Kikwete face to face with Drogba

Mkulu hata akimualika nani kwenye sijui msosi gani.lakini harudi tena ikulu .akafanye niño?? Halafu msije mkashangaa kina Drogba wakitinga fainali mkulu akaenda kuangalia!!nasema hivi bila kuficha si hela zebu za Lodi anazo na zinamruhusu.Sasa nani atazitumia Kama sio true?si mmempa kura na mtampa tena. Na ole wenu aje kusikia kuwa Angola kuna bembea .
 
Mi ningeshangaa kama asingefanya hili! Kwani si ni mkuu wa kaya tunamzungumzia? Au!
 
Mi ningeshangaa kama asingefanya hili! Kwani si ni mkuu wa kaya tunamzungumzia? Au!

Poa tu ila siku zake zinahesabika tu sasa hivi.siongei kwa jazba ila wananchi inatakiwa tusche kuwa wenu na tukubali mabadiliko.
 
Hiyo haitoshi tunawasubiri Real Madrid maana bwana mkubwa aliisha sema kama sijasahau. Kadhalika huo ni muendelezo wa matumizi ya ovyoovyo yalioyo anzia kwa Visura pale Ikulu mmesahau ?
 
Kwani Rais anatakiwa akutane na wakuu wa nchi na viongozi peke yake? Rais anatakiwa awe focused kwenye mambo machache tu? Mie naona amefanya jambi jema whether watarudi au ndio watakwenda kimoja. Ni heshima kwa timu hiyo ambayo kwa Afrika inapewa nafasi kubwa kwenye kombe la Afrika na World Cup. Nadhani ni bora rahisi anaye acknowledge kila sector. Kwahili naona hajakosea. Na pia tuzingatie maendelea ni gharama
 
Wadau, mimi sioni tatizo lolote kuhusu chakula alichowaandalia Ivory Coast maana Kiafrika hilo ni jambo la kawaida kabisa ya kuwa mgeni anakaribishwa na kupewa chakula kizuri kabisa kinachioweza kupatikana kwa mwenyeji wake. Huo ndiyo ukarimu wa Kitanzania.
Hii kazi ya kuandaa chakula na kuwakaribisha ni kazi ya TFF na labda Waziri wa Michezo lakini sio rais wa nchi, amekwenda kwenye mechi inatosha.

Pili, nampongeza Rais kwa alichofanya, amewaonyesha wageni ukarimu wa Kitanzania hasa ukizingatia wachezaji wengi wa Ivory Coast wanatoka na kuishi Ulaya kwenye maisha ya kibinafsi na kichoyo, tena hata watu wa huko Afrika Magharibi wana tabia za ubinafsi-ubinafsi kwa hiyo hilo ni somo tosha kwa wageni wetu.
Unadhani hao wachezaji wanajali?

Nne Wa-Ivory Coast, kwa kutambua ukarimu wetu wameahidi kuwa iwapo watatwaa kombe la CAN basi watalileta Tanzania. Kwa hiyo, tumeweza kuwa-impact.
Ebo!! sasa kama mambo yenyewe ndio haya kazi ya Taifa Stars ni nini? Hizi nguvu tunazoziwekeza kwenye kutafuta ujiko na kujikomba komba tungewekeza kwenye kuijenga timu yetu ya Taifa basi tungekuwa mbali sana kisoka.

Mwsiho, pamoja na mapungufu yake nimegundua kuwa JK anajua sana PR na ndo maana huwa anapata favor ya ahadi za misaada anapotembelea ughaibuni ingawa kwa kweli misaada haitaweza kutusaidia sana iwapo hatutakaza buti dhidi ya ufisadi na kuhakikisha kinachopatikana kinafanya kazi iliyokusudiwa.
Hiyo PR ukiizidisha sana inaonekana kama ni a** kissing.
 
Kuwaandalia chakula cha jiioni n.k ni mambo mema wala hakuna tatizo hapo na hicho alipaswa kufanya.
Kaka naona donge limekakaa! Pole sana!
095_pics.jpg
 
kuhusu kuwaalika chakula cha mchana sio mbaya na kama watu wanavyodai tumefuja hela sio mbaya vile kwenye gharama ya chakula na wapishi si walipa kodi kwahio wamelipwa na pia mchele ,nyama na vitu vingine vimenunuliwa kwenye masoko yetu kama mtu aliongezea cha juu sasa hio ni udokozi na ni swla tofauti kabisa.


turudi sasa kwa muheshimiwa rais ambaye kila siku ya mungu lazima aje na mpya na saa nyingine huwa najiuliza je kweli rais wetu ana watu wakumshauri na kama anao je ni wanao qualify hio kazi au ndio kubebana bebana tu kama tulivyozoea?


