Kikwete 'awapakazia' viongozi wa dini biashara ya madawa ya kulevya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete 'awapakazia' viongozi wa dini biashara ya madawa ya kulevya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 6, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Rais Kikwete alisema kuwa baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakishiriki biashara ya dawa za kulevya kwa kuwafanya mipango ya kuwatafutia vijana hati za kusafiria kwenda nchi za kufanya biashara hiyo.

  Kutokana na hali hiyo aliwataka viongozi wa dini kukemea biashara hiyo na kujenga uhusiano mzuri na vyombo vya dola kuhakikisha biashara hiyo haramu inakomeshwa kwa kuwafichua wahusika wanaofanya biashara hiyo ili wachukuliwe hatua za kisheria.
  nje

  “Inasikitisha sana na kutisha biashara hii haramu sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu, Taifa letu litaharibika tusipokuwa makini katika hili, baadhi yenu tumewakamata”, “Kauli zenu kemeeni jambo hili kwa kuelimisha jamii hususani vijana waweze kuepuka na matumizi ya dawa ya kulevya,” alisema Rais Kikwete.


  Majira
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Again, Rais Kikwete analalamika badala ya kuchukuwa hatua? What's wrong with this president? hivi anajua wajibu wake ni nini? Biashara ya madawa ya kulevya ni kosa, na sheria zipo? Sasa analalamika nini? Nani anatikiwa kulishughulikia hili?

  Na anaposema wakemee maana ya kukemea ni nini? Huko nyuma alishawahi kusema anawajuwa watu wanaouza madawa ya kulevya. Hivi kisheria mtu ukiwa na taarifa za uhalifu lakini ukaa kimya si kosa kisheria?

  Yeye kang'ang'ania kumkamata Mbowe huku analalamika watu kuuza madawa ya kulevya. Kwa upande mwingine nahisi hii ni another pre-emptive move. Something may come out soon.

  Mwanzoni alianza na 'kuna udini' sasa anakuja na viongozi wa dini, matope -matope for 2015.
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  Alishajifia siku nyingi, kosa ni wewe kulalama milalamo ya Kikwete badala ya kufanya kitu wapinzani waingie Ikulu. I mean that dont dance to his tune never even think about him, he is arleady looser!
   
 4. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Ombwe la uongozi linazidi kukua katika nchi yetu. Ukiona muuza dawa za kulevya Mzee m k w e r e tuma vijana wako wa wakamate na kupeleka mahakamani na sio kukemea au kulalamika. Tunakemea mambo ambayo si makosa ya jinai. Miaka 10 bila Rais je tutasalimika watanzania?
   
 5. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Imeandikwa leo kwenye vyombo vyetu vya habari kuwa Rais Jakaya Kikwete
  amewaonya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini hapa nchini kuacha
  tabia ya kushiriki biashara ya kuuza madawa ya kulevya na badala yake washirikiane
  na viongozi wa serikali katika kudhibiti biashara hiyo haramu.

  Alisema kuwa viongozi hao wa dini baadhi yao wamekuwa wakishiriki katika
  kufanya biashara ya madawa ya kulevya kwa kuwafanyia mipango vijana
  kuwatafutia hati za kusafiria kwenda nchi za nje kufanya biashara hiyo.

  Kadhalika aliwataka viongozi wa dini hapa nchini kukemea biashara hiyo na
  kujenga uhusiano mzuri na vyombo vya dola kuhakikisha kuwa biashara hiyo
  haramu inakomeshwa kwa kuwafichua wahusika wanaofanya biashara hiyo ili
  wachukuliwe hatua za kisheria.

  Hivi, ni aina gani ya kiongozi tuliyenaye ambaye hachukui hatua kazi yake kubwa
  ni kulalamika tu? Kama si mwaka huu mwanzoni basi ni mwaka jana alitamka
  kuwa majina ya wafanyabiashara wa unga anayo, kwanini hawachukulii hatua?
  Au ndo usanii!
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Dalili za kuchanganyikiwa mtu mwenye mafasi kubwa si lazima aokote makopo, uropokaji ni dalili tosha.
   
 7. N

  Nzogupata Member

  #7
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa dini naomba kusema kazi ya Mungu wanaifanya kunufaisha wanasiasa na woga wenu utawaponza. Akiwa Tabora alisema vita ya madawa ni ngumu. Ruvuma anasema viongozi wa dini wanahusika na hawajakanusha, misikitini na makanisani mnafanya nini?

  Yeye JK alishasema orodha anayo tangu anaingia madarakani na hakuwahi taja hata mmoja. Kwa maana nyingine kaanza kutaja viongozi wa dini na wengine wanafuatia ama ndo mwisho?

  Lakini pia atanabaishe wapi hao viongozi, au kwakuwa kasemea kwa wakatoliki tuamini kuwa maaskofu na mapadre ndo wanafanya biashara hiyo?

