Kikwete atoa taarifa ajali ya meli.

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
TAARIFA YA
MHESHIMIWA DKT.
JAKAYA MRISHO
KIKWETE, RAIS WA
JAMHURI YA
MUUNGANO WA
TANZANIA,
KUFUATIA AJALI YA
KUZAMA KWA MELI
YA MV SKAGIT
ILIYOTOKEA TAREHE
18 JULAI, 2012,
CHUMBE, ZANZIBAR
Jana tarehe 18 Julai,
2012, majira ya alasiri
kumetokea ajali ya
kuzama kwa meli ya
MV SKAGIT katika
eneo la Chumbe,
Zanzibar. Meli hiyo
iliyokuwa ikitokea Dar
es Salaam kueleka
Zanzibar ilikuwa
imebeba watu 290.
Kati yao watu
wazima 250, watoto
31 na wafanyakazi
wa meli 9.
Amiri Jeshi Mkuu,
Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete
aliagiza vyombo vya
ulinzi na usalama vya
Serikali ya Muungano
yaani JWTZ na Polisi
waanze kazi ya
uokoaji mara moja.
Kazi hiyo imefanywa
kwa kushirikiana na
vyombo vya usalama
vya Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar
na meli za
makampuni binafsi.
Mpaka giza lilipokuwa
limeingia na hivyo
kazi ya uokoaji
kusitishwa mpaka
kutakapokucha
tarehe 19 Julai, 2012,
watu 136 walikuwa
wameokolewa na
maiti 31 zilikuwa
zimepatikana. Aidha,
mali zilizokuwa
kwenye meli hiyo
hazikuweza
kuokolewa.
Kufuatia ajali hiyo,
Rais wa Jamhuri ya
Muungano
alizungumza na Dkt.
Ali Mohamed Shein,
Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar
na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi.
Alimpa pole kwa ajali
iliyotokea hasa kwa
vifo na majeraha
waliyopata
Watanzania wenzetu
na watu wasiokuwa
raia wa Tanzania.
Alimuomba afikishe
salamu za
rambirambi kwa
ndugu zetu
waliopotelewa na
jamaa zao na
kuwapa pole
waliopata majeraha
na maumivu
maungoni mwao.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano alisema
kuwa huu ni msiba
wetu sote na
kwamba majonzi yao
ni majonzi yake na ya
Watanzania wote.
Kwa ndugu zetu
waliojeruhiwa
tunawaombea kwa
Mwenyezi Mungu
awape ahueni na
wapone haraka ili
waweze kuendelea
na shughuli zao za
kujiletea maendeleo
na kulijenga taifa
letu.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa
Tanzania
amempongeza Rais
wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi,
Dkt. Ali Mohamed
Shein na viongozi
wote wa ngazi
mbalimbali kwa
uongozi wao thabiti
tangu taarifa ya
kutokea kwa ajali
mpaka sasa.
Aidha,
amewapongeza
maafisa na askari wa
vyombo vya ulinzi na
usalama na
wafanyakazi wa meli
binafsi, kwa juhudi
kubwa walizozifanya
za uokoaji wa ndugu
zetu waliopatwa na
maafa haya
makubwa na ya aina
yake. Amewataka
waendeleze juhudi
hizo leo na siku
zijazo.
Rais amewataka
wananchi wawe na
moyo wa subira na
uvumilivu wakati kazi
ya uokoaji inaendelea.
Kama ilivyofanyika
katika ajali ya MV
Spice Islander miezi
10 iliyopita, uchunguzi
wa kina utafanyika
kubaini chanzo cha
ajali.
Kutokana na ajali hiyo
na msiba huu
mkubwa, Rais wa
Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania,
Mheshimiwa Rais
Jakaya Mrisho
Kikwete,
ametangaza
maombolezo ya taifa
ya siku tatu ambapo
bendera zitapepea
nusu mlingoti kuanzia
leo, tarehe 19 Julai,
2012.
Asanteni sana.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Julai, 2012
 
Kichwa cha habari kimenichanganya. Ametoa taarifa au ametoa salam za rambirambi kwa Dr Shein?
 
