Kikwete face to face with Drogba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete face to face with Drogba

Discussion in 'Sports' started by Mzito Kabwela, Jan 6, 2010.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280
  JK apata dina la mchana na ivory coast, rwanda na taifa stars leo

  [​IMG]

  JK akimzawadia jezi ya TAifa Stars nyota wa Ivory Coast na Chelsea Didier Drogba katika dina la mchana alilowaandalia wachezaji na viongozi wa Taifa Stars, Rwanda na Ivory Coas mchana huu hoteli ya Golden Tulip jijini Dar.
  [​IMG]

  JK katika picha ya pamoja na timu ya Ivory Coast
  [​IMG]

  JK na Ivory Coast

  [​IMG]

  JK katika picha na timu ya Taifa ya Rwanda ambayo imedhatua nchini kucheza na Ivory Coast kesho neshno

  [​IMG]

  Kocha wa Taifa Stars Marcio Maximo na vijana wake

  [​IMG]

  Baadhi ya wachezaji wa Rwanda

  Picha na maelezo kwa hisani ya Blog ya Michuzi
   
 2. pius-ndiefi

  pius-ndiefi Member

  #2
  Jan 6, 2010
  Joined: Dec 11, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK akoshwa na ziara ya Ivory Coast
  *Awaandalia chakula maalumu Golden Tulip
  *Ammwagia sifa Drogba, amkabidhi uzi wa Stars
  *Awaombea watwae taji, aahidi Watz kuwashangilia


  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ameelezea kufurahishwa na ujio wa timu ya taifa ya Ivory Coast ‚The Elephant’ kwani umeutangaza nchi kutokana na wachezaji wake nyota wa kimataifa kujulikana akiwemo mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Didier Drogba.

  Akizungumza katika hafla maalumu ya chakula cha mchana aliyoiandaa kuwakaribisha Ivory Coast, kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar leo JK kasema Tanzania imepata sifa kubwa duniani baada ya kutangazwa kwa mara ya kwanza katika kituo cha televisheni cha Sky News, kuhusiana na ziara ya The Elephant katika habari za michezo, sambamba na kuonyesha picha.

  Kikwete alisema, kutangazwa kwa mechi kati ya Tanzania na Ivory Coast ni sifa kubwa kwa nchi, hasa ukizingatia Taifa Stars iliweza kuwamudu The Elephant ambao walikuwa wamesheheni nyota wa kulipwa na kutoka na ushindi mwembamba wa bao 1-0, lililofungwa na Drogba.

  Rais alimpa pongezi kubwa mshambuliaji huyo ambaye pia ni tegemeo wa klabu ya Chelsea ya England, kwa kuitangaza Tanzania alipokuwa akihojiwa na Sky News Sports, ambako hakusita kusifu kiwango cha wachezaji wa Stars, kuwa ni kikubwa.

  "Jana nilifurahi sana nilipokuwa nikiangalia kituo cha Sky News Sport, kwa mara ya kwanza kuona wakitangaza timu ya Ivory Coast ikiwa nchini, ambapo mchezaji nyota wa kimataifa Drogba alikiri kwamba, Tanzania soka lipo huku akisifu kiwango cha Stars," alisema Kikwete.

  Kikwete alisema, kutokana na Drogba kuwa mchezaji maarufu duniani, kwa kupitia umaarufu wake, Tanzania imeweza kujitangaza duniani kote na hiyo itasaidia kuwavutia nyota wengine kufanya ziara hapa nchini.

  "Hivi sasa Dunia nzima inatambua kiwango cha soka la Tanzania, natoa shukrani nyingi kwa Ivory Coast kuichagua nchi yetu kupiga kambi ya kujiandaa na fainali hizo za Angola," alisema Kikwete.

  Aidha alisema, alipanga kuandaa hafla hiyo na kuwaalika wachezaji wa Ivory Coast, lakini baadaye akaona ni bora ajumuike na timu zote tatu, ambazo ni wenyeji Tanzania, Rwanda na Ivory Coast.

  Katika hatua nyingine, Kikwete aliwataka wachezaji wa Rwanda ‚Amavubi’, kucheza kwa kujituma na ushirikiano mkubwa ili kuwafunga Ivory Coast, baada ya Stars kufungwa 1-0 licha ya kuwa, angalau wangeweza kutoka sare, lakini bahati haikuwa yao.

  Aliongeza kuwa, Tanzania itajivunia hivi sasa katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, kutokana na Ivory Coast kuichagua pekee kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na fainali za Angola, pamoja na Kombe la Dunia litakalofanyika Afrika Kusini.

