa kilimo cha michikichi, ambayo mbegu zake zimetoka Tanzania... "Lakini Tanzania iliyotoa michikichi hiyo sasa ni moja ya wateja wa mafuta hayo yanayotoka Indonesia."

Alishauri Serikali kuanzisha mashamba ya michikichi maeneo mbalimbali nchini kwa kuwa ardhi ipo ya kutosha hivyo kujitosheleza kwa mafuta hata ya kuuza nje.

"Ningelikuwa na uwezo wa kutoa uamuzi, vijana wetu wa JKT (Jeshi la Kujenga Taifa), ningewapa kazi ya kuanzisha mashamba ya michikichi nchi nzima kwani nchi yetu imejaliwa kuwa na ardhi kubwa na yenye rutuba, mapori yapo mengi," alisema Lowassa.

Alisema wananchi wanaweza kupewa matrekta na pembejeo mbalimbali za kilimo, lakini bila kupewa elimu elekezi ya namna ya kuzitumia pembejeo hizo kuzalisha mazao bora, itakuwa kazi bure kwa kuwa ongezeko la mazao litakuwa dogo kama ilivyo kwa kilimo cha jembe la mkono.

Alitoa wito kwa Serikali kutumia fursa zilizopo za miradi ya kilimo kuwaelimisha Watanzania ili baadaye waweze kupewa au kukopeshwa zana za kilimo, akieleza kuwa nguvu kazi na elimu, ndivyo vitakavyomkomboa mwananchi katika umaskini wa kipato.

Kabaka: Kilimo lazima
Alipotakiwa kuzungumzia kauli hiyo, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka alisema kilimo ni lazima na Lowassa lazima akubaliane na mpango wa Serikali wa kutekeleza Kilimo Kwanza.

"Lowassa lazima akubaliane na msimamo wa Serikali wa kutekeleza Kilimo Kwanza. Kilimo ni lazima," alisema Kabaka na kuongeza kuwa sekta hiyo ndiyo inayotoa ajira kwa watu wengi kuliko nyingine.

Alisema Tanzania ina wahitimu zaidi ya 800,000 wa elimu ya juu wa fani mbalimbali ambao moja ya ajira ambazo wanapaswa kujiunga nazo ni kilimo na hakuna ambaye anaweza kutafuta elimu akiwa na njaa... "Serikali itaendelea kusimamia Kilimo Kwanza na tunamtaka Lowassa atuunge mkono."

Waziri huyo alisema Serikali haipuuzi elimu, lakini ukweli unabaki kuwa sekta ya kilimo ilisahaulika kitambo hivyo kupitia Kilimo Kwanza ukiacha ajira za wakulima wa kawaida, pia maofisa ugani wa kada mbalimbali wanaajiriwa.

"Hata huko kijijini huwezi kusema unampelekea elimu mtu ambaye ana njaa. Huwezi kueleweka, lakini tunajua watu wakishiba wataweza kufanya mambo mengine hivyo kauli yake kuwa kwanza ingetolewa elimu haina tija," alisema.

Profesa Lipumba, Mbatia wamshangaa

Kauli hiyo ya Lowassa imeonekana kumkera mchumi maarufu nchini na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia. Kwa nyakati tofauti jana, viongozi hao wa vyama vya upinzani walihoji mamlaka ya kimaadili aliyonayo Lowassa ya kusema hayo.

Profesa Ibrahim Lipumba alimponda akisema anachofanya kada huyo wa CCM ni kujipapatua kisiasa kwani Kilimo Kwanza ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Profesa Lipumba alisema kauli hiyo ya Lowassa inaonyesha kana kwamba hafahamu vizuri mkakati huo wa Kilimo Kwanza hivyo ni bora akachukua muda kujifunza kabla ya kutoa kauli hizo.

Profesa Lipumba alisema katika kutekeleza Kilimo Kwanza, elimu pia hutolewa hivyo haiwezekani kusema kuwa itolewe kwanza elimu kabla ya kutekeleza mpango huo, kwa kuwa vyote vinakwenda pamoja.