  Kama sivyo hajawahi lisema hili msikitini ama zamu yao bado.
   
 8. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kama rais analalamika, viongozi wengine wafanye nini? Mbona alishasema kuwa majina ya wafanyabiashara ya dawa za kulevya yote anayo? Kwanini asichukuwe hatua badala ya kuishia kulalamika? Anamuogopa nani?
   
 9. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  JK hafanyi tathmini ya mambo anayoongea. Alipoingia madarakani 2006 alitamka hadharani kuwa anayo majina ya watu wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. Mpaka sasa hakuna hata mtu mmoja aliyekamatwa na hajaweza kuiweka hadharani hiyo list.

  Nafikiri badala ya kuwasingizia viongozi wa dini atueleze watanzania hiyo orodha ya wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya ameifanyia nini mpaka sasa ama ameamua kumalizana nao kimya kimya kama alivyofanya kwa wezi wa EPA.

  Tumeshachoshwa na kauli zake bora ajinyamazie tu.
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hujajua Kikwete ni mwerevu wa habari za kutunga? Alianza na udini, kaja na ukabila, kaendelea na uhaini, na leo anakuja hili la kuwapakazia viogozi wa dini kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
   
 11. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Sure! Hii maana yake ni kuanza kufilisika kisiasa kwa kutafuta kuonewa huruma. Aibu!
   
 12. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Hii niliisikia na ilinishtua kwani rais anapaswa kuwa na Busara kwa mambo sensitive kama haya hasa unapokuwa huna ushahidi.
  Huu ni mchemsho mwingine utakaomgharimu JK kwa siku zijazo kwani najua alimlenga hasimu wake mkuu Kadinali Polycapi Pengo. Mbona asiseme siku nyingine na badala yake ameonyesha kukosa adabu na madharau makubwa ambayo ni sawa na kwenda kumtukana mtu akiwa nyumbani kwake.

  Inabidi aulizwa alikuwa na maana gani na kwa kiaongozi muungwana inabidi aende mbali zaidi ktk kuonyesha wahusika wakubwa. Hivi leo pinda angetoa hotuba kama hiyo ndani ya baraza la kiislamu angetoka salama bila kula bakora kweli?.

  Inabidi washauri wa rais wampeleke hata darasa la kujifunza busara kama ya asili imegoma kwani kwa rais mwenye busara huwezi toa shutuma mzito namna hiyo. Mimi nachukulia haya kama matusi kwa dini ya katoliki kwani ingekuwa analenga viongozi wa kiislamu na wakristo basi angetoa hii hotuba mwisho wa mwezi kama kawaida yake. Kwa hili ni dhahiri alildhamiria kabisa kumweleza pengo live.
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nadhani Kikwete alijuwa fika kwenye ibada lazima maaskofu wangempa vidonge vyake live! Sasa kwa kujihami akaandaa 'kombora' la majungu. Kwa fitna na majungu huyu rais wetu yumo, na kutokana na tabia yake hii CCM inamfia.

  Sote tunakumbuka Salim Ahmed Salim, Rais mzima bila aibu unasimama kuwaambia wananchi kuwa una majina ya wahalifu? Mambo gani haya? Na kosa kubwa ni hili, kajichagulia safu ya washauri ambao wanamwambia yale anayotaka kusikia.

  Matokeo yake ni migogoro kila kukicha, sio ndani ya CCM, sio kwa nchi. Sasa naelewa ni kwa nini moja ya miiko/kiapo cha TANU ilikuwa 'nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko.
   
 14. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha na kukatisha tamaa sana rais wa nchi anapokuwa MZUSHI na MROPOKAJI
   
 15. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hopeless
   
 16. senator

  senator JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  [​IMG]
  Hapa kama baba askofu anaonesha unyenyekevu kwa mkuu na kuahidi kutekeleza yote atakayo agizwa nae!
   
 17. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  title na body haviendani.......!!
   
 18. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Kama wanahusika na biashara ya madawa ya kulevya na ushahindi upo si wakamatwe mara moja? Au ni harakati za kuwatisha?
   
 19. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Samahani kama nitawaudhi wengine; but is it true that JK is our Prseident or just a symbol of complaints? Sijui anatatizo gani huyu "Kijana"? sasa kama amewakamata kaishia wapi nao? ....anatia kinyaaa
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kama umewahi kupitia darasa la wahariri ungejua ugumu wa kuandaa kichwa cha habari, na ni kichwa gani cha habari unayokusudia kitaleta mvuto kwa wasomaji. Nadhani umenipata. Instructor wangu chuoni Creig Ashkraft alituambia darasani, ukitaka kuwa mhariri mzuri kazania ubunifu wa kichwa cha habari maana habari huna kazi nayo kwa vile unaandika unayoona, unayosikia na kusoma.
   
Loading...