Kikwete kashituka, anaweza kupunguza makali lakini kukwepa kabisa ni ngumu

UWEZO_WAKO

Member
Nov 17, 2010
39
4
Kikwete alitegemewa na wengi kuwa raisi toka 1995 lakini Nyerere alikuwa na mtazamo tofauti na hivyo kutokana na ushawishi wake mkubwa akafanikiwa kumwekee ngumu. Basi Mkapa akawa rais (1995-2005). Kwa Mkapa wengi wanaamini alifanya vizuri kipindi chake cha kwanza (1995 - 2000)hasa miaka ya mwanzo ambapo Nyerere alikuwa bado hai, lakini wengi pia wanaamini alifanya vibaya sana kipindi chake cha pili (2000 - 2005) na hata yeye mwenyewe kuitwa fisadi. Baada ya kustaafu wanachi hawakutaka hata kumuona kabisa, mzee wa watu akawa anajificha.
Kikwete alipopata urais wengi walikuwa na matumaini kwake na hata hotuba yake ya kwanza ilibeba matumaini makubwa kwa wananchi, maisha bora kwa kila mtanzania, kwa mfano. kujua uchumi umekua kwa serikali yake ni mtu aseme nilikuwa nakula mlo mmoja lakini sasa nakula milo 2,.. nk. Jamaa naona naye karudi kwenye kutumia statistics ambazo haziendani na hali halisi. Lakini zaidi serikali yake imelaumiwa sana kwa ufisadi, hili limempa Mkapa na Sumaye kuona hata wao pia si wabaya sana wameanza kuonekana onekana na hata kukaribishwa na kuwa karibu na Kikwete. Sasa naona kwa tabia hii ambayo wananchi wameianzisha ya kutotaka kuwaona na wakati mwingine hata kuwachukia viongozi wanaorudisha nyuma maendeleo yao, Kikwete namuona kuingia katika kundi hilo mara baada ya kumaliza uongozi wake 2015. Hasa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni bila kujali zitatimia vipi ili mradi tu ahakikishe anashinda kuna uwezekano mkubwa zisitimizwe. Kwenye hotuba yake uzinduzi wa bunge jipya hata hotuba yake pia inaonyesha kashituka hata kuiweka vizuri kwani ilikuwa ya jumla jumla sana na pia ya kukata tamaa maana anasema yapo mengi ya kuyaongelea lakini muda hautoshi... hivi hakujua kuwa hotuba yake inahitaji muda gani kukamilika au sehemu nyingine aliyoiacha ilikuwa inawahusu wabunge wa CHADEMA na kwa kuwa hawakuwemo ikamchanganya.
Anayo nafasi ya miaka 5 huenda akafanikisha na baraza lake jipya kuwapunguzia watanzania magumu ya maisha, lakini namuona kama mtegemewa kundi la wanaokimbiwa na wananchi. Unajua sasa hivi huwezi kuiona vizuri kwa sababu yuko serikalini na anavyo vyeo/nafasi nyingi za kuwateua watu na wengi kwa kujua amevishikilia hivyo wanavihitaji wanalazimika kumpamba (mpaka aliposhituka wakati wa kampeni na uchaguzi ulioisha) lakini atakapotoka na kukabidhi dhamana zote kwa mtu mwingine hapo utaona hata wa chama chake watakaposema hata ikiwezekana naye ahojiwe kwa nini hakuwashughulikia mafisidi wa EPA, huyu inawezekana yumo pia. Hivyo ndivyo watakavyosema, kwani hata kwa Mkapa ilikuwa hivyo. Mwalimu wengi walimlilia kwa ajili ya usafi na uadifu wa uongozi wake hata pale alipofanya vibaya watu hawalaumu kwa sababu hakufanya hivyo kwa maslahi ya mtu au kikundi fulani inachukuliwa ni makosa ya kawaida kwani naye ni binadamu. Kiongozi bora ni kama rafiki wa kweli ni vigumu kumpata, haiwezekani kumuacha, Mwalimu mwana wa Afrikaka kamwe hautasahaurika.
 

RealMan

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,367
1,386
Uchambuzi wako umetulia. Viongozi wetu hawana nia ya kumkomboa Mtanzania na hata wanapogombea hizo nafasi si wote wenye malengo sahihi (clear vision) ya nini anataka kutimiza iwapo atafanikiwa kupata uongozi
 

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
14,376
12,763
Kama ana dhamira ya dhati atafanikisha malengo.
ila kama atadumisha hulka ya "MIMI NI RAIS WENU MTAKE MSITAKE" mjue hatoweza kufikisha hata nusu ya robo ya malengo aliyojipangia.
 

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,080
6,030
EL, Rostam na Chenge ndio wanaoendesha nchi - tegemea matatizo zaid ya yale ye 2005 - 2010. Kwanza wananchi walikwishamtoa tatizo ni Lewis kumchomeka hapo.
 

Super Glue

Member
Nov 24, 2010
9
1
Naikubali analysis yako uwezo-wako, ila kwenye demokrasia ya kweli wananchi sio tu wanamnunia mtu anaewa boa bali wanaweza kumtosha pale alipo...Sisi naona mazali yetu ni kungoja tujaribishe tena 2015..tubadilike
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom