kwa nini mumfagilie mtuhumiwa mkuu wa ufisadi?hivi Tz imekosa watu makini kweli kwanza aje atuombe radhi kwa kutuingiza kwenye mkenge wa dowans na Richmond
"Matatizo tuliyo nayo leo hii yametokana na huu mtandao ulioasisiwa na Kina Lowasa na JK.Leo hii wapuuzi wengine wanatuaminisha kuwa EL ndio muarobaini wetu.
Naomba nipate majibu yafuatayo:
1:Ile hela iliyowekwa kama "Bond" na City water ilikwenda wapi?
2:Je,ni kweli walifukuzwa kwa kuto perform ,au ni kwasababu kiwanda cha kina EL cha mabomba kilipigwa chini ,kusupply mabomba na hao city water?
Kuna mabo mengi sana ya kujiuliza juu ya mtu huyu anayetumia fedha nyingi kujisafisha.
Tumeishapoteza miaka kumi.Hatuhitaji tena miaka mingine kumi.
Mfumo uliopo wa CCM ni laazima uondoke kuianzisha upya Tanzania Mpya.Ushabiki unaoletwa leo,ndio huuhuu walioingia nao wakati wa JK.Wakipata madaraka wanaanza kurudisha fedha zao badala ya kujali wananchi.
Kwa mtizamo wangu huyu jamaa aliisha poteza fedha nyingi kwenye siasa ,kwa hiyo anataka kuzirudisha ,kwa njia ya mikataba feki.
wao kama wanamtandao waliisha pata nafasi ambayo wameichezea,hatuhitaji kufanya majaribio upya.Muda hautusubiri.