"Huwezi kusema kuwa eti utoe elimu kwanza kisha ndiyo uanze utekelezaji. Hivi vyote vinatakiwa kwenda pamoja labda kasoro zilizopo ni kuwa Kilimo Kwanza kimewalenga wakulima wakubwa wakitarajiwa wawainue wadogo jambo ambalo haliwezekani," alisema.

Alisema utekelezaji wa Sera ya Kilimo ni jambo jema kutokana na ukweli kuwa katika kipindi cha zaidi ya miaka 10 iliyopita, wakulima wamesahaulika na kufanya ukuaji wa kilimo kuwa asilimia nne, kiwango ambacho ni cha chini kwa mahitaji ya ongezeko la watu ambalo ni wastani wa asilimia moja kwa mwaka.

"Kilimo ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa taifa lolote duniani na kitendo
cha kuwategemea wakulima wakubwa ni kasoro ambayo inapaswa kufanyiwa kazi katika utekelezaji wa mpango huu wa Kilimo Kwanza," alisema Profesa Lipumba.

Mbatia alisema anamshangaa Lowassa kupingana na uamuzi wa chama chake kwa kuwa mkakati wa Kilimo Kwanza ulipitishwa na chama chake... "Lowassa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, hivyo Kilimo Kwanza ni uamuzi wa CCM. Anapingaje wakati hata alipojiuzulu alisema anafanya hivyo kulinda masilahi ya chama, leo anapinga mipango ya chama hichohicho?"

Alisema kama anaona haendani na mambo yanayofanywa na CCM ni vyema ajiondoe na kujiunga na chama kingine au kuanzisha chake ili awe na fursa nzuri ya kupinga kazi za chama tawala.

Ajira
Lowassa pia alizungumzia suala la ajira akisema viwanda vikifufuliwa vitanufaisha Watanzania wengi kwa kupata ajira na hivyo kuondoa dhana ya kuwepo kwa wahitimu wengi wa vyuo vikuu wasiokuwa na ajira.
"Unapotangaza kazi ya watu 20, barua za maombi ya kazi zinakuja 2,000, tusisubiri maandamano, tutatue tatizo hili sasa," alisema Lowassa na kuongeza:

"Hili suala linahitaji ufumbuzi wa haraka ingawa tumechelewa. Nilimshangaa sana yule waziri niliposema kuna shida ya ajira, akasema hakuna tatizo hilo."

Tangu mwaka jana, Lowassa amenukuliwa na vyombo vya habari mara kadhaa akisema ukosefu wa ajira kwa vijana ni tatizo kubwa nchini, akilifananisha na bomu linalosubiri kulipuka ikiwa halitatafutiwa ufumbuzi.

Hata hivyo, Machi 21 mwaka huu, Kabaka katika mkutano na wanahabari alipinga kauli hiyo ya Lowassa akisema:

"Hali halisi ya ukuaji wa uchumi nchini ni nzuri lakini, haiwezi kuonekana kama wananchi wake ni maskini na hawana ajira. Hata hivyo, Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kushughulikia suala hilo ikiwamo la kuhimiza uwekezaji nchini," alisema Kabaka na kuongeza:

"Kitendo cha wanasiasa kuendelea kusema tatizo la ajira kwa vijana ni bomu linalosubiri kulipuka, siyo kweli na kudai Serikali haijafanya kitu wanakuwa hawaitendei haki. Tatizo limepungua kutoka asilimia 12.9 mwaka 2000/01 hadi asilimia 11.7, mwaka 2006.

Mbio za urais 2015
Alipotakiwa kueleza iwapo ana mpango wa kuwania urais mwaka 2015, Lowassa alisema suala hilo halipaswi kuzungumzwa sasa kwani linaweza kufungua uwanja wa malumbano.

"Waingereza wana msemo mmoja unaosema, ‘tutavuka daraja tutakapolifikia.' 2015 bado ni mbali ukisema chochote sasa utafungua uwanja wa malumbano, tusubiri 2015 bado ni mbali," alisema Lowassa.

 
attachment.php

Hii ndio maana halisi ya kilimo kwanza kwa upande wa CCM wananchi tuliwaelewa vibaya
 

Attachments

  • toyota-land-cruiser-v8-03.jpg
    toyota-land-cruiser-v8-03.jpg
    67.9 KB · Views: 127
Huyu anatafuta political credit tu kwanini hayo na mengine yale ya gesi hakuyasema bungeni kwenye hotuba Bajeti za serikali kama anaitakia mema kweli nchi?
 
