Kikwete Kafanya Vyema Wapi?

chumvichumvi

JF-Expert Member
May 6, 2010
1,206
304
Katika uongozi haswa nafasi ya juu ya ukuu wa nchi muongozaji wa nchi kwa maana ya raisi huwa na mamlaka makubwa sana ila zaidi na zaidi mamlaka hayo ugawanyika katika sehemu kuu mbili mbazo ni HEAD OF STATE na HEAD OF GOVERNMENT.

Swali langu kwa wanaojua ndugu yetu raisi wa Muungano wa Tanzania amefanikiwa kumudu sehemu gani kati ya hizo mbili na madhara yake ni yapi kwa kule ambapo ameshindwa kupamudu

Naombeni msaada wana jamvini wa kueleweshwa zaidi

I humble submit .....
 
Laiti thread ingekuwa inauliza ni wapi kafanya vibaya, bila shaka ingepata wachangiaji wengi sana.
 
Huyu msanii hana chema alichokifanya zaidi ya kutekeleza yale aliyoyaacha Mkapa. Ikumbukwe, yeye anatekeleza tu ila hajafanya maamuzi ya maana.
 
Hawezi fanya vyema si asili yao, wao wanaweza ngoma ya kigodoro, baikoko vanga, mdundiko kangamoko
 
Miundo mbinu kidogo amejitahidi, Magufuli na Mwakyembe wanamlindia kwa huko. Pia jamaa ana damu ya kupendwa tu. Hata akipita kwa wapinzani wa chama chake bado watu wanafurahia kutokelezea nae kwenye mapicha:photo::photo:.
 
Katika uongozi haswa nafasi ya juu ya ukuu wa nchi muongozaji wa nchi kwa maana ya raisi huwa na mamlaka makubwa sana ila zaidi na zaidi mamlaka hayo ugawanyika katika sehemu kuu mbili mbazo ni HEAD OF STATE na HEAD OF GOVERNMENT.

Swali langu kwa wanaojua ndugu yetu raisi wa Muungano wa Tanzania amefanikiwa kumudu sehemu gani kati ya hizo mbili na madhara yake ni yapi kwa kule ambapo ameshindwa kupamudu

Naombeni msaada wana jamvini wa kueleweshwa zaidi

I humble submit .....

uhuru wa kujieleza,tunajiachia sana JF,popote nikiulizwa ntasema JK ameturuhusu sana tujieleze,,,,pamoja na hayo amejitahid sana KUPANDISHA DENI LA TAIFA,AISEE NAMPONGEZA SANA
 
1. Miundo mbinu, kilometre za lami kwa awamu ya 4 ni nyingi kuliko ukijumlisha za awamu ya kwanza mpaka ya 3
2. ujenzi wa madaraja: kigamboni - on progress na mto malagarasi
3. Mgawo wa maendeleo sawa kwa taifa. Lami na miradi ya maendeleoa imefika mtwara, Ruvuma,kigoma, Rukwa, Tabora na Lindi na Pemba. Awamu ya 1 to 3...lami na miradi ya maendeleo ilikuwa baadhi ya mikoa na kanda km kaskazini

4. Kilimo kwanza: kwa takribani miaka 5 sasa Tanzania ndio inalisha East n central Africa. jana kenya wameomba tani za mahindi 200,000 sudan na somalia wameomba pia

5. Kuboresha mishahara ya wafanyakazi. kikwete ndio raisi wa kwanza kuongeza mishahara sekta ya umma kwa zaidi ya asilimia 40

6. Ujenzi wa bomba la gesi kutoka mtwara kuja dar ambalo.litapunguza adha ya umeme

7. mradi wa DART na tren ya Mwakyembe jijini Dar.

8. Ujenzi wa Terminal 3 uwanja wa Julius Nyerere

9. Mkapa aliua mashirika ya Umma. JK amefufua Reli, NHC, ATC, TANESCO

10. Kuboresha kidogo mikataba ya madini ktk mrahaba na kulipia kodi

11. Ujenzi wa UDOM

12. Mradi vitambulisho vya Taifa

13. Kukibali wazo la kuandika katiba mpya

14. Mradi wa umeme vijijini kupitia REA. zaidi ya asilimia 30 wameunganishwa na umems
15. mradi wa bandar ya bagamoyo

16. mradi wa airpot ya kisasa zanzibar

JK ana mapungufu yake.....lakini alojaaliwa kufanya ni hayo na mengine yanaendelea kutekelezwa
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,heko mkuu
 
Back
Top Bottom