Kikwete awafanyie nini CHADEMA ili waridhike?

Kikwete awafanyie nini CHADEMA ili waridhike?

atekeleze ahadi zake ndio tunachotaka,,tunazikumbuka sana
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24. Kujenga bandari Kasanga � Rukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani � Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36. Kulinda haki za walemavu - Makete
37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38. Kujenga barabara Musoma � Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma � Kaliua,Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43. Kuwafidia wanakijiji ng�ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha � Arusha mjini
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti � Ngorongoro
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) � Ruvuma
64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania � Ruvuma
65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda � Mtwara
67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

Nimekukubali mkuu lakini ile ya kujenga bandari bagamoyo sijaiona!
 
kikwete awafanyie nini Kikwete ili waridhike?
yatokee kama ya MWEMBECHAI kama ya Mh Mkapa ndio chadema iridhike?

Nikupe tu taarifa aliyewaamrisha polisi wawapige risasi watu pale mwembe chai si mwingine ni YUSUF MAKAMBA mwislam mwenzenu. Nilikuwepo pale na nilimsikia kwa masikio yangu mwenyewe. Sijawahi kusikia akilalamikiwa hata siku moja. Vitu vya ajabu kabisa
 
kikwete awafanyie nini Kikwete ili waridhike?
yatokee kama ya MWEMBECHAI kama ya Mh Mkapa ndio chadema iridhike?
Hayo ya mwembe chai yatamtokea nani,kikwete wenu hana uwezo wa kufanya hivyo. Dhaifu na bogus mkubwa mkubwa kabisa huyo.
 
sio awafanyie nini chadema, ni awafanyie nini wananchi, afanye yafuatayo:
1) apunguze wizi kwa hizo 10% na makampuni ya mifukoni kama Richmond
2) aache kuzurura na akae kuwatumikia wananchi
3) akemee kwa dhati udini aliouanzisha na awe na mikakati ya dhati ya kuumaliza badala ya yy nae kulalamika
4) apunguze mfumuko wa bei
5) ajali maslahi ya wafanyakazi.

Nawasikitikia! Yaani naona mnapoteza muda wenu bure kwa hili.
 
Akae ofisini awahudumie watanzania,atafakari na apime,kama tuhuma za udini zinazotajwa kuwa ameziasis ni za kweli aachie ngazi kwa wanaoweza kuongoza nchi bila kugawa watz.wapo wengi ndani na nje ya chadema.afu awashugulikie watesaji na wale wote wanaon'goa wengine meno kwani anawafaham na wameshatajwa kuwa ni wateule wake
 
kikwete awafanyie nini Kikwete ili waridhike?
yatokee kama ya MWEMBECHAI kama ya Mh Mkapa ndio chadema iridhike?

Atekeleze tu ahadi yake aliyoitamka mwenyewe Maisha bora kwa kila mtanzania sio bora maisha kwa kila mtanzania anayotekeleza sasa. Kampeni ya kung'oa meno na kucha kwani haitoshi mpaka mrudi Mwembe chai? Kumbukeni kuwa sasa inaonekana watumiaji wa maembe na chai wamekuwa wamezaliana na wamekuwa wengi hivyo angalieni msije mkaandaa chache kuliko wahudhuriaji.
 
La muhimu ni kujîuliza WEWE RAIA umeifanyia nini TANZANIA
na sio kuuliza TANZANIA imekufanyia nini..
kaa chini tafakari..
 
Hoja kama hizi mufilisi,
kwani Kikwete alichaguliwa na chadema?
 
kikwete awafanyie nini Kikwete ili waridhike?
yatokee kama ya MWEMBECHAI kama ya Mh Mkapa ndio chadema iridhike?

Watu wanataka warudie ile hali ya Mzee Mkapa ya kula "beche" kila siku. Vile vile na kuenzi ule msemo wa TTB (Tanzania Tea Blender) wa "Kila wakati ni wakati wa chai". Mchele Sh 2,500; Sukari Sh 3,000! Watu wanakula mlo mmoja kama boko.
 
atumie risasi za Moto Miskitini kama awamu iliopita. hapo ndipo CHADEMA WATASEMA KIKWETE SIO DHAIFU.
 
Kwanza rekebisha thread, uliza awafanyie nini Watanzania na siyo chama cha siasa.Kwanza kwakuwa ndege wanaofanana mabawa wanaruka pamoja, naye alikuwa anaruka pamoja na Lowassa aliyejiuzuru kwa ufisadi.Basi tunataka atuambie fedha za umma zilizolipwa kupitia RICHMOND zitafidiwaje?
 
ajiuzulu kwa kuwa alipokuwa Uturuki alikiri mwenyewe ya kuwa ameshindwa kongonza nchi,

na ndo maana muda mwingi anaishi nje ya aridhi ya ya Tanganyika,

kwa miaka takribani saba tangu awe Raisi wa Tanganyika amelala Tanganyika kwa miaka mitatu tu. miaka minne amelala kwa wanaume wenzie kina OBAMA, CAMERON....
 
sio awafanyie nini chadema, ni awafanyie nini wananchi, afanye yafuatayo:
1) apunguze wizi kwa hizo 10% na makampuni ya mifukoni kama Richmond
2) aache kuzurura na akae kuwatumikia wananchi
3) akemee kwa dhati udini aliouanzisha na awe na mikakati ya dhati ya kuumaliza badala ya yy nae kulalamika
4) apunguze mfumuko wa bei
5) ajali maslahi ya wafanyakazi.


1) Hilo nakubaliana na wewe
2) Kwani hujui kwamba kuzurura kwake ni kwa ajili ya kuwatumikia wananchi??
3)Kwani husikii akikemea udini?? au umeweka pamba masikioni
4)Nakubaliana na wewe; isipokuwa Mfumuko wa bei haujasababishwa na yeye kwani hata angekuwepo Rias nani huo mfumuko wa bei ungekuwepo tuu. Hilo sio tatizo la Kikwete ila kama Rais anatakiwa akabiliane nalo, na kama utachunguza truly say limeshaanza kupungua, kwa mfana mimi nipo Kahama bei ya mchele imeshuka kutoka Tsh. 2,000/= hadi 1,200/=
5)Hamumtendei haki Kikwete kama mtasema kuwa hajali maslahi ya wafanyakazi, hakuna Rais Tz aliyejali maslahi ya wafanyakazi kama Kikwete, kipimo sahihi angalia mshahara kima cha chini kimeongezeka more than 100% katika uongozi wa kikwete.
 
Hata aje Rais mwingine yeyote, akiwa ni Muislaam, kosa.
 
Back
Top Bottom