Angeendelea na uwaziri mkuu, tungekuwa tunapata mvua kila siku. Si unajua alishawaleta wataalam wa kufanya feasibility study ya kutengeneza mvua maabara kutoka Malaysia?
 
Pamoja na mtizamo hasi nilionao juu ya EL, hasa ambitions zake za kutaka kwenda Ikulu, lakini katika hili naona angalau anaanza kuleta mabadiliko katika siasa zetu....yaani mipambano ya kisera zaidi kuliko kung'ang'ana na siasa za maji taka.
 
baada ya kumsikia mbowe

acha upashukuna dogo fatilia siasa vizuri ndio useme,ukweli ni kwamba swala la elimu EL hajaanza leo bahati mbaya wewe ndo umeanza leo sinc alivyoachia upm akihojiwa na tido alilisema bila kificho.
sory for you kujua siasa za bongo ukubwani
 
Jana nimeangalia kwenye TV TBC, Lowasa alikuwa anapinga initiative ya rafiki yake kuhusu kilimo kwanza, anasema yeye anaamini elimu kwanza, kilimo baadae, inawezekana akawa na point, lakini mbona hakuyasema haya alipokuwa serikalinini? make wimbo wa kilimo kwanza JK kauanzisha siku nyingi.

Wakati Mhe. Rais Kikwete anasema Kilimo Kwanza na Lowasa anasema Elimu kwanza.., Prof Mark Mwandosya alivyopona na kurudi Bungeni mojawapo ya kauli za mwanzo kabisa baada ya salamu alisema AFYA KWANZA jamani. Huwezi kufanya kilimo wala huwezi kupata elimu bila kuijenga afya yako.
Rais Kikwete kweli alithibitisha muda mfupi uliopita kwamba elimu si kipaumbele na walimu hatuwezi kuwalipa zaidi ya walipavyo sasa, na akaoneshsa wazi kwamba hata Afya si kwanza...madaktari mkiona mnalipwa kidogo, ruksa kwenda popote mnapoweza kulipwa zaidi!!

Sasa bora nini kiwe kwanza? Imebaki kwa wananchi wenyewe kuamua.
 
Elimu ipi anayoongelea? wakati wote katika nyazifa alizoshika ameendeleza vipi Elimu? Anajua wazi kuwanjima watanzania Elimu ndio nguzo ya CCM kuwatawala na kuwakandamiza watanzania. Mwanya Kidogo uliotolewa sasa wa elimu kwa watanzania hasa mjini kumefungua wengi na kuongeza changamoto katika upinzani. Unafikiri Lowasa atatekeleza hayo anayoyasema?
 
Ndugu yangu weee, naona huwa hufuatilii mambo ya siasa kwa muda mrefu. Utakumbuka wakati Lowassa ni Waziri mkuu alivalia njuga shule za sekondari za kata. Baada ya Kikwete kuona anamfunika kwa kung'aa sana wakamzushia zengwe la Richmond ndo ukamshusha kutoka kwenye Uwaziri Mkuu.

Nikikuuliza ni maamuzi gani ya mawaziri yanapita kama kikwete hajui huwezi kuniambia hata moja kwa maana ya kwamba; maamuzi yote ya Baraza la Mawaziri kikwete ndo mweyekiti wa Vikao sasa iweje Richmond iwe ya Lowassa peke yake?? Kwanza Lowassa hayupo kwenye Richmond, Richmond ni ya KIKWETE NA MAKATIBU WAKUU KWA Taarifa yako wakishirikiana na Rostam Aziz.

Nyota ya Lowassa iling'aa sana wakaizima kwa tuhuma za uongo.

