Kikwete awatisha Wakatoliki kwa kusaini Muswada wa Katiba

Waswahili walisema penye 'udhia penyeza rupia', hivyo kelele zikizidi, peleka mchango wa ujenzi wa kanisa - Kwishney
 
Kwa hiyo, if one is tried is it necessarily that one committed the offence? Mara ngapi watu wanakuwa tried na baadaye kuwa acquitted? Halafu katika mazingira kama waliyokuwamo mapadre, masista nk ambao ilikuwa ni lazima watoe hifadhi kwa watu wanaokimbilia kwao ilichukuliwa kuwa kwamba kama wale waliokimbilia walikuwa 'aggressors' basi hata waliowapa hifadhi walijumuishwa kwenye kosa hilo na si rahisi padre au sista ajue nani ni aggressor na nani siyo maana wote wanakuja in great numbers na unachotakiwa ni kuwapa hifadhi. Na pale padre au sista alipoogopa kutoa hifadhi kwa kudhani waliokimbilia kanisani walikuwa 'aggressors' kama ilitokea kwamba baadaye waliuawa hata huyo padre au sista aliyekaa kuwapa hifadhi alichukuwa kuwa sehemu ya tatizo (kusababisha mauaji). Kwa mazingira kama hayo, ni unfair kutoa 'blanket judgement'.

Utajisumbua tu na huyu mama wa kipemba hana sera. Majuzi hapa somebody Uhuru1 kamuuliza hoja nzito zenye mashiko kuhusu CCM kala kona, sana sana akaishia kuongea utumbo na kujibishana na wasio na hoja. Ni kitu kama anatumiwa au ni CUF hasa hasa, yaani nikimaanisha mke wa CCM
 
alshabaab-new2.jpg
03_obama_terry_clip_image002.jpg

al-shabaab.jpg

Kweli dini ngumu, kumbe hata magwanda ya kufanyia ugaidi nayo yanatakiwa yawe njiwa(suruali fupi). Huyu mama anayetusumbua hapa yaelekea mumewe yupo ktk hili grupu lililotumwa na KANISA
 
Faiza Foxxy kuwa muungwana kidogo, tutafsirie hayo maandishi hapo kwenye bendera ya KANISA la Rwanda.
 
Wengine watakula muda wa kujadili mambo yaliyo muhimu tokana na misimamo yao ambayo si rahisi kubadilika. Mtu akisha toa jambo lisilo na maana - Leave him/her alone.
 
Kesho utasikia ndugu zetu wakitoa tamko la kupongeza rais kwa kusaini mkataba.

BAKWA-Kibatari sio?Haha tumewazoea,sio wabunifu kama UEFA,walisubiri magwanda waende magogoni nao wakajipanga,the same to hawa jamaa,husubiri wenzao waongeee then wao wanafuata.Avator hii inawafaa sana
 

Kikwete awatisha Wakatoliki
• Wahofia kuvunjika kwa amani

na Sitta Tumma, Mwanza
Tanzania Daima




KANISA Katoliki nchini (TEC) limeshitushwa na kutishwa na hatua ya Rais Jakaya Kikwete kusaini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011, harakaharaka kwa kuwa kunaweza kuipeleka nchi pabaya.

Akizungumza juzi jijini Mwanza na Tanzania Daima muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, kilichoandikwa na John Kasembo, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Jude Thadeus Ruwa'ichi, alisema Watanzania wengi walitaka muswada huo usisainiwe, na kwamba mkuu huyo wa nchi alipaswa kusikiliza mawazo ya wananchi wake, na si kuwahi kusaini na kuwa sheria.

Rais huyo wa TEC alisema kitendo cha serikali kukusanya maoni katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar peke yake, haitoshi kujenga hoja ya kusaini ama kupitisha muswada huo wa Katiba.

Ruwa'ichi alisema suala la kuundwa kwa Katiba mpya si hiari ya rais wala kundi na tabaka fulani, bali ni la Watanzania wote.
Rais huyo wa TEC ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza alisema hatua ya kulipeleka suala la Katiba mbindembinde linaweza kuipeleka nchi kubaya na Kanisa Katoliki halitaki Watanzania wafike huko.

