Una ukweli ndani yako. Labda nikukumbushe kitu hiki,: mchambuzi yeyote anayeweza kutoa tathimini yenye hoja zilizosimama ni yule ambaye aghalabu unbiased!. Mimi binafsi namtaza mwl Nyere na uongozi wake,mapungufu yake na mafanikio yake ktk angle hii:-1. Wakati anaichukua tanganyika,wasomi ambao angekaa nao kuweka mikakati ya kimfumo na utawala miongoni mwa watanganyika walikuwa wakihesabika..Sina kumbukumbu vizuri iliwahi kusemwa alianza akiwa na mainjia wasiozidi watano(naweza kusahihishwa).
2..katika mazingira duni,wasomi wakuhesabika,miundombinu isiyopitika,uchumi mbovu, nk ,mwl alijitahidi kwakweli kwa asilimia 100% (KWA WACHAMBUZI WANAOANGALIA MAZINGIRA YA TANGANYIKA 1961 kama nilivyoanisha hapo juu) kujenga Nchi yenye kuheshimiana,usawa,na ustaarabu. Kumbuka misingi na fikra zake juu ya Arusha declaration.,kufanikiwa au kutofanikiwa ni jambo lingine but dhamira na uthubutu unapambanua Mwl ni kiongozi wa aina gani..
Anyway,ninayomengi mno kutetea misingi na utukufu wa mwl in leadership. Huwezi kulinginsha wanariadha tamati zao bila kugusia muda na startng point zao. Lets say,mmoja aanze saa moja asubuhi poitia A, na mwingine aanze zaa tatu asubuhi point B ahed of opint A,then useme wote at the same contant speed wafike point C at ttime, huo ni uwendawazimu.
Mkuu Waberoya,nakuheshim sana,but kwa wenye hekima,kumsema mwl mapungufu yake kwa misingi ya kujitetea,au kuhalalisha upuuzi wao, ni UPUNGUANI. SI KWASABABU HAKUKOSEA,HAPANA,BALI KWA AINA NA UWAJIBIKAJI WA SERIKALI YAKE,ALIYOIONGOZA KWA KUANZIA NA WASOMI WATAALAM KIDUCHU,NA UMASKIN WA NCHI,UCHUMI AT ZERO,MIUNDOMBINU ZORO, THEN ULINGANISHE KIKWETE NA WASOMI WASHAURI KIBAO,ANAAMUA KWA MAKUSUDI KUCHAGUA MATAPEL BADALA YA WAZALENDO WASOMI,THEN UTETEE, NOOO!!! n
Wareboya
nimefanya makusudi kabisa kutumia maneno makali juu ya hoja yako kwa sababu nina uhakika kabisa wewe ni mtu msomi na muelewa wa mambo lakini kwa sababu ya chuki binafsi au maslahi binafsi sometimes hutaka kuutumia usomi wako kupotosha mambo! Wewe uko kama wanasiasa wa Kenya!
Leo katika hotuba yake ya siku ya kuzaliwa CCM, kuna kauli nyingi za kikwete ambozo kama rais hakustahili kuzisema, mojawapo ya ,ni kauli yake ya kwamba pamoja na kumsifu sana Nyerere lakini alishindwa kutatua changamoto nyingi katika utawala wake na hivyo hivyo kwa marais wengine waliomtangulia, sembuse mimi (Kikwete). Alisema hayo akijitetea kwamba yeye sio wa kwanza kushindwa kuondoa matatizo ya watanzania.
Mimi nimeichukulia kauli hii kama simple/cheap excuse ya kikwete kwa jinsi alivyoshindwa kutatua matatizo ya watanzania. Sio tu kikwete ameshindwa kutatua matatizo bali ameyaongeza na kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu zaidi. Anaweza kutuambia yeye kama rais am-achiave nini, wenzake wote wana vitu vya kujivunia.
Nyerere alijenga umoja wa kitaifa na kufanya watanzania kuwa wamoja na kuwepo kwa amani ambayo kikwete anajivunia leo, lakini pia mzee huyu alijenga uwajibikaji kwa watumishi wa umma kitu ambacho kikwete ameshindwa.
Mzee Ruksa aliruhusu uchumi wa soko ambao ulisaidi kufanya upatikanaji wa bidhaa muhimu ambazo mwanzo zilionekana kama anasa.
Mzee Mkapa akajitahidi kujenga uchumi imara bila kusahau miundo mbinu na kurudisha heshima ya wafanyakazi.
Pamoja na mapungufu yao viongozi waliopita wanayo ya kujivunia.
Akaja kikwete
1) akaharibu kabisa umoja wa kitaifa kwa kuanza na makundi ndani ya CCM (kwa kuanzisha mtandao wake uliowavuruga wengine) na baadae kuharibu umoja taifa zima kwa kuchochea ajenda zake za udini na ukabila.
2) Akabomoa kabisa uchumi alioujenga mzee Mkapa kwa kuendekeza anasa, matumizi makubwa serikalini, kusafiri kwenda kubembea na kuendekeza ununuaji wa magari ya kifahari yasiyo na tija, gharama za maisha zimepanda mno, thamani ya shilingi imeshuka sana, mfumuko wa bei hauelezeki.
3) Ametengeneza mitandao ya wizi kwa kuwatumia marafiki zake kama RA, ED kwa kutaja wachache.
4) Akaharibu kabisa mfumo wa elimu kwa kuanzisha kisiasa shule za kata zisizo na walimu wala vifaa, ukiangalia wanafunzi wanaofeli ni heri hata tungebaki na shule chache bora,maana waliofeli wanabaki kuwa darasa la saba hawawezi kusema wana elimu ya form IV.
Ni mengi jamani yanayoonyesha tofauti ya utendaji kazi wa kikwete na watangulizi wake, naomba niishie hapa.
Lakini Kikwete please dont look for cheap excuses, just admit that ur the most failure president we ever had.
NIMEISOMA HOTUBA JK -sikubaliani kabisa kabisa na kikwete anapodai kuwa Mwalimu aliacha nchi hii si TAJIRI, naomba nimkumbushe kikwete na CCM kwamba Baba wa TAIFA aliacha Tanzania na utajiri wa kutupwa na ni baabda ya kifo chake mafisadi wakaibuka, wawekezaji wanyonyaji wakaingia na kuididimisha nchi hii kwenye umaskani ukashika kasi kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. Kikwete na CCM wakumbuke kuwa Mwalimu alifanya haya wakati wake
1. Madini yote alitaka Watanzania wayachimbe ni kikwete kama waziri wa madini alishiriki uibaji wa mali yetu hiyo
2. Mali asili na utalii tunayojidai leo ni kwakuwa mwalimu hakuruhusu wizi wakati wake
3. Mwalimu aliwasomesha bure akina kikwete na mafisadi wote wanaotunyonya kwa sasa
4. Mwalimu hakuwa na mgao wa umeme -miradi ya mwalimu ya umeme ndio hiyohiyo mpaka leo serikali ya kikwete inategemea
5. Wakati wa Mwalimu hapakuwepo mafisadi
6. Wakati wa mwalimu hapakuwepo na bodi ya mikopo why bodi?
7. wakati wa Mwalimu hapakuwepo mfumuko wa bei kama huu wa sasa
JK na CCM wanatakiwa wamwombe radhi mwalimu ameshalala wamwache apumuzike