Kikwete 'awapakazia' viongozi wa dini biashara ya madawa ya kulevya

Code:
Hivi karibuni wapo viongozi wa dini wamekamatwa kwa rushwa, ngono na kutuhumiwa kujihusisha na vitendo mbalimbali ambavyo ni kinyume na maadili yasiyo tegemewa na jamii kwa ujumla, wapo ambao wameshakamatwa na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria, wapo wanaochunguzwa, tumeshawashuhudia na bado wataendelea kushuhudiwa. Hili si jambo dogo la kujitetea kwa kauli nyepesi kutoka kwa watu wanaotegemewa na jamii kwa kumpa Rais saa 48.

Tatizo kwa JK hii mifano yote aliyoitoa pamoja ya kuwa ni ya kweli amechemsha sana kwa sababu hakuna hata mfano mmoja alionao wa viongozi wa dini kukamatwa wakijihusisha na madawa ya kulevya....................................mbona mashkhe hawagusi..................au anamaanisha ya kuwa ni viongozi wa kikristu tu ndiyo wanakabiliwa na tuhuma hizi.............................by the way can the real JK stand up na kutuelezea what happened to the list of drug baros he was handed to....................................


Huyu dawa yake ni kumwotea kwenye kona ya 2015 tulimalizie hilo li chama lake la porini ambalo liko ICU. Anajibu kijeuri namna hii siyo basi naye aonyeshwe jeuri na lichama lake lisijaribu kuwaomba kura wauza unga ifikapo 2015. Maaskofu hivi JK asipokuwepo Askofu hasimikwi? Kuna siku atajisaidia kwenye altare huyu ndo mtakoma kumwalika mcheza kiduku madhabauni
 
Pengine watu wanadhania viongozi wa dini ya kikristo ni rc, kkkt na anglikana tu, si kweli
Ukienda mambo ya ndani utapata kujua kuna madhehebu mangapi hapa tanzania, unaweza kuzimia lakini hawa wote ni wakristo, kuanzia pengo hadi mtu alienzisha kanisa lake porini huko na akalisajili wote ni viongozi wa dini.

Na kwa taarifa yako hakuna taasisi zinazoongoza kuingiza madawa kama za makanisa maana wao wanapata misamaha na mizigo yao inaaminiwa kwa kigezo cha misaada ya makanisa.

Mbona hujasema Islam yenyewe sio dini? Wao hawapati misaada?
 
Jaman huyu jamaa alishawahi kusema anawajua wauza unga na majina yao anayo,aliongea mwaka 2006,hadi leo hajawataja,halafu mwaka 2009 alisema anawajua wapokea rushwa mamlaka ya bandari,hadi leo yupo kimya jeee bandar hakuna rushwa???je madawa hayaingiii,je kesi za hao wanaokamatwa zinaishaje?
 
Well done Premi ! mie mwenyewe nilishangazwa kuona Mokiwa anataka watajwe , hili si jukumu la Rais kuna vyombo vya usalama ndio kazi zao hizo. Na wengine wameisha kamatwa pia, je Mokiwa hawajui ?. mie hapo ndipo ninapooona uwezo wa viongozi wa dini kufikiri siku hizi unaathiriwa na matashi yao ya kisiasa. Na Mokiwa anajulikana ni mfuasi mkubwa wa Chama Cha Demokaya na Magwanda

Tujuze hayo majina...mbona mnazunguka zunguka kama pia!..magamba bwana kaazi kwelikweli
 
usicheke sana, ntakunulia hijabu na kanzu kwa ajili ya kufichia pilau...

mwenyezimungu ni mwenye kusikia na kuhifadhi kila dharau na vicheko vyako kwetu sisi waislam,haya yote unayotamba nayo hapa kuzalilisha mavazi yetu sisi waislamu utayakuta yenye kudhihirishwa kwako pindi utakapoanza maisha ya ukweli baada ya kufa,,weye jitape tu kwenye maisha haya ya maigizo hapa duniani
 
Ni kweli Haswa baadhi ya maustaadhi wamezidi kulawiti watoto wa madrasa. Na mbaya zaidi ni pale baadhi ya maustaadhi wanapojidai kwenda kuswali kumbe ni asusa ya waumini wenzao wenye tabia za ulawiti.

Nadhani kichwa chako kidogo kina walakini si vibaya kumuona psychiatrist, umetawaliwa na dhana za UDINI, suala la kulawiti ni udhaifu binafsi hakuna DINI inayokubaliana na matendo machafu ya viongozi wa dini ambao wamepewa dhamana ya kuwalea watoto wetu, labda nikuulize unajua ni kiasi gani mpaka sasa KANISA KATOLIKI limelipa kwa kesi za kulawiti? HILI NI TATIZO LA UDHAIFU WA KIROHO HALIHUSIANI KABISA NA MAFUNDISHO YA DINI ZETU.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
hapa ndipo makanisa yanapokuwa na nguvu. ccm ikitishwa kidogo na makanisa yanakuwa taharuki. mbona huwa kimya kwa waislam?

maaskofu si vyombo vya usalama. Ni kazi za police kutafuta nani muagizaji wa madawa ya kulevya na kuwafikisha mbele ya sheria. Hiyo statement ya mkuu ni ya kuwadhalilisha kwa kiasi kikubwa hawa watu. Huwezi sema kitu kikubwa kama hicho kwa ujumla. Anatakiwa awataje anaowatuhumu na si kusema ki ujumla. Ni maoni yangu binafsi.
 
