Kikwete ateua Makatibu Tawala wapya saba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ateua Makatibu Tawala wapya saba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mpita Njia, Mar 21, 2012.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD]Telephone: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
  press@ikulu.go.tz
  Fax: 255-22-2113425


  [/TD]
  [TD="width: 118, bgcolor: transparent"][/TD]
  [TD="width: 284, bgcolor: transparent"]
  PRESIDENT'S OFFICE,
  THE STATE HOUSE,
  P.O. BOX 9120,
  DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: UTEUZI
  NA UHAMISHO WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA _________________________
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, leo, Jumatano, Machi 21, 2012 ameteua Makatibu Tawala wa Mikoa saba na kufanya uhamisho wa wengine watatu.Ifuatayo chini ni taarifa kamili iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue ikitangaza uteuzi huo:-

  A: MAKATIBU TAWALA WA MIKOA

  (i)
  Dkt. Faisal Hassan Haji ISSA, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa KILIMANJARO. Kabla ya hapo Dkt. Faisal alikuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

  (ii)
  Bibi Mariam Amri MTUNGUJA, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa MBEYA. Kabla ya hapo Bibi Mtunguja alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea.

  (iii)
  Bwana Eliya Mtinangi NTANDU, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa MOROGORO. Kabla ya hapo Bwana Ntandu alikuwaKatibu Tawala Msaidizi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Dar es Salaam.

  (iv) Bwana Severine Bimbona Marco KAHITWA, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa GEITA. Kabla ya hapo Bwana Kahitwa alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dodoma.

  (v) Eng. Emmanuel N.M. KALOBELO, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa KATAVI. Kabla ya hapo Eng. Kalobelo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasharui ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

  (vi) Bwana Hassan Mpapi BENDEYEKO, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa RUVUMA. Kabla ya hapo Bwana Bendeyeko alikuwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro.

  (vii) Dkt. Anselem Herbert Shauri TARIMO, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa SHINYANGA. Kabla ya hapo Dkt. Tarimo alikuwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.Uteuzi huu unaanzia tarehe 21 Machi, 2012. Wataapishwa Ikulu, Jumamosi tarehe 24 Machi, 2012 saa nne asubuhi.
  B: UHAMISHO

  (i) Bibi Mgeni BARUANI – Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro anahamishiwa Mkoa wa NJOMBE.

  (ii) Bibi Mwamvua A. JILUMBI – Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga anahamishiwa Mkoa wa SIMIYU.

  (iii) Bibi Bertha O. SWAI, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya anahamishiwa Mkoa wa PWANI.
  Balozi Ombeni Y. Sefue
  KATIBU MKUU KIONGOZI

  IKULU,
  DAR ES SALAM.

  21 Machi, 2012
   
 2. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
 3. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hao watendaji wanamsaidia rais utendaji kazi? Au nikifuta jasho kwa kukosa tucheo flani?
   
 4. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
  [TABLE="class: cms_table_MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD]Telephone: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
  press@ikulu.go.tz
  Fax: 255-22-2113425

  [/TD]
  [TD="width: 118, bgcolor: transparent"][/TD]
  [TD="width: 284, bgcolor: transparent"]
  PRESIDENT'S OFFICE,
  THE STATE HOUSE,
  P.O. BOX 9120,
  DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Hiki kiingeraza hapa wakati taarifa ni ya kiswahili
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Du!
  Anateua tu, hafuatilii wanachofanya!
   
 6. only83

  only83 JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Kha!! Kila kitu ni raisi!! raisi!! raisi!! katiba mpya inatakiwa haraka.
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  spilling of government revenues
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hata Hajua Qualification Zao; Mkoa wa Katavi Sasa Katibu ni Eng. na Mkuu wa Mkoa Eng.

  Nilidhani tuna upungufu wa Eng. nchini
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu , Mkuu awa Mkoa wa Katavi ni Mhandisi nani vile?
   
 10. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Katavi, njombe, geita, simiyu....hivi hii nchi siku hizi ina mikoa mingapi? Kuna mtu aweza nitajia?
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hoyo ni mikoa mipya Mkuu, imetangazwa hivi majuzi kwenye gazeti la serikali
   
 12. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ikulumawasiliano@yahoo.com

  Rywyemamu huyoooooo!!!!!
   
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  25 sasa(bara)
   
 14. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hii serikali sijawahi kuona upuuzi wa namna hii.........

  Mkoa wa Katavi una miwala mbili!!!......hii ni akili au dafu!!!
   
 15. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280

  Mkuu ni wilaya sio miwala
  Hiyo ni kumfurahisha PM anayetokea huko bana
  Si unaona mpaka uwanja wa ndege umejengwa kule mkulu akienda asichafuke vumbi
  Vipaumbele vya bongo ni kupeana ulaji tuu sio maendeleo
   
 16. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Halafu kuna mbuzi wanalipwa kama IT specialists
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  miwala mbili ndo nini?au una maanisha wilaya? khaa watu kweli mna hasira mpaka mnakosea kuandika kudadadekii
   
 18. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  alafu piga na gharama za kuwaweka hawa makatibu tawala huko kwenye vituo vya kazi, je wanafanya kazi gani pamoja na wakuu wa mikoa!?

  Jamani wakuu, ni muda wa kutoa sauti zetu ili katika mchakato huu wa katiba mpya wakuu wa mikoa waondolewe na hata ikiwezekana vyeo vingine visivyo na tija kwa nchi hii vifutwe.

  Kodi za Watanzanzania masikini haziwezi na sio busara kutumika kulipia fadhila kwa baadhi ya wapuuzi wachache

   
 19. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu watu wana hasira mbaya
  Kuona watu wanapeana ulaji tuu halafu maendeleo hakuna
   
 20. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ..Katika kazi ambazo Rais Kikwete anapenda kuzifanya ni hii ya Uteuzi, Sasa subirini Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya Soon.
   
Loading...