I MAY BE HAVING A SMILING FACE BUT AM FIRM ON STRONG ISSUES: ni kauli ambayo mkuu wa kaya alishaitoa mwaka 2006 na ameanza kuitimiza juzi juzi tu baada ya kuamua kumtosa swahiba wake mkubwa ambae wameshatueleza hawakukutana barabarani ila juzi amempa nafasi ya kutafakari na kuchukua uamuzi mwenyewe kabla chama hakijawaonyesha mlango wakutokea
vipi kuhusu suala la katiba mpya?
Umechambua vizuri Mkuu....
Bila kusahau suala la Madaktari wetu na sekta nzima ya afya kwenye mgogoro wa juzi...
Ametuonyesha jinsi alivyo "firm" pale alipowakatalia Mponda na Nkya wasijiudhuru nyadhifa zao kuokoa maisha ya WATU.
Mgogoro wa Zanzibar ulikuwa mpango wa Amani na Seif + wazanzibari wanaoijua pesa. Mgogoro wa Zanzibar haukuwa na maslahi kwa biashara ya utalii biashara ambayo ukiwaulizia wazanzibari watakwambia ilivyokuwa na umuhimu kwa uchumi wa visiwa hivyo na kwa Rais Mstaafu Amani mwenyewe.Vipi kuhusu mgogoro wa kisiasa Zanzibar mfupa uliowashinda wengi
Vipi kuhusu kuwapeleka Mahakamani Mawaziri na Katibu wakuu mfupa uliowashinda wengi..
Vipi kuhusu .....
Topical,Vipi kuhusu mgogoro wa kisiasa Zanzibar mfupa uliowashinda wengi
Vipi kuhusu kuwapeleka Mahakamani Mawaziri na Katibu wakuu mfupa uliowashinda wengi..
Vipi kuhusu .....
Mawaziri waliopelekwa mahakamani walikuwa wanamuunga mkono mgombea tofauti na wanamtandao so it is another show off isiyo na deal. Usishangae ikaishia watu kuachiwa huru. Kwa mwenye nia ya kuthubutu Kagoda isingechomoa kirahisi wala DOWANS.
Topical,
Mawaziri gani unaowazungumzia wewe? Unazungumzia Mramba na Yona? Mbona hawa hawana kesi za kujibu?
Mramba yuko mahakamani simply because alimpunja Kikwete mgao kwenye lile dili la Alex Stewart.
Kaka hufuatilii mambo? DOWANS kuvunjiwa mkataba (pamoja na madai ya wananchi wengi kudai uvunjwe) ulivunjwa kwa kuwa kulishaonekana mwanya wa kupata fedha zaidi kuliko ungesubiri kumalizika time. TANESCO walipokata rufaa swala la ufake wa Richmond halikuwasilishwa mahakamani ili DOWANS wapate mwanya wa kushinda na ikawa. Mwanasheria wa TANESCO alikuwa mwajiriwa wa Rostam (Voda) hadi miezi kadhaa iliyopita sawa na Waziri wa Wizara hiyo kabla ya kuingia Bungeni. Ndiyo maana Ngeleja alikuwa wa kwanza kushangilia malipo mapya ya DOWANS na sasa inadaiwa bado TANESCO wanaweza kukata rufaa kupinga kufanya malipo hayo jambo ambalo litawaongezea ulaji watakaposhinda mwishoni. Hujui serikali yetu kwa maana ya wakubwa wanapata zaidi DOWANS ikishinda kesi kuliko ikishindwa?Aisee dowans si umeondoka na PM (rafiki yake) ulifikiri bila kuwa firm angeweza kubaki na PM wake..lakini anafuata sheria ukiboranga unaondoka..
Hizo ni romuors tu, kama hawana kesi ya kujibu itakuwa kosa la mahakama na wanasheria wetu (ukosefu wa uzalendo) na si JK
Unaweza kushindwa kuamini ukweli huu, pamoja na kumtabiria anguko kwa kutochukulia hatua baadhi ya mambo mazito JK bado anapeta tu na anaendelea na smile yake almost muda wote. Richmond, DOWANS, EPA (Kagoda) na yote ambayo amepuuza maoni ya watu wakweli takriban wote ndani na nje ya nchi waliomsisitiza achukue hatua, yanaendelea kusahaulika kwa show off zinazoibuka kila kukicha.
Unaikumbuka ile ya miaka hamsini ya uhuru wa Tanganyika? Inadaiwa imekula billions kibao halafu mwezi huo huo mishahara ya watumishi wa serikali ikalipwa kutokana na mikopo ya benki za hapa nchini (Inasemekana).