Alisema walitegemea Kikwete angethamini na kujali maoni ya wadau wengine, lakini katika namna ya ajabu hakuonekana kujali chochote.

Ruwa'ichi ambaye alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika uzinduzi wa kitabu hicho, alieleza kushangazwa na kitendo cha Bunge kupitisha harakaharaka muswada huo.
"Hivi Bunge linashughulikia masilahi ya nani? Wabunge wamepewa dhamana na wananchi, hivyo ni lazima wawasikilize wanachotaka, halafu ndicho wakifanyie kazi, na si kuonekana kama ushabiki fulani.

Alipoulizwa kuhusu suala la udini linaloonekana kutumiwa na baadhi ya wanasiasa nchini, Rais huyo wa Baraza la Maaskofu alikiri kuwapo kwa jinamizi hilo, na kusema ajenda ya udini kwa sasa imekuwa kama kichaka cha watu fulani kuficha maovu yao.

Alionya kwamba iwapo serikali itaruhusu mijadala ya udini kutawala nchini, basi taifa lipo hatarini kupoteza ustawi wake, na akataka watu wasitumie mgongo wa dini kuficha madhambi yao.

Katika hatua nyingine, baraza hilo limesema mambo yote mema yaliyotendwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere yametupiliwa mbali, na sasa kila mtu anatenda lolote linaloonekana kuwa na manufaa kwake.

Katibu Mtendaji wa Idara ya Liturjia ya TEC, Prelato Monsinyori Julian Kangarawe, alisema Watanzania wengi wakiwemo viongozi wameshindwa kudumisha maisha ya uadilifu na mwenendo mwema aliokuwa nao Mwalimu Nyerere wakati wa uhai na utumishi wake.

Kangarawe aliyasema hayo jana katika ibada ya ufunguzi wa kongamano la siku tatu la kutetea uhai linaloendeshwa na Shirika la Kutetea Uhai Tanzania (PRO-LIFE) iliyofanyika katika kitongoji cha Boko, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

"Huko nyuma watu walifuata nyendo za Mwalimu na maadili aliyoyataka lakini baada ya kuondoka watu wamebadilika na kuacha maadili yake na kufuata njia zao ikiwemo kuwa mafisadi wakubwa wanaojilimbikizia mali," alisema.

Kangarawe alisema ili kurejesha heshima katika nchi, ni wajibu wa kila Mtanzania kushiriki bila woga kutoa maoni yao katika uundwaji wa Katiba mpya ya Tanzania ili itetee na kupinga mambo maovu, likiwamo suala la utoaji mimba na kutambua haki za uhai wa binadamu.

Kiongozi huyo wa kanisa alisema viongozi na watu walio na madaraka wanapaswa kuiga maisha ya watakatifu kama vile Mtakatifu Ambrose, askofu na mwalimu mkuu kwa kufuata nyendo zake za kutoruhusu sera za utoaji mimba kwa kisingizio cha ongezeko la watu duniani.

Alisema msimamo wa Kanisa Katoliki duniani chini ya uongozi wa Papa Benedict wa XVI ni kupinga kwa nguvu zote utoaji mimba na linawataka watu bila kujali tofauti ya dini zao kulinda uhai wa mwanadamu.

Naye Mratibu wa Kanda wa shughuli za kutetea uhai katika nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza (Angrophone for Africa), Emil Hagamu, alisema kuwa wameamua kuandaa kongamano hilo ili kutoa maoni na mchango wao utakaosaidia katika uundwaji wa Katiba mpya itakayokataa kuhalalisha utoaji mimba.
Hagamu alisema kuwa shirika lao lipo kwa ajili ya kuhakikisha kila binadamu anapata haki ya kuishi tangu mimba inapotungwa, kwani wanaamini uhai huanza siku ya kwanza ya utungwaji wa mimba.

 
Nadhani wasaidizi wa Rais huwa hawasomi magazeti ya habari zaidi ya yale ya udaku. Hivyo hawaoni mambo kama haya.
 
Back
Top Bottom