Kikwete: Hata Nyerere alishindwa ingawa tunamsifu sana

mwalimu hakuwahi kumpenda JK

Ila CCM walijifanya kimbelembele baada ya Mwalimu kufa, Alimjua na kunaviongoza alowajua aliwaita Mchwa Mmoja wao ni JK na Lowasa!

Nilisikia kwenye moja ya Hotuba Zake
 
"MWELEVU hujifunza kupitia makosa ya wengine, MPUMBAVU Hujifunza kupitia Makosa yake mwenyewe" BY SEKULU
 
Mwalimu alitulisha unga wa Yanga, wengi wenu mlikuwa hamjazaliwa!

NA wote mlikula na hakuna alolala na njaa na mlisoma vizuri pumbav zenu, Saa hii mnalishwa nini na Mkwere??, Gap kati yako na maskini unaliona au unakurupuka. Mlikula unga wa yanga na wote mlikua kwenye level moja including watoto wake, Uliza mtoto wa mkubwa gani ambae yupo sawa na Mwanao.

Fikiria kwanza!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
JK anadhani chini ya uongozi wake anaweza kuwa kama Nyerere jambo ambalo ni gumu sana kwake na kutokana na maono ya mwalimu kumgusa kila analofanya au kubolonga,hujikuta bila kujielewa anatengeneza chuki bila ya yeye kujijua na mwisho wake analopoka mambo ambayo hata mtoto mdogo ukimuuliza atakwambia kuwa JK hayupo sahihi.
Anahitaji msamaha maana hali aliyonayo sasa haiwezi na kazidiwa na upepo mbaya wa mabadiliko,wanamapinduzi wanajipanga na soon tutaona kitakachojiri.
 
Wakati Nyerere anamkabidhi Mwinyi madaraka, pale Moshi kulikuwa na viwanda vifuatavyo vikifanyakazi kwa zaidi 50% ya uwezo wake


  1. Moshi Tanneries
  2. Tanzania Bag Corporation - Mill 1 and Mill 2
  3. Kiltimbers
  4. Moshi Plywood
  5. TBL
  6. Moshi Textiles
  7. Coffee Curing
  8. Kibo Match Corporation
  9. Kibo Paper
  10. National Milling
  11. TWICO Imara Furniture
  12. Kilimanjaro Machine Tools
  13. Babu Mkate
Leo hii ni viwanda vingapi vinafanya kazi na vinaajiri watu wangapi ukilinganisha na 1985? Huu mfano ni kwa wilaya moja ya Moshi


Mwalimu kila Mkoa aliacha kitu ambacho kama tungekua na viongozi makini Tatizo la Ajira lisingekua kubwa kama ilivo hivi sasa,
Yaani hawa jamaa ni mchwa mchwa michwa.

Very Hopeless kazi kujiita madocta tu wakat shule ziliwashinda.
 
"MWELEVU hujifunza kupitia makosa ya wengine, MPUMBAVU Hujifunza kupitia Makosa yake mwenyewe" BY SEKULU

Hakuna kitu kinachotokea miaka hii ambacho ni kipya na hivo hakuna haja ya kikwete kujitetea kana kwamba hivi vitu ni viiipya wakati mpaka sas vinatokea nchi zingine.
 
Ni kweli kwani aliyejenga chuo kikuu cha Dodoma kama sio Mkapa atakuwa Nyerere au Mwinyi! Akili za kushikiwa hizo watoto!
 
Ni kweli kwani aliyejenga chuo kikuu cha Dodoma kama sio Mkapa atakuwa Nyerere au Mwinyi! Akili za kushikiwa hizo watoto!

Kwa msingi huo ndio umlinganishe na Nyerere???

Ni kichaa tu anaweza kuilinganisha timu ya Barcelona na Manyema FC eti kisa wote wanatumia miguu kucheza mpira.
 
Mwalimu alisababisha watu wavae magunia na matairi

sawa tulivaa matairi na magunia na tukala unga wa yanga. lakini watu walikuwa hawiibii serekali kiuwazi hivi nakujilimbikizia mali kwa wachache namna hii hata udiwani sasa hivi ni dili? where are we going? wakati ule unasoma na kukaa na watoto wa mawaziri darasa mmoja sasa hivi kiko wapi? wao academy sie HAKI ELIMU. pigine heasabu la GAP BETWEEN WALICHO NACHO NA MWANANCHI sio utani. this is serious
 
Ni kweli kwani aliyejenga chuo kikuu cha Dodoma kama sio Mkapa atakuwa Nyerere au Mwinyi! Akili za kushikiwa hizo watoto!

Chuo Kikuu cha Dodoma kimejengwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Serikali ya JK haijatoa hata senti, Subiri kizazi kijacho kitakapoanza kulipa deni wakati madini yameisha ndo watakapofukua mafuvu yenu kuyapeleka maabara!
 
Kosa kubwa sana kujilinganisha na marais waliopita hasa Nyerere!Usawa upo wapi?Eti nchi haijawahi kuwa tajiri hata baada ya kuongozwa na maraisi wanne!Hivi hii nayo ni pointi?Uchumi wa nchi unamilikiwa na kundi dogo la watu huku wananchi wengi wakiishi maisha ya kubahatisha.Halafu eti wamchekee tu huku maisha yakizidi ugumu wa kawaida!
 
Kikwete kumponda Nyerere iko kidini zaidi! anajua wapi anapata nguvu na anajua kuwa kuna kundi lina msupoort kwa nguvu zote.
 
Watu wanadai kipindi cha Nyerere watu walisoma bure!... watu hawakusoma bure isipokuwa serikali ilikuwa inapanga bei za mazao na kuwakata watu juu kwa juu, na then pesa zao hizo hizo pamoja na Kodi zao ndo zilikuwa zinafinance Elimu.
Serikali haina uwezo na wala haijawahi kutoa elimu bure.!
 
Halafu anamuta Mzee Nyerere! Hata heshima ya 8aba wa Taifa hampi.
Mwal JKN alitaka watu wasome kwanza,watambue rasilimali zao na baadae waweze kuzitumia vema kuondoa umaskini lakini imekuwa bure kabisa...
 
Back
Top Bottom