Kikwete kavutwa naye amevutika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete kavutwa naye amevutika

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Oct 11, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kikwete kuanza kuzungumzia maneno ya uchochezi ya kumwaga damu siku moja baada ya kusambazwa inaashiria kitu gani? Lini kafanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa si maneno ya kubuni. Je tukisema anahusika na kuyaandaa ili aje kuyatumia kisiasa tutakuwa tunamwonea?

  Inaonyesha amemaliza ahadi zote na kuanza kujiingiza kwenye siasa za maji taka kama katibu wake Mkuu. Ndugu wana jamvi mimi nina wasiwasi na Kikwete kuwa ni mmojawapo wa walioandaa maneno hayo kwa jinsi alivyoyachukulia upesi upesi na kuanza kuyatumia majukwaani.

   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nimesikia amezungumzia hilo kwenye kampeni zake huko Songea.

  Jamaa ana matatizo kweli.

  Hivi mtu kama huyo utamtofautishaje na watu wa taarabu? Akisikia umbea anaugeuza kuwa kweli na kuuhubiri.

  Au anaangalia na hadhira wanaomsikiliza?

  Hebu akaseme maneno hayo Mbeya, Moshi au hata Iringa kama hajapigwa mawe.
   
 3. minda

  minda JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  ningekuwa makamba ningemshawishi m/kiti wangu wa ccm(T) turuhusu wangombea wetu kushiriki katika midahalo mbalimbali kwa sababu inaonekana chama chetu kimekataa majadiliano ya hadharani na kujibu na kuanzisha majadiliano mengine gizani.
  hata kama chama chetu hakihusiki na kampeni hizo chafu za;
  • udini
  • ukabila
  • rangi
  • umwagaji damu
  lakini mazingira yanaonesha kwamba sisi kama washika mpini tunahusika kwani wahusika mbalimbali wamenywea kusema chochote kama ilivyo kwa ile msg ya private no. in red call.
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mkulu kanasa kwenye mtego alioutega
  Mungu atunusuru
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Kikwete mdini wa vitendo kawaahidi mengi waislamu ndiyo maana waislamu walitamka wazi kuwa hawatoip[igia kura ccm na kikwete kwa kuwarubuni waislamu lkn kuna habari za uhakika kuwa kikwete kawatuliza waislamu wanyamaze kimya kwanza achume kura za wakristo alafu ataweka mambo yote sawa baada ya uchaguzi..................


  Hamjiulizi kwa nini waislamu wametulia alafu wanajistukia kwa kudanganya umma kuwa kuna wagombea wanataka udiini wkt wanajua fika kuwa kikwete ndiye mdini kwa vitendo?
   
 6. h

  hagonga Senior Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kauli hizi za umwagaji damu mimi ndio naskia kwake, hivyo ndiye mtoa hoja wala asiwasingizie wapinzani.
   
 7. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  unajua mkuu wetu ni wa lile kabila la wanataarab kwa hiyo msimshangae kama aliweza kuwashushia wafanyakazi maneno ya taarab (wanafki,wazandiki hawana lolote wana lao jambo bila kusahau enyi mbayuwayu mimi ndo mwajiri wenu) hayo mimi wala siyashangai ila ni hatari kwelikweli
   
 8. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Shimbo kasema habari ya kumwaga damu
  Mashehe wanasema habari hii hii
  Sms za kijana wake Miraji zisema haya haya
  Sasa JK kajiunga na wimbo huu

  Kwa nini wasiwakamate na kuwahoji waliosema hayo ya kumwaga damu kama wapo? Slaa aliwaagiza na kuwapa siku 7 ili hao wachukuliwe haraka hatua za kisheria.

  Mpaka hapa mimi naona ni maneno ya kutungwa na kwa hiyo ni uchochezi.
   
 9. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Haitakuwa sahihi na wala haki kulinyamazia hili la JK kudai kusoma taarifa za gazeti fulani(angelitaja walau) kwamba kuna watu wanatishia kumwaga damu. Ningekuwa na uwezo ningewakutanisha wapinzani wote tuandae maandamano ya amani kupinga kauli ya JK na kumtaka kama Raisi ambaye bado yuko madarakani hadi 31 Octoba, kumchukulia hatua huyo ambaye anatishia amani ya taifa hili. Ningefanya hivyo mapema kabla ya uchagui kuhakikisha hali hii tete haitatokea (pre-empty the situation). Lakini uwezo huu maskini sina!
   
 10. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  kama kuna mtu anayewaza kumwaga damu ni yeye mwenyewe kikwete maana nina uhakika hatokubali kushindwa ikizingatiwa kuwa redet na synovate wamepika research ambazo sampling zake wamezifanyia lumumba street na kwenye lango la shoprite supermarket
   
 11. F

  Froida JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  KIKWETE ni mbaya sana anachochea tuingie kwenye vita ni mtu hatari sana huyo nakumbaka Sumaye alivyosema mtu anayeingia IKULU kwa karamu hata taka kutoka milele kwa namna nyingine atuaminisha kwamba atatumia majeshi kuua wananchi ili awe Raisi kipindi cha pili,Watanzania tungemsikiliza Mwalimu Nyerere huyu mtanzania mwenzetu hakufaa kabisa kupewa nafasi hiyo angalia sasa anakopeleka nchi yetu,
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nimeshangazwa sana na kauli yake hiyo.
  Tukapige kura dhidi yake naamini Mungu atatunusuru.
  Pia ameanza kuwatumia kisaikolojia wenzetu waislam. maana kuna kauli wamezitoa hapa karibuni mpaka najiuliza kama kweli hawa walikaa chini na kujadili au chama tawala kimeamua kuikumbatia dhambi aliyowaasa Baba wa Taifa (malumbano ya kidini).

