Kikwete kilimo kwanza, Lowassa elimu kwanza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete kilimo kwanza, Lowassa elimu kwanza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jack Beur, Mar 16, 2011.

 1. J

  Jack Beur JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Jana nimeangalia kwenye TV TBC, Lowasa alikuwa anapinga initiative ya rafiki yake kuhusu kilimo kwanza, anasema yeye anaamini elimu kwanza, kilimo baadae, inawezekana akawa na point, lakini mbona hakuyasema haya alipokuwa serikalinini? make wimbo wa kilimo kwanza JK kauanzisha siku nyingi.
   
 2. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa mtu yoyote mwenye akili timamu, huwezi kusema kilimo kwanza ndiyo kinachoweza kuinua maisha. Mimi ninamuunga EL 100% elimu kwanza.
   
 3. S

  Strategizt Senior Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 176
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli kilimo bila elimu kwa upande wangu naona kama tutakuwa hatujafanya lolote katika karne ya Sayansi na Teknolojia!!!
   
 4. B

  Bobby JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Halafu hicho kilimo kwanza chenyewe ni cha kutegemea mvua na vocha zake za pembejeo ndio hizo mafisadi wanagawana mabilioni mfano mmojawapo ni huko anakotoka pm, watu wametafuna vocha mpaka wakavimbiwa. Hiki ni kilimo zero si kwanza. When will we be serious?

  Nakumbuka 2006 tuliahidiwa kuwa mgao wa umeme soon utakuwa historia, 5 years later tunauliza utekelezaji wa ahadi yetu tunaambiwa yeye si mvua. So ulipoahidi ulikuwa mvua au? Hukuliona hilo ulipoahidi kwamba hukuwa mvua so ulipaswa kuwa na njia mbadala ndio utoe ahadi?
   
 5. shemasi

  shemasi Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safari ya kuelekea ikulu ni ngumu hivyo yamuhitaji amponde hata rais wa sasa ili kufanikisha ajenda yake.wananchi amkeni msije ingia kwenye huu mtego.
   
 6. o

  oyoyoo Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama tutabakia na ufupi wa kufikiri kwamba kila jambo zuri linasababisha mtu kuwaza kuwania madaraka bila shaka hata wewe tutasema unawaza safari ya 2015. Hoja aliyotoa ina mantiki maana nani hajui kuwa shule za kata ziliachwa na kutelekezwa kwa kuwa watu fulani walikuwa wakisema unajua shule hizi zikifanya vema atapata credit Lowassa. Kwani huna taarifa kuwa hilo ndilo lililozaa Kilimo Kwanza ikiwa ni lengo la kusahaulisha Elimu kwanza ambayo ndiyo ilikuwa sera ya kwanza ya wamu hii. Hate him but his credit muachie.
   
 7. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  siungi mkono hoja hii kwani suala la shule za kata changamoto zake zajulikana na naamini with tym zitaisha.naomba ujue lowassa hana nia njema kwa sisis wananchi kwani nia yake ni urais tuu.atasema lolote kutulaghai ili aingie magogoni.
  ina maana hakuna watu wasafi hadi tumflash lowasa aingie ikulu?
   
 8. Paddy

  Paddy JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 273
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Nchi zote duniani zilizoendelea zina kauli mbiu za Elimu kwanza isipokuwa vinchi masikini kama Tanzania. Chama cha Conservative uingereza katika uchaguzi kilisema priority yake ni education education education. Sisi eti kilimo kwanza, kitainua uchumi wetu na maisha bora namna gani? Afya itaboreshwa vipi na kilimo? Lakini education ndiyo msingi wa kuboresha sekta zote ikiwapo hicho hicho kilimo. Need we say more than JK being a lazy thinker??

  http://www.thesun.co.uk/sol/homepage/news/2812399/Conservative-leader-David-Cameron-education-vow-in-election-fight.html
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Lowasa anajitahidi kujisafisha wee lakini wapii!
  Ninachomsifu huyu jamaa huwa hakati tamaa.
   
 10. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ni kweli lowasa alikuwa na maovu yake tena mengi tu ila ukwel si kwamba hakuwa na mazuri na alipokuwa madarakani aliisimamia elimu na hasa katika shule za kata hata kama hazina mafanikio makubwa lakini zitakuja kutengemaa hapo baadae lakini kuliko ubaya wa wake unalinganishwa na kilimo kwanza?


  Kilimo kwanza cha jk ni hofu ya kuporomosha uchumi ukizingatia unalima nini? nani mkulima wa leo nyakati ambazo wimbi la vijana lipo mjini? mazao gani na yenye tija gani? hayo mazao unauza wapi,kwa mlaji wa ndani au nje? miwa inalimwa wapi na sukari anakula nani? na anayekula sukari ni kwa bei ipi? hizi ruzuku zinashusha uchumi na ni bora ziwekezwe kwenye elimu.


