Kikwete azidiwa jukwaani, akimbizwa mapumziko

Nashanga kweli, tatizo liko wazi kwa nini mkulu asichukue muda kulitafutia ufumbuzi na kumalizana na haya majinamizi ya kuanguka anguka hovyo?
 

Babu mwanakjj mbona unanishitua mjukuu wako hapo nilipobold pananitia utata
 
Mhhhh je Ni Kweli wanavyosema Mtaani na Watu wengine Kuwa Pale Kulikuwa Na UPAKO?/\
 
Huyu Bwana siyo mzururaji bali ni mchapa kazi anayewajali wananchi. Hivi mlitaka akae Ikulu huku wakuu wa wilaya na mikoa wakidanganya hakuna njaa ingali watu wanakula mizizi? Tumwombea apate afya njema.
 

Mkuu mwanakijiji heshima mbele.

Tafadhali tunakuomba uje jamvini hii maneno kuhusu afya ya mkuu wa kaya inatutatiza wajukuu zako.

Binafsi nimekuwa na mashaka makubwa na afya ya mkuu wa kaya mara ya mwanzo wapinzani wake wa kisiasa walikuwa wanavumisha ana ngoma lakini wakati wa ile kampeni aliyoizindua ya kupima ukimwi pale mnazi mmoja uvumi ulikwisha.

Ugonjwa wa mtu ni suala la faragha lakini mtu mwenyewe anapokuwa Rais wa nchi faragha inawekwa pembeni hasa tukitilia maanani majukumu na uzito wa nafasi ya Rais kwa taifa changa kama Tanzania.Bila shaka Muungwana alikuwa na ugonjwa unaomsumbua kabla hajawa Rais wa JMT naomba kuuliza swali dogo hakuna utaratibu wa kupima afya ya mtu anayegombea nafasi ya Rais?.Leo hii ukiomba kazi hata ya ukarani ni lazima uchekiwe afya kabla ujaanza kazi,vipi katiba yetu haisemi chochote au tume ya uchaguzi hawana utaratibu wa kuwacheki afya wagombea.
 
raisi wetu inabidi apunguze safari za kuunganisha i know he working hard kwasababu anatakiwa kupunguza majukumu ya nyumbani na serikali and he need time to rest kwasababu nchi bado ni maskini kutoka kwenye wimbi hili inahitajika kuondoa mafisadi wote
 
kachoka kwa sababu ya kwenda marekani!!!!!!!!!!!!!!!!!!....
 
hapana ni kiongozi muwajibikaji sana,kiasi cha kuogopa kudelegate kwa VC,PM na wengineo.
pole sana mpendwa baba Chodo na Mungu akupa nafuu.
 
Wauliza Mwanza kuna nini? mshaurini kuwa kila anapoenda kwa watani zake Mwanza ni lazima atoe nondo zake zote za ukwereni aziache Dar, kwenda nazo ni hatari kwani zikiumana na za kisukuma reaction yake ndio hiyo!

Mkuu Kadushik,

Kikwete ni Mkwere. Na Wakwere historia yao ni "Wanyamwezi waliolowea Bagamoyo/Pwani". Sasa basi pamoja na kulowea, bado wanakumbuka asili yao au tuseme mababu zao ni akina nani (hapa ninamaana ni sisi). Kwa kuowanisha hilo utagundua kuwa Mkwere na Msukuma ni mtu na MTOTO WAKE. Mkwere hawezi kuwa na utani na MSUKUMA/MNYAMWEZI na kimila ni kuwa Wakwere inabidi wawaheshimu saaana Wanyamwezi/Wasukuma.
 
Kumradhi wakuu, hivi alivyoanguka pale Jangwani kuna mtu anaweza kunikumbusha ilikuwa tarehe gani? Mwaka si tatizo, tarehe na mwezi pls
 
Kumradhi wakuu, hivi alivyoanguka pale Jangwani kuna mtu anaweza kunikumbusha ilikuwa tarehe gani? Mwaka si tatizo, tarehe na mwezi pls

mkuu sina jibu ila ninamchango unaoweza kusaidia ktk kutafuta jibu. Kikwete alipatwa na mkasa huo ktk mkutano wa mwisho wa kampeni (funga kampeni). Uchaguzi ulifanyika December 14, 2005. Mwanzo ulipangwa kufanyika tarehe 30 October lakini uliahirishwa. Hivyo Kikwete alipatwa na matatizo hayo Mwezi December 2005.
 
Nadhani wapambe wake JK wangekuwa wanatumia busara zaidi kusisitiza kuwa Mheshimiwa apimwe afya yake .

Kazi ni kubwa .. Ni jana tu kakiri jinsi alivyo mbishi anaposhauriwa na watu.
 
Thanks mkuu Nemesis,

Nimepata details toka kwa mtu alokuwa kwenye kampeni na muungwana mwaka 2005. Ilikuwa tarehe 13, Disemba 2005.
 
Kazi ni kubwa .. Ni jana tu kakiri jinsi alivyo mbishi anaposhauriwa na watu.

Lakini wapambe nao wasimtie kiburi kwa kusema eti haumwi... anaumwa na ni kitu serious, akapime afya na atafute matibabu sahihi.
 
Isee watanzania we need to pray for our president awe na afya njema.
 
Isee watanzania we need to pray for our president awe na afya njema.

Mwenyezi Mungu, Muumba wa Mbingu na Nchi tunakuomba umponye Rais wetu mpendwa J.M. Kikwete; Mpe afya ya Kiroho, nafsi na mwili, mwezeshe aweze kuwatumikia watu wako wa Tanzania kuanzia sasa hadi 2015.

Tunaomba hayo kwa Jina lako Mungu wetu. Amen.
 


pale jangwani ilikuwa PLACEBO....hakupimwa mtu pale..that was just awareness campagne.....

uvumi kuwa hana ngoma aliukanusha pale ....ofisi ya ccm kibaha wakati akitangaza kugombea urais mwanzoni mwa mwaka 2005......akamsimamisha na mkewe kukanusha kuwa hawana ngoma[lakini ni siri yao-ni afya yao]...pamoja na kuwa maadui zake serikalini walikuwa wakisema walikuwa na ushahidi na hilo....ni vigumu kuwaamini moja kwa moja...siri anaijuwa yeye!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…