Kwenye Maadui watatu Mwl. Nyerere aliokuwa anawapiga vita yaani
1.Ujinga
2.Maradhi
3.Umasikini

Tuongeze adui mwingine hatari sana:
4. viongozi(Washkaji zake,mademu zake,mashemeji zake,wakwe zake,binamu zake) wa serikali ya Jakaya
 
TAARIFA YA MHESHIMIWA DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
KUFUATIA AJALI YA KUZAMA KWA MELI YA MV SKAGIT ILIYOTOKEA TAREHE​

18 JULAI, 2012, CHUMBE, ZANZIBAR Jana tarehe 18 Julai, 2012, majira ya alasiri kumetokea ajali ya kuzama kwa meli ya
MV SKAGIT katika eneo la Chumbe, Zanzibar. Meli hiyo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kueleka Zanzibar ilikuwa
imebeba watu 290. Kati yao watu wazima 250, watoto 31 na wafanyakazi wa meli 9. Amiri Jeshi Mkuu,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliagiza vyombo vya ulinzi na usalama vya Serikali ya Muungano yaani JWTZ na Polisi
waanze kazi ya uokoaji mara moja. Kazi hiyo imefanywa kwa kushirikiana na vyombo vya usalama vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na meli za makampuni binafsi. Mpaka giza lilipokuwa limeingia na hivyo kazi ya uokoaji
kusitishwa mpakakutakapokucha tarehe 19 Julai, 2012, watu 136 walikuwa wameokolewa na
maiti 31 zilikuwa zimepatikana. Aidha, mali zilizokuwa kwenye meli hiyo hazikuweza kuokolewa. Kufuatia ajali hiyo,
Rais wa Jamhuri ya Muungano alizungumza na Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Alimpa pole kwa ajali iliyotokea hasa kwa vifo na majeraha waliyopata
Watanzania wenzetu na watu wasiokuwa raia wa Tanzania. Alimuomba afikishe salamu za rambirambi kwa
ndugu zetu waliopotelewa na jamaa zao na kuwapa pole waliopata majeraha na maumivu maungoni mwao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano alisema kuwa huu ni msiba wetu sote na kwamba majonzi yao ni majonzi yake na ya
Watanzania wote. Kwa ndugu zetu waliojeruhiwa tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape ahueni na wapone haraka ili
waweze kuendelea na shughuli zao za kujiletea maendeleo na kulijenga taifa letu. Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi
wote wa ngazi mbalimbali kwa uongozi wao thabiti tangu taarifa ya kutokea kwa ajali mpaka sasa. Aidha,amewapongeza
maafisa na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama na wafanyakazi wa meli binafsi, kwa juhudi kubwa walizozifanya za uokoaji wa ndugu zetu waliopatwa na maafa haya makubwa na ya aina yake. Amewataka
waendeleze juhudi hizo leo na siku zijazo. Rais amewataka wananchi wawe na moyo wa subira na uvumilivu wakati kazi
ya uokoaji inaendelea. Kama ilivyofanyika katika ajali ya MVSpice Islander miezi 10 iliyopita, uchunguzi
wa kina utafanyika kubaini chanzo chaajali. Kutokana na ajali hiyona msiba huu mkubwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ametangaza maombolezo ya taifa ya siku tatu ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia leo, tarehe 19 Julai, 2012. Asanteni sana.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Julai, 2012
 
Ilikuwa na abiria 290, 136 hai 31 maiti. mathematically, 290-(136+31)=123 wamelala baharini either wakiwa hai (5%) au tayari wameshakufa (95%). Duuuu? mbona balaa, hata mwaka haujaisha mamia waliteketea leo tuna the same story, ee Mungu tuokoe.
 
Zanzibar ni nchi sasa naamini!
 
Mmliki wa hii meli anajulikana?
bado miliki hajajulikana, hivyo serikali imeviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufuatilia suala hili.....kwa kushirikiana na sumatra na lile shirika la zanzibar, wakati huo huo bunge nalo kwa kushirikiana na baraza la wawakilishi litaunda tume kufuatilia jambo hilo ili lisijirudie tenaaaaaaaaaaa.
 
mMILIKI anajulikana ila hana ofice, so no where to trace the owner
 
Back
Top Bottom