  Jk anashindwa kuelewa hata huko china, ufilipino na vietnam walijua kilimo ni kukuza uchumi ila leo hii bado wanazo fikra hizo? au wamebaki kupindua muono upande mwingine? mawazo yake ni sahihi lakini naona hayana tija kabisa......elimu kwanza ni best ila ni lazima pia iwe na tija.


  mipango bora ni kujifunza hata kwa wengine
   
 11. Dinipevu

  Dinipevu Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 25
  Goood......na wakati mwingine tujfunze kutoka kwa watu wanaojua mambo zaidi yetu,kwa mfano Netanyahu wa Israeli alikuwa waziri mkuu hapo kale ya zamani na muda wake ulipoisha alirudi hadi ngazi ya ubunge na sasa tena amerudi na anafanya kazi vizura hata kama kuna sehemu ailjikwaa na kuteleza si sababu ya yeye kutotoa mchango wa kimawazo katika jamii na kama tutafanya hivyo basi ni kusema tuna tatizo hasa katika kipengele cha fikara yakinifu.  hakuna kibaya milele na kizuri pia.
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Anajisafishia njia....
   
 13. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,875
  Likes Received: 2,817
  Trophy Points: 280
  Katika hilo nakubaliana na Mh. F***di, hata wakati wa u-PM wake yeye alikuwa kwenye Elimu. Tukumbuke jinsi alivyokuwa anawaweka kitimoto wakuu wa Mikoa na Wilaya kwenye ziara zake kama akikuta masuala ya Shule za Kata yanalegalega. Hivyo priority ya Mh. Fi***d ilikuwa Elimu. Hili la Kilimo Kwanza lilianza kwenye hotuba moja ya Mkwere kwenye sherehe za nanenane, hapo PM wenu mchovu ndo akalidaka kila alikopita Kilimo kwanza, kilimo kwanza, kilimo kwanza!! Upuuzi mtupu!! Nchi gani iliyoendelea kwa kutegemea kilimo na kusahau Elimu?

  Tunakuunga Mkono EL kwa kuweka bayana kwamba kipaumbele cha wilaya ya Monduli ni Elimu. Abarikiwe aliyesema kipaumbele chake cha kwanza ni Elimu, cha pili ni Elimu na cha tatu ni Elimu!!! Pinda wewe ubongo wako ume-Pinda hata tufanyeje huwezi kutusaidia!!!
   
 14. N

  Ntandalilo Member

  #14
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama nimesoma mada vizuri ni kwamba EL anaamini but hajapinga kuhusu kilimo though ndo kupinga ki utu uzima huko............ anyway naamini hivyo pia and for that go Lowassa go man !!!
   
 15. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,183
  Likes Received: 1,184
  Trophy Points: 280
  Sikubalian na wewe hata kidogo, rafiki jielimishe na uboreshe kumbukumbu zako.
   
 16. N

  Nenetwa Member

  #16
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Katika bajeti ya Tanzania, tunaambiwa Elimu inaongoza kwa kupewa fedha zaidi ktk bajeti, hapa napata wazo la Elimu Kwanza (ili hali ubora bado duni), lakini upande wa pili, viongozi wetu wa juu serikalini wanatuhubiri Kilimo kwanza, hapa tena napata wazo la Kilimo kwanza (ili hali bado kilimo kinategemea mvua)
  Mkanganyiko huu wa nini hasa ni priority number one, unatuchanganya na tunashindwa kujua nini hasa ni "Kwanza" hapa Tanzania, na wapi hasa wananchi waelekeze nguvu na rasilimali zao! Hii inapelekea kushindwa kuonesha ufanisi. Ni vizuri PRIORITY NUMBER ONE, ikaelezwa na vitendo endelevu vikafanywa!
  Bajeti inaonesha Elimu ni ya Kwanza. Viongozi wanahubiri Kilimo Kwanza, Mtanzania anakoseshwa msimamo!
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lowassa kama kweli anaamini Elimu kwanza mbona naye kenda Lokiondo?...Au ndio hiyo imani ya kiroho iko juu ya elimu.
   
 18. S

  Seacliff Senior Member

  #18
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Kwani hatuwezi kuweka priority kwenye sera zote mbili? My take is that they are both right! Tuweke elimu mbele kwa watoto wetu lakini kilimo bado kibakie uti wa mgongo wa Tanzania!
   
 19. S

  SUTU BUTUGURI Member

  #19
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  No. To both, KIKWETE & LOWASA ufisadi kwanza ...
   
 20. k

  kayumba JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tukijakufika 2015, tutaona na kusikia mengi sana!

  NARUDIA;
  Nitakuwa wa mwisho kuaamini nia njema ya huyu jamaa kwa waTz PERIOD
   
Loading...