  "Ninaamini kuwa, Bara hili la Afrika lina timu nyingi huku Ivory Coast ikiwa inaongoza kwa ubora, hivyo kwa kuchagua kuja nchini kwetu kufanya mazoezi ya mwisho ya kujiandaa kwenda Angola katika Fainali za Afrika, ni jambo la kujivunia kwa kila Mtanzania," alisema Kikwete.

  Wakati huohuo, Kikwete alisema, anawaombea kwa Mungu na Miungu mingine kutwaa ubingwa wa Afrika, ili kurejea na Kombe hilo kama walivyopanga kulileta na kulipeleka Mlima Kilimanjaro na kuongeza kuwa, ana imani watashinda.

  Aidha alisema, Tembo hao wa Ivory Coast watakapotinga hatua ya fainali, Watanzania watakwenda kuipa sapoti ili kutwaa taji hilo.

  Mwisho wa hafla hiyo, Rais Kikwete aliwakabidhi jezi ya Taifa Stars, wachezaji nyota wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drogba, Kolo Toure, Emmanuel Eboue, Solomon Kalou na Yaya Toure.

  Fainali za Mataifa ya Afrika zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 10 hadi 30, mwaka huu nchini Angola.
   
 3. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280
  Ama kweli Rais tunaye.....Kikwete Oyeeeeeeeeeeee!
   
 4. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2010
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hii nchi kiboko hela za walipa kodi zinaunguzwa ukiuliza unaambiwa tunasaidia kuitangaza nchi. SMH!!!
   
 5. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli Chama Cha Majambazi hakina aibu. Pesa ya walipa kodi inateketea bila huruma. Je hii ilikuwa ni necessary?

  Tanzania haihitaji kutangazwa na vimburu inaweza kujitangaza bila gharama yoyote. idi@ots@

  Haya tupeni kiasi mlichotumbua? Inatia aibu.
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Jan 6, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  ..sijui ni lini atawakumbuka wananchi wa Kilombero.

  ..labda mpaka Drogba atakapoondoka nchini.

  ..naona kama Raisi amechanganyikiwa kabisa tangu hii timu itie mguu bongo.

  ..for two days Raisi yuko nao. kwanza kwenye mechi, halafu kama hiyo haitoshi anakuja na karamu ya kifahari kabisa.

  ..kile kitambaa cheusi cha maombolezo ya msiba wa Kawawa sioni hata mmoja amekivaa.
   
 7. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2010
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi kwangu nina ujumbe kwa CAG: Usisahau kukagua haya matumizi kama ulivyofanya kwa wale walimu maskini waliokuwa wanadai posho zao
   
 8. P

  PELE JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 229
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mabilioni mangapi yametumika katika mlo huo? Nani kaidhinisha matumizi hayo kama hayakutoka mfukoni kwa Kikwete? Mwalimu asingefanya upuuzi kama huu. Kweli Rais tunaye! Pia anajua kujikomba sana, timu nzima akawape uzi wa Stars Drogba, Kolo Toure, Emmanuel Eboue, Solomon Kalou na Yaya Toure tu!
   
 9. Companero

  Companero Platinum Member

  #9
  Jan 6, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  What a JK's cost-benefit analysis!
   
 10. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Wadau, mimi sioni tatizo lolote kuhusu chakula alichowaandalia Ivory Coast maana Kiafrika hilo ni jambo la kawaida kabisa ya kuwa mgeni anakaribishwa na kupewa chakula kizuri kabisa kinachioweza kupatikana kwa mwenyeji wake. Huo ndiyo ukarimu wa Kitanzania.

  Pili, nampongeza Rais kwa alichofanya, amewaonyesha wageni ukarimu wa Kitanzania hasa ukizingatia wachezaji wengi wa Ivory Coast wanatoka na kuishi Ulaya kwenye maisha ya kibinafsi na kichoyo, tena hata watu wa huko Afrika Magharibi wana tabia za ubinafsi-ubinafsi kwa hiyo hilo ni somo tosha kwa wageni wetu.

  Tatu, si kweli kuwa kuna mabilioni ya shilingi yameteketea kwa gharama za kuandaa mlo mmoja, naamini hata mapato yaliyopatikana siku ya mechi yenyewe badi ni makubwa kulinganisha na gharama za chakula walichoandaliwa.

