Kikwete ateua majaji wapya 10 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ateua majaji wapya 10

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by FDR.Jr, Jul 14, 2009.

 1. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Umetenda jambo jema kama mkuu wa nchi kwa kutungozea majaji; nathubutu kusema hadharani kuwa ni uteuzi makini kwa waliostahiki.

  Nimefurahishwa na ujasiri wako wa kutambua kada hii ya mahakama kama moja wa nguzo ya kuifanya legacy yako kujipambanua mapema mkuu.

  ** umewapa changamoto judiciary kuwa wajitahidi kutenda kazi na jicho lako litawaona pasipo kinyongo**

  this time 90% ni wa judiciary wenyewe.

  Songa mbele mkuu.

  Hongereni majaji wapya, kwa niaba yenu wote ninapitisha pongezi via mh.jaji mteule ferdinand wambari, mh.jaji mteule kalombora na jaji mteule prof....

  Habari yenyewe hii toka kwenye gazeti la Mwananchi:

  Rais Kikwete ateua majaji wengine 10 Mahakama Kuu

  Na Leon Bahati

  RAIS Jakaya Kikwete ameteua majaji wengine wapya 10 wa Mahakama Kuu ya Tanzania katika jitihada zinazoonekana kuwa ni za kutatua upungufu wa watendaji wa idara ya mahakama ambao umesababisha kesi nyingi kuchukua muda mrefu kutolewa uamuzi.

  Huu ni uteuzi wa tatu mkubwa tangu Rais Kikwete aingie madarakani mwaka 2005 baada ya kuteua kundi la kwanza la majaji 20 mwezi Desemba, 2006 na baadaye kuteua majaji 11 Mei mwaka 2008, huku akiongeza idadi ya wanawake hasa katika uteuzi wa mwaka jana alipoteua majaji saba wanawake.

  Katika ya majaji walioteuliwa, sita ni wanawake na hivyo kufanya majaji wanawake walioteuliwa tangu Rais Kikwete aingie madarakani kuwa zaidi ya 10 kati ya majaji wapatao 41 walioteuliwa na kiongozi huyo wa serikali ya awamu ya nne.

  Uteuzi huo umefanyika wakati tayari Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe akiwa ametangaza kuwa katika mwaka wa fedha 2009/10 serikali itaiimarisha idara ya mahakama kwa kuiwezesha kutumia vifaa vya kurekodi sauti ili kuharakisha usikilizaji wa kesi Mahakama Kuu.

  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, ilimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo akisema kuwa uteuzi huo ulianza tangu mwezi uliopita.

  Taarifa hiyo inawataja walioteuliwa kuwa ni Ferdinand Wambali, aliyekuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, Eliamnani Mbise, aliyekuwa Msajili Mahakama Kuu na Sekela Moshi, ambaye awali alikuwa mkurugenzi wa mahakama za wilaya hadi rufani.

  Wengine ni aliyekuwa mkurugenzi wa mahakama za mwanzo, Fatuma Hamisi Masengi, naibu msajili mwandamizi Mahakama ya Rufani, Sivangilwa Mwangesi, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Pellagia Khaday na msajili wilaya wa Mahakama Kuu Iringa, Moses Mzuna.

  Katika orodha hiyo ya majaji wapya, wapo pia msajili wa wilaya wa Mahakama Kuu Mbeya, Hamisa Kalombola, msajili wilaya wa Mahakama Kuu-Mwanza Fredrica Mgaya na mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Profesa Ibrahim Juma.

  Katika maadhimisho ya Siku ya Sheria Februari mwaka jana, Jaji Mkuu Augustino Ramadhan alitoa ombi kwa Rais Kikwete kushughulikia idadi ndogo ya majaji akisema kuwa ucheleweshwaji wa kesi utaendelea iwapo mahakama haitakuwa na watendaji wa kutosha.

  Kesi nyingi, hasa za mauaji, zimekuwa zikilalamikiwa kuwa zinachukua muda mrefu kabla ya kutolewa maamuzi na kusababisha baadhi ya watuhumiwa kukaa mahabusu kwa zaidi ya miaka mitano.

  Katika bajeti ya mwaka 2009/10 ya Wizara ya Sheria na Katiba, Waziri Mathias Chikawe aliahidi kuongeza idadi ya watendaji kwenye idara hiyo kwa lengo la kuharakisha utoaji wa haki.
   
  Last edited by a moderator: Jul 14, 2009
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu FDR Jr,

  Tafadhali naomba kupata majina ya majaji wote walioteuliwa na kama ikiwezakana uzoefu wa kazi,elimu na nk.eg source
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu FDR Jr bahati nzuri nimeyaona majina ya majaji wateule kwenye gazeti la Habarileo.


  RAIS Jakaya Kikwete ameteua majaji wapya 10 wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuanzia Juni 26 mwaka huu. Idadi hiyo inafanya majaji wa Mahakama Kuu kufikia 59, awali walikuwa 50, kabla ya kustaafu kwa Jaji Thomas Mihayo hivi karibuni. Mahakama ya Rufani ina majaji 16. Katika uteuzi huo mpya wa Rais Kikwete, majaji wanawake ni sita na wanaume ni wanne.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo jana Dar es Salaam, majaji hao ni Ferdinand Wambali aliyekuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, Eliamani Mbise aliyekuwa Msajili Mahakama Kuu na Sekela Moshi, aliyekuwa Mkurugenzi Mahakama za Wilaya hadi Rufani.

  Pia aliwataja majaji wengine walioteuliwa kuwa ni Fatuma Masengi aliyekuwa Mkurugenzi wa Mahakama za Mwanzo, Sivangilwa Mwangesi aliyekuwa Naibu Msajili Mwandamizi, Mahakama ya Rufani; Pellagia Khaday aliyekuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani na Moses Mzuna aliyekuwa Msajili Wilaya Mahakama Kuu, Iringa.

  Aidha, aliwataja majaji wengine wapya wa Mahakama Kuu kuwa ni Hamisa Kalombola aliyekuwa Msajili Wilaya Mahakama Kuu, Mbeya; Fredrica Mgaya, aliyekuwa Msajili Wilaya Mahakama Kuu, Mwanza na Profesa Ibrahim Juma aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria. Mei mwaka jana, Rais Kikwete pia aliteua majaji 11 wapya wa Mahakama Kuu huku saba kati yao wakiwa wanawake
   
 4. O

  Ogah JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kuteua Majaji si Suluhisho...........ni kuongeza gharama zisizo za lazima.....sikubaliani na hoja ya Jaji Mkuu...........

  ...............Suluhisho ni kufanya kila liwezekanalo kumaliza uhalifu na ufisadi
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Ila angalau itapunguza mlundikano wa mahabusu wa kesi kubwa kubwa....mauaji na wizi wa silaha na ujambazi.....wanajaana na wanakaa muda mrefu sana....hadi miaka 5 kesi haijaanza sikilizwa halafu unaachiwa inauma sana uonevu unakuwa ila wakiweza kupunguzaa hadi miezi 3 hadi 6 afadhali
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  kuwa na majaji wangi kunaharakisha kumalizika kwa kesi mbalimbali especially zile za jinai.

  Hongera JK
   
Loading...