Upuuzi kiasi hiki! Bora asingeandika jina lake hapo chini! Ameonyesha uwezo wake wakufikiria unaaishia wapi! Unatetea nini?
 
haya majibu ya kijinga awapelee watoto wa chekechea

Tulitaka rais atusaidie kutaja ili tuwaondoe kwenye huduma ya kanisa wahusika in case sheria ichukue mkondo wake.

Tabia ya Maaskofu kumwalika JK ikome manake ni hawa maaskofu wanaoonesha kujipendekeza kwake.
Maaskofu wawaalike viongozi wanaotumia akili na sio matumbo kufikiria

chaguo la Mungu.
 
Taarifa hii kama imeandikwa na mwandishi wa raisi, kweli imekosa vigezo vyote vya kuwa taarifa iliyotoka kwa raisi. Taarifa hiana mshiko na hakuna ilichosema kimantiki. Kikwete kuwa makini na wasaidizi wako, hao wanakwangusha.

Mbona kila kosa mnasingizia wasaidizi? Mnajuaje kuwa hawakuwambiwa hivyo? Kama hujui hayo ndo matunda ya semina elekezi.
 
Hayo ndo madhara ya kuwa na raisi kilaza mropokaji..shuwainiiiiiiiiiiiiii!!!!!!!

Baadhi ya miropoko yake ni hii
1. sizitaki kura za wafanyakazi
2.maisha bora kwa kila mtanzania
3.kila kata kuwa well equiped sec school
4.kila mtz kuwa na ajira
5. ...rais bush kasifia mistari ya jeshi letu imenyooka...
 
Baadhi ya miropoko yake ni hii
1. sizitaki kura za wafanyakazi
2.maisha bora kwa kila mtanzania
3.kila kata kuwa well equiped sec school
4.kila mtz kuwa na ajira
5. ...rais bush kasifia mistari ya jeshi letu imenyooka...

Mgao wa umeme na tatizo la maji Dar vitakuwa historia
Kila shule ya sekondari Tanzania itaunganishwa na mkongo wa mawasiliano wa internet
 
sijaona ubaya wa hotuba ya rais.kwani watumishi wa mungu ni maaskof tu??? Viongozi wa dini zingine siyo watumishi wa mungu?????
 
siyo wanahaha kumwokoa, Mokiwa kachemka kwani rais mpaka anaongea ujue isue ina ushahidi. Ila hawezi kurupuka na kutaja majina kama mokiwa anavyoota mchana, kwani ujue akimtaja tu vyombo vingine vinatakiwa chukua hatua ya kumkamata. sasa chukulia kuwa amemtaja ni askofu mwala au kadinar na kisha vyombo husika wakawakama ivi hali itakuwaje? je wafuasi wao watakubali moja kwa moja kuwa viongozi wao siyo watuhumiwa na wasizue vurugu? jibu ni hapana watazua vurugu kwahiyo hawezi kurupuka kuwataja kama Mokiwa aotavyo,ila kama anajijua anafanya aache kwani wanawajua.

Unajua Mr. Mak umejieleza kama mtoto wa chekechea na ukadhani unaongea na watoto wa chekechea. Unataka kutuambia kuwa Rais anatumia busara kwamba anao ushahidi wa wauza madawa, mafisadi na majambazi lakini hachukui hatua kwa sababu eti mhusika ni Askofu. Kama sheria haijasema kuwa wavunja sheria wakiwa maaskofu waachwe, hayo unayotueleza yanatoka wapi? Ndiyo maana anapambana na mafisadi lakini akiulizwa ni kina nani anasema hawafahamu. Rais ni msanii na wewe unataka kutuingiza katika usanii huo
 
kitu huna uhakika nacho bora kunyamaza tu.tamko la rais ni kama sheria so watu wanamsikiliza kwa makini kila neno analosema.siyo razima awataje yeye,anweza mtuma hata Ruhanjo akawataja tu.sioni sababu ya kuonea aibu waharifu wakati sisi vijana tunateketea.ni kweli serikali ya ccm inawajua wanaouza madawa coz tangu enzi za Amina chifupa alishasema anawajua.na juzijuzi kuna Mbunge alishutumiwa na uongozi wa ccm kama anauza madawa eti kisa amewambia wajivue gamba.je wamemchunguza?
 
Jamani ukiona Rais ametamka hivyo, huwezi kujua makubwa yaliyopo nyuma. Huenda anawajua wanaojihusisha lakini hakuna ushahidi wa kuwashtaki mahakamani. Ni sawa na hizi kesi zingine za ufisadi. Wapo wanaoshutumiwa lakini hawajachukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa hakuna ushahidi wa kutosha. Hilo liwe onyo kwa watumishi wa Mungu wanaotumia utumishi wao kupitisha madawa ya kulevya. Nina uhakika vyombo vinavyohusika vikiwa na ushahidi wa kutosha wanaohusika watashtakiwa.

Kauli ya Rais ni kauli ya mwisho, rais akishatamka ujue kuna vyombo mbalimbali vimefanyia kazi jambo hilo kama usalama wa taifa, polisi, Takukuru na hata JWTZ. Rais Obama alipotangaza kifo cha Osama alikuwa na ushahidi wote hivyo tunamuomba rais awataje maana ameyadhalilisha madhehebu ya dini na kibaya zaidi amesema wengine wamewakamata hivyo ni vyema awataje ili arudishe imani kwa waumini na watumishi wa Mungu, vinginevyo tutampuuza na kumudharau. Ametudanganya sana alisema list ya wauzaji anayo, aliwapa majambazi muda wa kujirekebisha mpaka leo haujaisha na mambo kibao, wasaidizi wake wamemchoka na sisi tumemchoka!!
 
Back
Top Bottom