  Nne Wa-Ivory Coast, kwa kutambua ukarimu wetu wameahidi kuwa iwapo watatwaa kombe la CAN basi watalileta Tanzania. Kwa hiyo, tumeweza kuwa-impact.

  Mwsiho, pamoja na mapungufu yake nimegundua kuwa JK anajua sana PR na ndo maana huwa anapata favor ya ahadi za misaada anapotembelea ughaibuni ingawa kwa kweli misaada haitaweza kutusaidia sana iwapo hatutakaza buti dhidi ya ufisadi na kuhakikisha kinachopatikana kinafanya kazi iliyokusudiwa.
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,596
  Likes Received: 1,996
  Trophy Points: 280
  Labda Sheick Yahya amemtabiria Ivory Coast watatwaa makombe yote la Africa na lile la Dunia,kwani hamjaona wameshapanga kulipandisha kombe la dunia mlima Kilimanjaro?Halafu pia mmesahau kuwa alitabiri Kawawa atakufa kabla mwaka uliopita haujaisha.....Vile vile kwamba mpinzani yoyote wa JK atakufa...Tanzania imenishinda.
   
 12. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jan 6, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuwaandalia chakula cha jiioni n.k ni mambo mema wala hakuna tatizo hapo na hicho alipaswa kufanya.
   
 14. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tusipende kutetea kila kitu hata kama tunampenda vipi. raisi wetu ni hodari sana kwa mambo haya ya kuonekana na kupiga picha na Boyz 2 Men, Hasheem Thabeet na Drogba.
  Kwangu mimi hii si zaidi ya Cheap Popularity.
  Akitaka apate 'thumbs up' yangu na atumie kasi hii hii ya kuwapa lunch akina Drogba na kupiga picha na akina Boyz 2 Men katika kuwaita Ikulu wale wahindi wa TRL na kuwashughulikia, Awaite akina Idrisa na akina Ndulu na kuwauliza nani kawaruhusu kujenga nyumba za mabilioni zenye swimming pool katika nchi hii hii ambayo bado kuna watu hawana maji safi ya kunywa na wengine wanakufa na njaa. Na mengi mengineyo.
  Na sitaki mtu aniambie kuwa kuna watu maalumu kwa hayo. hata la kuwapa lunch kina Drogba lina watu maalumu. Waziri w Michezo na Wasaidizi wake.
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Jan 6, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Huh? I think you are being sarcastic because you are extremely tired and upset.
   
 16. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  Unashangaa hicho kuna $7mio ziko njiani kuunguzwa ati kutangaza Tanzania kwa kuhost timu itakayocheza World Cup na watu wamekaa kimyaa jiiiii!
   
 17. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280

  Ila....?ule uzi mweusi uko wapi?
   
 18. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2010
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ye wooooooooooomi!
   
 19. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  JK hajui ma star wakiondoka pale tu wameshamsahau na kinchi chake....waanafikiria mambo yao ya kuingiza pesa....baasi,angewaomba waje wawekeze kwenye ball kujenga academy....kama wameona tuna vipaji,,,,,,
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Jan 6, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mjukuu wa chifu juma akienda kwa chifu ali hukaribishwa na wajukuu wa chifu ali... JK is way too high for that; angeachia akina mkuchika, TTB na wauza bia hiyo lunch, kumbuka kitaifa huwa kuna dhifa zake, na naona siku hizi hayo ya dhifa yamekufa!!! tumebaki na ubwabwa wa mchana


  Yaani tumefikia hatua ya kuletewa kombe na wenzetu tulione??? kisa?? ni kama la dunia au??? Mh, i am really disappointed ku-support eti watupitishie kombe na sie tuone!!! Guys...

  Hizo PR nyingine ni kazi za watendaji anafanya yeye!!! no delegation, no quality of service and proper monitoring... accountability principles ziko wazi. Ningependa wewe ujiulize, amesafiri mara ngapi na amepokea mara ngapi?? kwa utamaduni wetu utajiri na heshima ni wageni na SIO kutembelea watu, unless wana misiba!!!

  SAMAHANI KAMA NIMEKUKWAZA LAKINI NADHANI NCHI YETU INA MACHUNGU MENGI SANA HATA YA WIKI HII TU, KWA RAIS WETU KUANDAA LUNCH WAKATI KULE KONDOA KASKAZINI, BABATI, KITETO, SIMANJIRO, KILOSA NK KUNA MAFURIKO NA WATU WANAKUFA ...TTB, SERENGETI NA WENZAO WA WIZARA WANGEWEZA HILO
   
Loading...