  Sikuona popote kakobe akipiga kampeni za kidini kuhusu wagombea na kuchochea watu wachague kwa misingi ya udini. Nadhani CCM imewauma sana kuona kuwa siku ya jumapili watu watasitisha ibada na kwenda kuchagua viongozi huku wakiwa na maamuzi mazito moyoni.

  Watanzania, tuepuke watu wanaotumia mbinu chafu kutuvuruga, kutugawa na kututumia kama mitaji ya kisiasa. Hata akishuka malaika leo na kuanza kupandikiza chuki baina yetu ni wajibu wetu kumtokomeza na kumpuuza kabiza. Inawezekana mtu akawa kiongozi lakini asiwe mmoja wetu ktk kusimamia misingi ya taifa letu.

  Lazima tuseme hapana
   
 13. M

  Mikomangwa Senior Member

  #13
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nimeshangaa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawaonya wafuasi wake kuwa wapinzani wako tayari kumwaga damu. Kama kweli Kikwete ni mcha Mungu basi amwogope sana Mungu wake. Neno damu linatisha masikioni mwa watu. Kadiri anavyolitamkatamka litaanza kukomaa miongoni mwa raia na hatimae watu wakajiandaa kumwaga damu. Dr Slaa usijiingize sana huko kwa kuwa Mungu ni mwema sana kiasi kwamba mawazo ya Kikwete si mawazo ya Mungu. Na vita ya ukombozi wa mwanadamu siyo vita yako Slaa, ni vita ya Mungu mwenyewe kwa kuwa ameona watu wake wanavyozidi kuangamia. Mbinu chafu hazitashinda bali kweli na haki itasimama milele. Mungu tupiganie na taifa lako litasimama.
   
 14. Azadirachta

  Azadirachta Senior Member

  #14
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkulu wakati mwingine hutumia Udongo badala ya Ubongo!
   
 15. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Dr. Slaa wewe ni mkristu uliyepikwa katika Imani thabiti: mpende bwana mungu wako kwa moyo wako wote na kwa akili yako yote:mpende na jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe.Tunakuomba uamini katika hili na Mungu atakusaidia na sisi tunaamini hauko kwa ajili ya kuhamasisha kumwaga damu ,bali uko kwa ajili ya kulikomboa Taifa la Mungu la Tanzania.Udumu katika sala na maombi mungu yuko pamoja nawe na watanzania wako pamoja na wewe
   
 16. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Akihutubia mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea jana, Jumapili, Oktoba 10, 2010, Rais Kikwete amewasuta wanasiasa ambao wamekuwa wanatishia umwagaji wa damu nchi kama hawakufanikiwa kushika nafasi za uongozi wanazozitaka.

  "Sisi ni CCM. Sisi ni chama kisichohubiri umwagaji damu. Sisi ni chama cha amani. Umwagaji damu hauna maslahi yoyote na wala tija kwa yoyote isipokuwa kwa wanasiasa wanaotaka kutumia maiti za watu kama ngazi ya kuingilia Ikulu," amesema Rais Kikwete na kuongeza:

  "Hawa siyo watu. Hawana maana yoyote. Achaneni nao watu wa namna hii wanaotaka kupata madaraka kwa ngazi ya maiti za wananchi wasiokuwa na hatia."

  Amesisitiza Rais Kikwete: "Wanachochea watu wamwage damu na wao wapande ndege kwenda zao Ulaya na kuwaachia nyie mkitoana damu."

  My take: Haya ni maneno mazito kutamkwa na kiongozi hasa rais wa nchi. Kikwete kama rais alitakiwa akemee message hizo na wanaozisambaza kwa kuwa zinachonganisha watu badala yake yeye bila kufanya utafiti kama yaliyotamkwa ni ya kweli au la anaanza kuzitumia kama mtaji wa kisiasa. Inawezekana anajua zinakotoka.
   
 17. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Pole, usijali yatakwisha haya siku moja.
   
 18. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hizo message anatuma yeye sio anajua zinakotoka, hii sio coincidence, yaani message leo kesho anatamka hayo hayo, kuna walakini
   
 19. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,653
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Kama kuna damu itakayomwagika kutokana na uchaguzi huu basi Jakaya Mrisho Kikwete ataibeba kichwani mwake kwa siku zote za maisha yake kwani ni yeye anapanga umwagaji huo wa damu kwa kupanga kuiba kura ili atangazwe kuwa mshindi wa zaidi ya 80%. Wewe Kikwete na mahench men wako hamtakwepa hasira ya Mungu kwa kumwaga damu ya watanzania wasio na hatia
   
 20. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mama yangu weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.maneno haya yametoka mdomoni mwake kweli?Yaani jamani afadhali mungu akunyime utajiri akupe akili...Wapi palipohubiriwa umwagaji wa damu?kweli kikwete umeishiwa ,khaaa this is very low for you...wewe si ndo unatuma majeshi yatishe watu wewe,synovate na REDET na tafiti zao za makengeza..mbona una hofu sana mwanakwetu...kaa utulie kushindwa ni kawaida TZ ya leo sio ya 2005....wewe watu hawakupendi na hawakutaki kwa kuwa serikali yako longolongo au nalo hulielewi
   
Loading...