Kikwete awatisha Wakatoliki kwa kusaini Muswada wa Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete awatisha Wakatoliki kwa kusaini Muswada wa Katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nikupateje, Dec 8, 2011.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  ***************************************

  SOURCE: TANZANIA DAIMA
  DATE: DECEMBER 08, 2011 (Today)
  PAGE: FRONT PAGE
  SUBHEADINGS: Wahofia kuvunjika amani, Washangazwa na Uamuzi wa Bunge, Wasema Nyerere amesahaulika

  ***************************************

  Kanisa Katoliki nchini (TEC) limeshtushwa na hatua ya Rais Jakaya Kikwete kusaini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011, harakharaka kwa kuwa kunaweza kuipeleka nchi pabaya.

  Akizungumza jijini juzi na TANZANIA DAIMA muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa kitabu cha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, kilichoandikwa na John Kasembo, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Askofu Mkuuu Jude Thadaeus Ruwa’Ichi alisema Watanzania wengi walitaka muswada huo usisaniwe, na kwamba mkuu huyo wa nchi alipaswa kusikiliza mawazo ya wananchi wake, na si kuwahi kusaini na kuwa sheria, Rais huyo wa TEC alisema kitendo cha Serikali kukusanya maoni mikoa ya Dodoma, Dar-Es-Salaam na Zanzibar peke yake, haitoshi kujenga hoja ya kusaini ama kupitisha muswada huo wa Katiba.

  Askofu Ruwa’Ichi alisema suala la kuundwa kwa Katiba mpya si hiari ya Rais wala kikundi na tabaka Fulani bali ni la watanzania wote.

  Rais huyo wa TEC ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza alisema hatua ya kulipeleka suala la Katiba mbindembinde linaweza kuipeleka nchi kubaya na Kanisa Katoliki halitaki Watanzania wafike huko.

  Alisema walitegemea Kikwete angethamini na kujali maoni ya wadau wengine, lakini katika namna ya ajabu hakuonekana kujali chochote. Ruwa’Ichi ambaye alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika uzinduzi wa kitabu hicho, alieleza kushangazwa na kitendo cha Bunge kupitisha harakaharaka muswada huo.

  “Hivi Bunge linashughulika na maslahi ya nani? Wabunge wamepewa dhamana na wananchi, hivyo ni lazima wawasikilize wanachotaka, halafu ndicho wakifanyie kazi, na si kuonekana kama ushabiki fulani”, alisema Askofu Mkuu Ruwa’Ichi.

  Alipoulizwa kuhusu suala la udini linaloonekana kutumiwa na baadhi ya wanasiasa nchini, Askofu Ruwa’Ichi alikiri kuwapo kwa jinamizi hilo, na kusema ajenda ya udini kwa sasa imekuwa kama kichaka cha watu Fulani kuficha maovu yao.

  Alionya kwamba iwapo serikali itaruhusu mijadala ya dini kutawala nchini, basi taifa lipo hatarinikupoteza ustawi wake, na akataka watu wasitumie mgongo wa dini kuficha madhambi yao.

  Katika hatua nyingine, TEC imesema mambo yote mema yaliyotendwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere yametupiliwa mbali, na sasa kila mtu anatenda lolote linaloonekana kuwa na manufaa kwake.
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Serikali imesema itatoa fursa kwa wananchi wote kutoa maoni yao juu ya swala la katiba. Je Wakatoliki si Watanzania? Pia kauli hiyo imetolewa na taasisi ya Kanisa Katoliki haimaanishi kila mkatoliki nchini atakua na mawazo sawa na uongozi wa kanisa lao.
   
 3. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Daima mwenye busara hutoa maneno yenye busara. Safi sana baba askofu. Tunataka viongozi ambao wanathubutu kusema bila woga si wale wanosema kwa maslahi ya kikundi au chama fulani. Waumini tupo nyuma yako. Ila na sis tunasikiliza maneno yenye busara na yanayo jenga tu na si vinginevyo.
   
 4. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Kwanza rais si ndiye mwenyekiti wa "Catholic Church Movement". Sasa wanamlalamikia nini mwenzao.
   