nasema haya yote kwani kitu kikubwa kilicho nishangaza kwenye tukio hili ni muheshimiwa rais kitendo chake cha kuwabagua wachezaji wengine wa ivory coast na kwenda kuwapa jezi Drogba,Kalou,K.toure,y. toure na E. eboue.hili swala sidhani kama rais alifanya tendo hili kupitia washauri bali alikurupuka tu kiushabiki na kibinafsi na kuwapa wachezaji hawa 5 jezi kwa vile ndio anawaona kwe runinga akiwa amepumzika weekend na sio kwamba kawapa hizi jezi kwa niaba ya watanzania yeye kama rais.kama ingekuwa kwa niaba ya watanzabia basi wachezaji wote wa ivory coast wangepewa jezi ya timu yetu ya taifa.kitendo hichi ni cha kusikitisha sana na nategemea wausika watajirekebisha siku nyingine kwani wote wale wachezaji wanafanikio makubwa na wanastahili kuheshimiwa kama hao wengine hawakuja hapa kushinda au nani bora wamekuja hapa kitimu na walitakiwa kuwajibishwa kwenye lolote lile.kama jk alikuwa ana waona hao wa 5 bora angetafuta mda wake binafsi baada chakula wangekutana hawape hizo jezi aliowaandalia.



Kosa la mwisho ni jezi za taifa letu kuandika majina ya hao wachezaji.muheshimiwa rais jezi za taifa ni tofauti na za club,jezi ya taifa ni sawa na bendera ya nchi na kitendo cha kuandika majina yao ni sawa na kuandika jila la {drogba} kwenye bendera ya nchi yetu.nadhani washauri wako hawakufanya uchambuzi zaidi na nichawashauri kwa vile lengo letu kubwa kuitangaza nchi yetu siku nyingine itakapokuja timu kama hivi ni vizuri jezi hizo za taifa muandike majina ya vivutio vyetu vya utalii nyuma badala ya kuandika majina ya hao wachezaji maarufu.kwa mfano hapo tungewapa wahezaji wote wa ivory coast jezi za taifa yenye majina tofauti hili kila mmoja wao atangaze nchi yetu popte waendapo.Badala kuandika Drogba mngeandika tu serengeti,mt.kilimanjaro ma kadhalika,hii ingesaidia sana kutangaza nchi yetu na ingekuwa wachezaji 25 badala ya 5.


hayo nimaoni yangu binafsi na tafadhalini kama ivory coast wakifika fainali haina haja kuwasafirisha watu kwenda kuishangilia tuwashangilie majumbani kwetu au kama kuna watanzania angola waende lakini tunaomba tusisikie delegation imetumwa Angola.kombe wakiataka kulileta mlima kilimanjaro walete ndio kutangaza kwenye na ndio nia yetu kubwa.
 
Mtani (Arsene Wenger),
Mimi mwenyewe nimeshangaa sana kuona Drogba anapewa jezi ya Taifa Stars na jina lake, kwani baada ya mechi wachezaji hawakubadirishana jezi? EPIC FAIL!!
oazsds.jpg
 
This thread is needless, overanalysis and total waste of time. JK tulimchagua wenyewe hivyo wenye kubeba mdhamana wa matendo yake ni sisi sote kwa uzoba wetu.
 
Hivi JK katika serikari yake hana waziri wa michezo???. nadhani huyo ndo alistahili kuwa na hizo timu.
 
Mimi kwangu nina ujumbe kwa CAG: Usisahau kukagua haya matumizi kama ulivyofanya kwa wale walimu maskini waliokuwa wanadai posho zao

Mkulu vp banaaaa...... Umisahau wabunge wetu walafi walipitisha mabilioni ya shillingi kwa ajili ya refreshments na vitafunwa na kuipa kampeni ya Kilimo Kwanza Mil. 700.. Mwambie CAG asisahau na kukaugua huo utafunaji!!! kudoz
 
MNAMUONEA MKWERE WA WATU!muacheni jamani.

kwenye hili mnamuonea
 
JK hajui ma star wakiondoka pale tu wameshamsahau na kinchi chake....waanafikiria mambo yao ya kuingiza pesa....baasi,angewaomba waje wawekeze kwenye ball kujenga academy....kama wameona tuna vipaji,,,,,,


Lakini hilo halituzuii sisi kuwakarimu....


hakuna maendeleo yanayokuja bure kaka
 
Jamani tuache majungu Drogba katutangaza ulimwenguni hakuna ubishi hapo! Pesa iliyotumika kwa ajili ya chakula cha wachezaji pale kinaweza kuwa kidogo sana ukilinganisha na faida zingine zinazoweza kupatikana kutokana na kutangazika huko.
 
Hii nchi kiboko hela za walipa kodi zinaunguzwa ukiuliza unaambiwa tunasaidia kuitangaza nchi. SMH!!!

Acha mawazo mgando wewe,unataka hela za walipa kodi zitumike kufanya nini? Wewe nyumbani kwako ukijiwa na mgeni unafanya nini?

Hii ni nchi bwana.
 
Back
Top Bottom