Elections 2010 Kikwete atashinda bila majority ya wabunge

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Imenichukua zaidi ya siku mbili kuitafakari riport ya REDET waliyoitoa juzi kuhusu mwelekeo wa siasa nchini, mwanzo nilikuwa siiamini lakini nilipoiangalia kwa undani nimeona kuna ukweli fulani ndani yake ingawa si ukweli wote umewekwa wazi.

Ukweli wenyewe umefunikwa kwa ushabiki wa kisiasa zaidi, watu na hata magazeti mengi yameipokea ripoti hiyo kwa kusikiliza brief 'hints' zilizotolewa pale Maelezo na Dr. Killian bila details zenyewe, kuwa Kikwete atashinda kwa asilimia 77.2 bila kujiuliza baada ya kushinda serikali yake itakuwaje. Ningekuwa mimi Kikwete au mwanaCCM nisingekuwa na sababu ya kufurahia matokeo haya.

Ripoti imesema 2/3 ya wabunge wa chama chake hawatarudi bungeni ingawa hatujaambiwa sababu(utendaji mbovu?) wataenda wapi hata kama nusu ya hao watarudishwa na chama chake bado Rais atakuwa na wakati mgumu kupata support kubwa bungeni pindi anapotaka bills zake zipite.

Ripoti imesema
“Mgombea urais wa CCM anaonekana kupata kura nyingi zaidi kuliko kura za wabunge ambapo kiwango cha kura za wabunge kimepungua kwa asilimia tisa, kiwango cha kura kwa wabunge wa Chadema ni kikubwa mara mbili kuliko cha mgombea urais wake, wakati kwa CUF tofauti kati ya kura za rais na mbunge si kubwa sana,” alisema

Ukiichambua sentensi hii tu ni kusema kuwa, kama Kikwete atapata kura nyingi katika kila jimbo wagombea ubunge wa chama chake watapata shida sana kupita ndiyo kusema majority ya wabunge wake watashindwa hivyo kumpa wakati mgumu atakapoingia madarakani, inaniwia vigumu kuoanisha ripoti hii na hili wimbi la bunge la sasa kurundikiwa bills nyingi kipindi hiki cha lala salama zingine zikisomwa kwa kikao kimoja tu na kupitishwa kwani Kikwete anawasiwasi gani kuzi-table kwenye bunge lijalo?

Pia nimekuja kugundua kuwa REDET huwa wanafanya research vizuri lakini tatizo liko kwenye majumuisho ya ripoti zao sijui kama hii inafanywa makusudi au ni typical error.

There are two types of Research Report:A Written Research Report and An Oral Research Report, either of the two the writer must ensure that the report informs without misinforming. Kwenye research kuna kitu kinaitwa 'Iron Law', People would rather live with a problem they cannot solve than accept a solution they cannot understand'. Regardless of the research process, the project is a failure if the research report fails.

Hapa naweza kusema TEDET wanauwezo mkubwa wa Written Research Report lakini si Oral Research Report kwa sababu wanachosema kama alivyofanya Dr. Killian ni tofauti na kile wanachoandika, hata ukiangali ripoti hii kuna contradictions nyingi sana kwenye data zao na walivyo-ripoti pale maelezo, ndiyo maana nasema inawezekama wanafanya hivyo kwa makusudi kabisa ili kuipotosha jamii kwa malengo yao kitu ambacho ni hatari kufanywa na watu wasomi kama wa REDET.

Kwa REDET kufanya hivyo sijui wanamdangaya nani Kikwete na CCM au wanaidanganya Jamii, narudia tena sina tatizo na process za research ila jinsi REDET wanavyo communicate hizo research kwa jamii.

Naomba kutoa hoja.
 
Wabunge ata wakibadilika watakuwa wengine lakini CCM so majority ya chama chetu cha mapinduzi iko pale pale...lol :p
 
Luteni,

Nani kakwambia hao 2/3 ya wabunge wa CCM watakaoshindwa, nafasi zao zitachukuliwa na upinzani?

Inaelekea hujaielewa kabisa hiyo report, isome tena.
 
Watakaochukua nafasi za hao wabunge wa CCM watakaoshindwa ni wanachama wa CCM wengine. Vyama vya upinzani vinatakiwa kujiimarisha ili wachukue majimbo, wasikae mijini wawe na mitandao hadi vijijini ndiyo wanaweza kushinda majimbo mengi.
 
Luteni,

Nani kakwambia hao 2/3 ya wabunge wa CCM watakaoshindwa, nafasi zao zitachukuliwa na upinzani?

Inaelekea hujaielewa kabisa hiyo report, isome tena.
buckreef

Kwani wewe nani kakwambia hizo nafasi watabadilishana wabunge wa CCM kama mashati.
 
Hili halitawezekana maana utapangwa mkakati mzito wa wizi wa kura ambao utahakikisha Wabunge wa CCM wengi wanachaguliwa tena.
 
Hili halitawezekana maana utapangwa mkakati mzito wa wizi wa kura ambao utahakikisha Wabunge wa CCM wengi wanachaguliwa tena.
At least na wao sasa waanze kuwa na mawazo ya kupigania majority kuliko zamani ilivyokuwa inakuja automatically bila usumbufu.
 
Watakaochukua nafasi za hao wabunge wa CCM watakaoshindwa ni wanachama wa CCM wengine. Vyama vya upinzani vinatakiwa kujiimarisha ili wachukue majimbo, wasikae mijini wawe na mitandao hadi vijijini ndiyo wanaweza kushinda majimbo mengi.
Babalao,
Yaani katika uchaguzi huo watashindana CCM vs CCM?
 
Maswali waliyowauliza wananchi yako wapi?
Wewe fikiria mtu anaulizwa eti unaonaje utendaji wa serikari ya Kikwete na wapinzani wake sasa unategenea mtu atajibu nini, REDET wanaficha ukweli na maswali, tunataka methods of adminstering questionnaires kama sivyo tutachukulia research yao is a forced research ambayo ina malengo fulani simple.
 
Back
Top Bottom