Mbona wewnye tuhuma za kweli za rada, tanesco na zingine hawashuulikiwi?? Ni kwa vile hawajang'aa wakampita Kikwete. Ona wanavyomzima Membe...... Shauri yako ndugu soma alama za nyakati
 
Wakati Mhe. Rais Kikwete anasema Kilimo Kwanza na Lowasa anasema Elimu kwanza.., Prof Mark Mwandosya alivyopona na kurudi Bungeni mojawapo ya kauli za mwanzo kabisa baada ya salamu alisema AFYA KWANZA jamani. Huwezi kufanya kilimo wala huwezi kupata elimu bila kuijenga afya yako.
Rais Kikwete kweli alithibitisha muda mfupi uliopita kwamba elimu si kipaumbele na walimu hatuwezi kuwalipa zaidi ya walipavyo sasa, na akaoneshsa wazi kwamba hata Afya si kwanza...madaktari mkiona mnalipwa kidogo, ruksa kwenda popote mnapoweza kulipwa zaidi!!

Sasa bora nini kiwe kwanza? Imebaki kwa wananchi wenyewe kuamua.
Amebaki kuua watu wasio na hatia kwa kutumia polisi wake. Unajua ndugu hawa watu wanataka tusipate elimu ili waendelee kututawala kipuuzi. Wanataka kuwa madarakani kwa kuongoiza wapumbavu kumbe wameshachelewa, yaani wanavuta shuka kumekucha au wanaloga kweupe na tumewaona hawa maforong'ong'o wa CCM - Chama Cha Majizi
 
Elimu ipi anayoongelea? wakati wote katika nyazifa alizoshika ameendeleza vipi Elimu? Anajua wazi kuwanjima watanzania Elimu ndio nguzo ya CCM kuwatawala na kuwakandamiza watanzania. Mwanya Kidogo uliotolewa sasa wa elimu kwa watanzania hasa mjini kumefungua wengi na kuongeza changamoto katika upinzani. Unafikiri Lowasa atatekeleza hayo anayoyasema?

Lowassa alikuwa ameanza vizuri wakamziba mdomo kwa kumsukia zengwe la Richmond. Mbona kina Chenge, Karamagi na wengine hawaguswi??? Mbona Ngeleja anakula kuku na mgao wake feki?? Mbona maige naye yupo uraiani na nyumba yake ya dola 700,000 hamsemi??? Lowassa tu na Richmond!! Mpeni Urais muone atakavyorudisha hizo hela zilizoko Uswis, na uone watu watakavyohama nchi hii kwa kuogopa mahakama. Acha bwana Lowassa Mwanaume wewe.
 
Ulimboka kapona ndiyo tunashukuru, lakini atuambie yaliyomsibu na si afiche uovu wa hawa manyani waliomfanyia unyama. Sisi tunajua anawajua na sipowataja kwa kweli tutajua kapewa rushwa na ile sala ya toba aliyoongozwa itakuwa bure kwa sababu amepokea rushwa kuficha uovu ambao Mungu alitaka wananchi wote wajue ni viongozi gani walionao, viongozi wasiopenda ukweli na haki kwa watu wake.

ULIMBOKA FUNGUKA YEBO. POLE LAKINI USIPOFUNGUKA UMEKULA RUSHWA AKI YA MUNGU
 
Yeleuuuuuuuwi

Jk = kilimo kwanza
Lowasa = elimu kwanza
Membe = Lake nyasa kwanza

mbona sisi hatusemi?
 
Lowassa alikuwa ameanza vizuri wakamziba mdomo kwa kumsukia zengwe la Richmond. Mbona kina Chenge, Karamagi na wengine hawaguswi??? Mbona Ngeleja anakula kuku na mgao wake feki?? Mbona maige naye yupo uraiani na nyumba yake ya dola 700,000 hamsemi??? Lowassa tu na Richmond!! Mpeni Urais muone atakavyorudisha hizo hela zilizoko Uswis, na uone watu watakavyohama nchi hii kwa kuogopa mahakama. Acha bwana Lowassa Mwanaume wewe.

Hana jipya. Ungekuwa umefunguka kielimu husingetoa hoja kama hiyo. Lowasa ameshika nyazifa nyingi ambazo tungeshaona Kilio chake katika kuendeleza Elimu. Kuhusu kurudisha waliopeleka fedha Uswiss kamwaleze arudishe kwanza zile za EPA alizopitishia kwa wale walioingiza gari na Ndege. Watanzania wako kimya lakini wanajua mengi. Pole kunyima watanzania elimu ni mtaji wa CCM
 
Back
Top Bottom