 5. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo mwenzako akikosea hupaswi kulalamika au kumkosoa siyo?? Hayo mawazo ya kiCCM ndiyo maana hatutaendela. Mambo ya zidumu fikra za Mwenyekiti................ ndiyo hayo unayotuletea!! Unafikiri hao maaskofu na mapadri wao sio raia wa nchi hii siyo??
   
 6. crome20

  crome20 JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 831
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  Aliye kuroga ameisha kufa.
   
 7. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,006
  Likes Received: 2,658
  Trophy Points: 280
  Mkuu achana na mwendawazimu huyo,atakuumisha kichwa bure.
   
 8. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #8
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Kweli hekima haifichiki,busara nayo pia!nchi ni yetu sote watanzania na siyo mali ya ccm wala ya Kikwete,na siyo mali ya dini flani!hongera baba askofu kwa kuwatoa wengine tongotongo!labda watafunguka sasa.
   
 9. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hakika ukiwa mjinga na ukajikubali na ujinga wako, kamwe hutaziona fursa za kujinasua ktk ujinga wako kwa kuwa umeukumbatia. Hebu angalia hapo nilipokubadilishia rangi kwenye utumbo uliopost hapa, halafu jijibu swali dogo tu: Shida yako ni kutoa maoni au kuona kuwa yapo mazingira yatakayowezesha maoni yako kufanyiwa kazi?

  Kama serikali hii hii imekuwa ikikusanya maoni juu ya mambo mbali mbali na kuyaweka kapuni, leo hii tutakuwaje na imani na maneno tu ambayo siku zote yameahidiwa na yasitekelezwe? Rais aliyeshindwa kuwadhibiti wauza sukari kwa ahadi za kuwachukulia hatua ataweza kuwadhibiti maafisa wake watakapoanza kuipeleka katiba kwa mtindo wa kifisadi?

  Mara nyingine tutumie akili zetu na sio kuunga mkono vitu bila kufikiri kwa sababu za woga au kutojiamini. Kama unaona serikali ina nia njema ktk kusaini huu muswada ilhali kuna manung'uniko lukuki, hebu niambie serikali ingepungua wapi kama ingeusoma kwa mara ya kwanza bungeni (kama kanuni inavyosema) na kuacha umma uujadili?

  Mtu mwenye akili zake timamu, hawezi kumsikiliza dobi anayejiandaa kutia nguo zake kwenye maji machafu kwa kuwa tu dobi kasema 'usiwe na wasi wasi ndugu mteja, haya maji ni masafi tu na nguo zitatakata' wkt dhahiri unayaona yana tope.

  Kaa ukijua kuwa kuna watu wamedhamiria kuhakikisha lengo na kuwa na katiba itakayoweza kuwawajibisha mafisadi halifikiwi. Hata mimi nakubali kuwa uwezekano wa kutoa maoni ni mkubwa, lkn msijitahidi kupotosha maana ya sisi wanaharakati kwa kutumia ukosefu wa elimu wa watu wengi. Hatusemi kuwa maoni hayatatolewa, tunachodai ni mazingira ya uwajibikaji na mgawanyo wa majukumu.

  Nasisitiza tena Watanzania wenzangu: TUTUMIE AKILI ZETU. Hawa wanaoendesha huu mchakato kwa ubabe wa wingi wa viti bungeni wana wanalonufaika na katiba mbovu itakayotungwa, sisi tunaodhulumiwa kila kukicha kwa EPA, RAD, DOWANS, MEREMETA na mengineyo tusiunge mkono kwa kuambiwa nganjera za amani ambayo kiukweli hatunayo. Wanachofanya ni kuhakikisha hakitungwi kitu kitakachowawajibisha kwa mabaya waliyoifanyia nchi.
   
 10. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  watanzania , hivi nyie hamjui kuwa katiba ikibadilishwa kwa manufaa ya wananchi ni sawa na kuwa, kaburi la nyerere halitatawala nchi? Kafariki lakini kaburi lake bado linaendelea kutawala!!!! muungano haubadiliki, kiingereza hakirudishwi mashuleni,ujamaa bado utaendelea kutawala na kuongoza nchi,TUCTA kutokuwa na nguvu, na wazurulaji kutokupata kazi!
   
 11. R

  RMA JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo kwa maoni yako unapendekeza nini? Wakae kimya? Hebu tuelimishe basi: ungependekeza akina nani ndio wawe na uhuru wa kuongelea katiba?
   
