Kikwete: Chanzo cha udini Tanzania hakijulikani

Kikwete: Chanzo cha udini Tanzania hakijulikani

Status
Not open for further replies.

juni

Member
Joined
Apr 5, 2011
Posts
87
Reaction score
19
akiongea katika shrehe za mei mosi rais Kikwete amesema hakuna anayejua chanzo cha udini hapa nchini

pengine alikuwa anawajibu wale wanaodai yeye ni kinara na mhasisi wa udini, na wenzake akina mwigulu ambao wanadai chadema ndiyo chanzo
 
Huo ni unafiki anajua vizuri mbona akina sheikh Ilunga hakumtuma Said Mwema amkamate lakini historia haitamucha kikwete kwa kufumbia macho udini.
 
Sasa NDIE Rais wa NCHI hana USULUHISHI kwa Wananchi ??? NYERERE alikuwa anatumia hii mikutano kuwaelewesha Wananchi Msimamo wake na Jinsi gani Amani itapatikana...

sasa kama Rais hajui CHIMBUKO na HAJUI JINSI ya KUSULUHISHA... are we all dropped off the BUS??

Aheri Mstaafu Rais Mwinyi angeweka Misamiati yake... Kuifumbua wengine ingetuchukua hadi 2015...
 
Mbona RIZT anapiga kampeni waziwazi kuhamasisha udi i wake babake hajui hilo tanzania haina dini watuachie nchi yetu waende uarabuni au soth wakaishi huko.
 
Nimemsikia mkuu,huyu jamaa ni mnafiki kweli,watu wamegoma kumpigia makofi.,mwenyewe kajishtukizia
 
Acheni chuki binafsi kipi kibaya alichokisema kilichowauma?
Acha unafki na wewe kwamba hajua chazo ni nin,eti kashtukizia watu wanagombania kuchinja,umjue ni mnafki anasema'hili jambo nililiona toka muda mrefu nikalisema',sasa how come hajui chanzo
 
niliwahi kumshauri jk ajiuzulu nchi imemshinda siku ya pili akatoa jibu kuwa nchi haijamshinda. AMA KWELI SIKIO LA KUFA
 
Kama ni raisi tunae, Mmiliki wa richmon hawajui, chanzo cha udini hakijui, waliomteka na kumgoa meno bila ganzi Dr. ulimboka hawajui, walie muua pade kule znz hawajui, waliomuua mwangosi hawajui..........sasa kazi ya hao aliowajaza hapo ikulu ni nini au kuedit video ya chadema..huu ni upum
 
akiongea katika shrehe za mei mosi rais kikwete amrsema hakuna anayejua chanzo cha udini hapa nchini

pengine alikuwa anawajibu wale wanaodai yeye ni kinara na mhasisi wa udini, na wenzake akina mwigulu ambao wanadai chadema ndiyo chanzo

It is ECONOMY... Avichukue Viwanda vyote MKAPA alivyoviuza vya TEXTILES vilikuwa labor intensive avifufue awapatie ajira vijana wa Dar ambao Majority ni Waislam... Wakiwa na kazi nzuri malazi mazuri -- SIJUI kama hayo Machafuko ya KIDINI yatakuwepo... kwasababu hata wa KIKRISTO pia watapata kazi pia wataacha kushinda makanisani na misikitini
 
Acha unafki na wewe kwamba hajua chazo ni nin,eti kashtukizia watu wanagombania kuchinja,umjue ni mnafki anasema'hili jambo nililiona toka muda mrefu nikalisema',sasa how come hajui chanzo
wewe unaejua chanzo hebu tueleze ilivyokua.
 
Haiwezekani tuwe na Kiongozi wa nchi asiyejua kiini cha matatizo yanayowasibu 'watu wake'. Amefanya juhudi gani kutafiti hata aje na majibu marahisi rahisi kwa tatizo gumu. Laikini hata pale alipodai bila kulazimishwa na mtu kuwa anawajua wauza madawa ya kulevya, ni hatua gani aliwachukulia? Nakerwa kuwa na kiongozi wa namna hiyo. Pengine hii ndiyo sababu Mnyika alimwita DHAIFU. Kwa nini wanaomshauri wasilione hili? Kama yeye hajui ngoja wenye majibu (Lema) waje wamjulishe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom