Kikwete awajia juu mawaziri watukanao- | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete awajia juu mawaziri watukanao-

Discussion in 'International Forum' started by Ngongo, Apr 17, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Rais Jakaya Kikwete ameelezea kukerwa na vitendo vya baadhi ya mawaziri wa nchi za Afrika Mashariki kutumia lugha za matusi na kuikejeli Tanzania kutokana na msimamo wake wa kutokubali suala la ardhi na ajira liwe la Afrika Mashariki kwa sasa. Rais Kikwete alielezea masikitiko yake hayo juzi wakati akijibu maswali ya Watanzania waishio hapa wakati alipokutana nao katika Hoteli ya Riyadh Palace.

  Ingawa Rais Kikwete hakutaja mawaziri hao ni wa nchi gani, lakini hivi karibuni zimekuwapo taarifa kuwa baadhi ya mawaziri wa Kenya wamekuwa wakiikejeli na kupingana na Tanzania kwa msimamo wake wa kutaka suala la ugawaji ardhi kwa wananchi wa Afrika Mashariki lisiingizwe kwenye masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, bali nchi husika iwe na mamlaka juu ya umilikishwaji huo wa ardhi. Rais Kikwete alisema: “kinachonisumbua sasa juu ya suala hili ni jinsi linavyojadiliwa kwa kejeli, waziri tu anatukana nchi nyingine, lugha zinazotumiwa hazitasaidia kujenga Afrika Mashariki, silifurahii hili la kutukana nchi nyingine.

  “Kama hili la ardhi sasa haliwezekani tusigeuze kuwa kama hilo haliwezekani basi Jumuiya ya Afrika Mashariki haiwezekani, kama kwa sasa suala la ardhi ni gumu liachwe yafanywe mengine yanayowezekana na wakati ukifika litajadiliwa”. Mbali na hilo, Rais Kikwete ambaye alimaliza ziara yake jana, aliwambia Watanzania hao kuwa kutokana na hali ya mvua mwaka huu kutokuwa nzuri nchini, kutakuwa na upungufu wa chakula.

  Alisema uhaba wa mvua upo katika mikoa ya Pwani, Tanga, Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Morogoro na kuongeza: “Lakini tutajitahidi kukabiliana na uhaba huo”. Aliwaasa Watanzania hao kukumbuka nyumbani kwa kupeleka maendeleo na kuwasaidia ndugu zao na si kujisahau na wanaporejea nyumbani wanajikuta wakiwa na maisha magumu. Aliwataka waishi hapa kwa kuzingatia sheria za nchi na kuongeza: “Huwezi kuishi hapa kwa sheria zako, watakushughulikia, ukifanya makusudi kuvunja sheria hutatunyima usingizi, lakini ukionewa ubalozi utakusaidia”.

  Akijibu swali la Mtanzania aliyetaka kuanzishwe shule ya Afrika Mashariki ili watoto wasome kwa kufuata mtaala wa Afrika Mashariki, Rais Kikwete aliwataka mabalozi wa nchi za Afrika Mashariki kukaa na kuanzisha shule hiyo na serikali zao zitasaidia kupeleka mitaala ya kufundishia. Kuhusu uraia wa nchi mbili, alisema Watanzania wengi waishio nje wanalitaka hilo, na kwa sasa suala linafanyiwa kazi.

  Katika hatua nyingine, mke wa Rais, Salma Kikwete, aliwambia wanawake Watanzania wanaoishi hapa, kuwafundisha watoto wao utamaduni wa Kitanzania na lugha ya Kiswahili. “Asiyekuwa na utamaduni ni mtumwa, wafundisheni watoto utamaduni wa nyumbani na nyinyi kumbukeni kusaidia nyumbani,” aliwambia. Wakati huohuo, Rais amesema kuanzia sasa Tanzania itaanza kupata mikopo yenye masharti nafuu kutoka taasisi za fedha duniani kutokana na utendaji wake kuwa mzuri.

  Tanzania ni miongoni mwa nchi tano za Afrika zilizofanya vizuri kiutendaji ambapo Rais Kikwete alisema: "Kutokana na utendaji wetu mzuri mlango wa kupata mikopo sasa utafunguliwa na tutafanya maendeleo zaidi." Akifanya majumuisho ya ziara yake mjini hapa, Rais aliwataka wafanyabiashara wa Tanzania kujitayarisha kuchangamkia uwekezaji kutoka Saudi Arabia.

  "Tujitayarishe katika maeneo ambayo wafanyabiashara wa Saudi Arabia wameonyesha nia, mfano katika kilimo, ili wakija wakute watu wako tayari kushirikiana nao… wamesema wana dola trilioni 1.6 na kati ya hizo dola bilioni 60 wamezitenga kwa utalii nasi tutumie nafasi hiyo," alisema. Akijibu swali aliloulizwa sababu za utawala wake kupata misaada mingi kuliko mikopo, alisema: "Kila kitu kina wakati wake na kukaa kwangu miaka 10 nikiwa Waziri wa Mambo ya Nje, kumenisaidia kupata marafiki wengi ambao sasa wananisaidia kupata misaada katika nchi zao kama Marekani, Uingereza, Japan na Ufaransa".

  Alisema licha ya Tanzania kupata misaada kutoka Saudi Arabia kama kusaidia ujenzi wa daraja la Mkapa lakini bado haijatumia sawasawa fursa za kupata misaada hiyo na kuongeza kuwa sasa itaitumia nafasi hiyo. Alisema ziara hiyo ya kikazi ya siku tatu imekuwa na mafanikio na sasa Tanzania ina matumaini ya kuuza bidhaa zake Saudi Arabia.  Source;Habari leo
   
 2. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,081
  Likes Received: 1,728
  Trophy Points: 280

  1. Uraia wa nchi mbili siyo matatizo ya msingi ya watanzania kwa sasa. Na wala haliwezi kuwa suluhisho la matatizo yanayokabili nchi na wananchi wake. Acha! usitupotezee muda! Shughulikia mambo ya msingi ya maendeleo.
  2. 'wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia'... huu ni uswahili! Kuna mipango, malengo, mkakati gani? Hao waarabu wanaosemwa kuja kuwekeza wamejipanga, wamefanya utafiti na upembuzi yakinifu na hatimaye kuamua kuja kuwekeza Tanzania. Iweje wafanyabiashara wa kwetu 'wachangamkie'.. tu? Acha Uswahili.
   
 3. Sabode

  Sabode Senior Member

  #3
  Apr 17, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ila hata mimi sifurahii kejeli za mawaziri wa jirani zetu.
  wakati mwingine huwa naona upungufu mkubwa wa staha kutoka kwa wenzetu. pia nionavyo wanatumbulia sana macho ardhi yetu japo hatuja wakewa mazingira bora ya kuitumia lakini sioni haja ya kuiacha wazi kwa kila mtu kujimegea na hasa ninapo kuwa na hofu kuwa hata hao wakenya wa kawaida hawata nufaika isipokuwa wale wale waloo iba vyakula vya wanyonge na kujinufaisha . ikiwa heka mmoja wanafyatukwa na vitisho kuingia vitani sembuse za huku ? siliiungi mkono suala la ardhi kuingizwa katika muunganiko huu. HIVYO NDIVYO NIONAVYO MIE
   
 4. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2009
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  1: Ni wapi JK aliposema suala la uraia wa nchi mbili ni la msingi?
  2: Kuhusu wafanyabiashara wa TZ na wawekezaji wa Saudia mbona umeondoa neno "KUJITAYARISHA"? au kwako hili neno halina maana? JK alikuwa na maana gani kusema wafanyabiashara wa TZ WAJITAYARISHE kuchangamkia?
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mimi sijaona mantiki ya kuwakatalia Wakenya na Waganda kuja kulima lakini tunakimbilia kuwapa Wasaudi ardhi kwa miaka 99. Hainiingii akilini kabisa.
   
 6. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #6
  Apr 17, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Ukifika mwaka 2020 mkoa wa kilimanjaro utakuwa umekodisjhwa kwa wakenya , mwanza ni waarabu , kagera ni brazil , mtwara wareno dodoma hapo kwa waoman wote hawa watakuwa na mikataba ya miaka 99 kuendeleza kilimo
   
 7. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakenya na Waganda ni washkaji tu. "Ngozi nyeupe" ndo investor.
   
 8. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  At this rate, by 2070 tutakua tumeuza nchi yote kwa kaburu, mchina, mhindi na mwarabu. 2090 Waafrika wote tutaswekwa national parks, game reserves, sanctuaries and in zoos.

  Where is Mugabe when you need him?
   
 9. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,805
  Trophy Points: 280
  hodi .. hapa!
  nimevutiwa na huu msemo "URAIA WA NCHI MBILI" TZ itakuwa imefanya dhambi kubwa kama wakija kuruhusu hii kitu ya uraia wa nchi 2,
  tutakuja kupata mamluki ya wageni toka nchi nyingine, angalia wachina walivyozagaa hapa k/koo , wahindi ambao sio wazawa , waarabu, na watu wa matifa mbalimbali wakisubiri huu mlango wa uraia wa nchi mbili ufunguliwe,
  nchi yetu itakuja kukondaaa huku tukisokoa macho mali zikiamishwa nchi nyingine..

  ni hayo! tu! nipo safarani nilitua baraza hili kupumzika!
  salaam
   
 10. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Sisi huwa hatujui tunataka nini wapi na toka kwani na kwa maslahi ya nani.................tupo tupo tuu
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hahahaha
  naona unagawa urithi kabla hujahesabiwa na babu zako mkuu
  hahaha
   
 12. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,081
  Likes Received: 1,728
  Trophy Points: 280

  1. Kutamka tu kuwa serikali inashughulikia uraia wa nchi mbili ilihali kuna matatizo kibao ambayo serikali hiyo hiyo haionekani hata kuyashughulikia, mfano, elimu, afya, kuporwa kwa rasilimali, umeme vijijini, maji, rushwa, mipango miji mibovu na kadhalika, ni ishara kuwa serikali imekosa kubaini kipaumbele cha maendeleo ya Taifa. JK alipaswa aeleze adhira yake kuwa mambo ya uraia wa nchi mbili siyo kipaumbele cha taifa/serikali kwa sasa.
  2. Uwapi Mkakati mahsusi wa kitaifa unaotoa mwangozo kwa wafanyabiashara wanaohimizwa kujitayarisha? Hili ni jukumu la serikali ati! Siyo?
   
 13. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Nadhani ndugu zangu mnakumbuka jinsi mkapa alivyokuwa anachangamkia "ubinafsishaji" wa mashirika yetu ambayo sasa ndio tunagundua kuwa yaliuzwa kaw bei poa na sera yenyewe haikuwa na manufaa kwa nchi yetu; lakini ndio hivyo tumeliwa na there is nothing we can do to reverse the transactions!! Hivyo hivyo naona nae muungwana anafikiri kwa kuwakaribisha wageni anaowaita wawekezaji ndio nchi yetu itajikombomboa; HIVYO HIVYO KAMA ALIVYOFANYA MKAPA KWA MASHIRIKA YETU, kIKWETE NAE ANATAKA KUFANYA MCHEZO NA ARDHI YETU KWA KUWAPA WAARABU LAKINI ANAKUWA MKALI KWA WAKENYA NA WAGANDA NA WARUNDI; MCHEZO WA KUREKA REHANI ARDHI NI HATARI SANA KWANI MWISHOWE WANANCHI HAWATAKUWA NA PA KUEGEMEA MATOKEO YAKE hayatakuwa mazuri kwa mustakabali wa nchi yetu!!
   
 14. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ni kweli, kama tunawakatilia wakenya na waganda, halafu tunawapa waoman na waarabu wengine, wareno na wabrazil(kama ni kweli yasemwayo), itakuwa kuruka matope afu unakanyaga innya. au badala ya mtoto kukojoa anatita kabisa.....kikwete hatutaki ulete magaidi hapa bongo. ila hatuna shida, kwasababu wakileta za kuleta tutawatoa mkukumkuku wataondoka bila hata nguo.
   
Loading...