 12. i

  iMind JF-Expert Member

  #12
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Kesho utasikia ndugu zetu wakitoa tamko la kupongeza rais kwa kusaini mkataba.
   
 13. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #13
  Dec 8, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Vua hicho kilemba jua lipige kichwani ubongo uchangamke. Chokochoko haziletwi na kanisa bali na serikali isiyotaka kuwajibika kwa wananchi wake. Wewe unaathiriwa na udini na huo unakufanya usione ukweli wa mambo. Uko radhi kuacha haki zako zipotee kwa kuwa tu kanisa ndio linazipigania. Hii vita dhidi ya serikali dhalimu si ya kanisa, hata wewe inakuhusu. Askofu ametoa tu mawazo na wewe toa yako lkn sio kumshutumu kuwa analeta fujo.

  Ngoja sasa nikuoneshe udhaifu wa ubongo wako.
  1. Fujo za Syria na Lebanon zinasababishwa na kanisa au wananchi wanaodai haki kutoka serikali yao dhalimu?
  2. Majeshi ya wanamgambo wa Janjaweed yanayoua wasudan wasio waarabui kwa ufadhili wa Omar Al Bashir yametumwa na kanisa?
  3. Serikali inaponyang'anya mashamba vijiji na kuwapa wawekezaji na baadae kunatokea migogoro na mauaji kama kule babati na mbeya wametumwa na kanisa?
  4. Tunataka katiba yenye kuweza kuwawajibisha watendaji wa EPA, RICHMOND, MEREMETA, KAGODA, POSHO, n.k, je haya yanaliathiri kanisa au mimi na wewe?

  Kuna mambo mengi na ya msingi ambayo ungeyafikiria kwanza usingeandika utumbo na kuupost kwa kuwa tu unajua ku-type.
   
 14. s

  shukia Member

  #14
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Serikali imesema itatoa fursa kwa wananchi wote kutoa maoni yao juu ya swala la katiba"

  Kama serikali ingekuwa na nia ya dhati kusikiliza maoni, muswada usingesainiwa. Kungekuwa na tatizo gani kama muswada usingesainiwa ili wenye maoni watoe na marekebisho yakafanyika?
   
 15. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #15
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ANGEKUA AMESEMA SHEHE UNGESHADADIA NA KUMUUNGA MKONO! Mwanamke badilika acha udini na propaganda za kizee!
   
 16. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #16
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  "wote wamepotoka hawana hekima wala maarifa tena. Ni heri kijana mwenye hekima kuliko mzee mpumbafu ambaye hawezi tena kupokea maonyo"

  Kiongozi wa kweli ni lazima awe na uwezo wa kukemea uozo unapotokea bila woga wowote.
   
 17. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #17
  Dec 8, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Kama huyo mtu ni mwendawazimu nahisi wewe ni mwendawaazimu.
   
 18. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #18
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo lako la msingi hujui nini maana ya muswada na ni nini kimo ndani ya muswada huo ambao tayari rais ameshausaini kuwa sheria. Uvivu wa kufikiri ni hatari kama mtu huwezi kujiuliza maswali kwa nini muswada huo ulipelekwa mkuku mkuku bungeni na rais akasaini haraka haraka. Unasema serikali imesema itatoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao, lakini wewe hujui kama kwa mujibu wa sheria hiyo tayari imewekwa mipaka jinsi ya kutoa maoni, kama vile unavyomruhusu mbuzi kula majani lakini kwa sheria ya urefu wa kamba.
   
 19. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #19
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,953
  Likes Received: 1,279
  Trophy Points: 280
  utakuwa Mpemba wewe!
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Kanisa ni taasisi kwa hiyo wakitoa tamko ni kwamba ndio kauli ya waumini wao, ambaye yupo kinyume na kauli ya kanisa anaweza akashiriki katika makundi mengine kama Watanzania wengine.
  Lakini nijuavyo mimi Kanisa na CCM ni kitu kimoja huwa wanatofautiana kwa vitu vidogo sana, na ukitaka kuamini kauli yangu angalia wana CCM wote wanaoota Urais kampeni zao wamezielekeza kanisani, wanajuwa wakishakubalika na kanisa Biashara imekwisha, Bakwata unawaweka sawa viongozi wasiozidi 10 tu basi kura za waislamu zinamiminika
   
Loading...