Kikwete atangaza mikoa, wilaya mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete atangaza mikoa, wilaya mpya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Rais Jakaya Kikwete

  Exuper Kachenje, Dodoma

  RAIS Jakaya Kikwete ametangaza mikoa mitatu , wilaya, tarafa na halmashauri za wilaya mpya ili kuimarisha utawala bora.

  Kwa sasa Tanzania bara ina mikoa 26 hivyo kwa tangazo hilo la kusudio la kuanzisha mikoa mipya mitatu itafikia 29.

  Hata hivyo, Pinda alidokeza kuwa mazungumzo bado yanaendelea kuhusu uanzishwaji wa mkoa wa Mpanda na mkoa wa Arusha kupewa hadhi ya kuwa Jiji.

  Wakati hayo yakiwa yanaelezwa taarifa zinaonyesha kuwa gharama ya kuanzisha mkoa mpya ni kati ya Sh4 mpaka 6 bilioni na kwa
  wilaya mpya ni Sh1 bilioni.

  Gharama hizo zinajumuisha ujenzi wa makao makuu, kulipia gharama za uendeshaji, kuweka miundombinu muhimu pamoja
  na kuajiri watumishi.

  Kusudio la kuanzishwa kwa mgao huo mpya ulitangazwa bungeni mjini Dodoma jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokuwa akihitimisha hotuba ya Makadirio ya Bajeti kwa Ofisi yake ambayo ni Sh2.6trilioni. Bajeti hiyo ilipitishwa jana jioni.

  Kwa mujibu wa Pinda mikoa mipya itakuwa ni mkoa wa Njoluma, Simiu na Geita ambapo mkoa wa Njoluma utajumuisha maeneo ya Njombe, Ludewa na Makete.

  Mkoa wa Simiu unagawanywa kutoka mkoa wa Shinyanga na Geita.

  Kwa mujibu wa Pinda baadhi ya wilaya zinazokusudiwa kuanzishwa ni Butiama mkoani Mara, Mbogwe mkoani Rukwa, Nyang'wale, Ilemela na Ushetu mkoani Mwanza.

  Nyingine ni Kwela na Bulele mkoani Rukwa, Kaliua, Ikungi mkoani Singida, Kalambo, Ushelu, Gairo mkoani Morogoro, Mkalama, Nyasa mkoani Ruvuma na Uvinza mkoani Kigoma.

  Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, serikali pia inakusudia kuanzisha halmashauri za wilaya mpya ambazo ni Kaliua, Uvinza, Kakong'o, Kalambo na Mkalama.

  Nyingine ni Nyasa, Nyang'wale, Kahama, Masasi na Lindi.

  Hata hivyo, akitoa maelezo wakati wa kujadili vifungu vya bajeti ya Waziri Mkuu kabla ya kupitishwa, Waziri wa Nchi (Tamisemi)
  Celina Kombani alisema mikoa na wilaya hizo hazikutengewa bajeti kwa mwaka 2010/2011 kwa kuwa mchakato wa kugawa mipaka yake bado unaendelea.

  Alisema hatua ya kuanza kazi kwa mikoa na wilaya hizo zitapelekwa kwa rais ambapo pia wananchi watashirikishwa kabla ya kutolewa kwa notisi kwenye gazeti la serikali.

  Kikwete atangaza mikoa, wilaya mpya
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jun 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hongera JK, hapa ajira zitaongezeka na maendeleo zaidi yatawafikia wananchi!
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hiyo mikoa na halmashauri inasaidiaga nini?
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  acha wapitishe tu madudu tunasubiri waje mitaani baada ya miaka mitano tuwachague tena na hiyo ndo kazi yetu..........
   
 5. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ajira milioni moja ndo zitapatikana?
  mimi binafsi sioni kisababishi mbona mkoa wa kilimanjaro ni mkubwa na watu hali zao siyo mbaya?kuna sehemu hata ukifanya kata kuwa mkoa maendeleo hayatoonekana mpaka wazawa wadhamirie.....
   
 6. K

  Kikambala Senior Member

  #6
  Jun 19, 2010
  Joined: Jun 28, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kwa taarifa yako makofia mkoa wa kilimanjaro sio mkubwa unaizidi Dar tu
   
 7. K

  Kikambala Senior Member

  #7
  Jun 19, 2010
  Joined: Jun 28, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kuuita mkoa wa Njoluma haina maana uitwe mkoa wa Njombe inatosha ,ukiitwa Njoluma maana yake ni NJOMBE LUDEWA MAKETE,ila kuanzisha mkoa wa Njombe inastahili maana maendeleo yanaonekana dhahiri,makambako iwe wilaya mpya
   
 8. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Sielewe Buchanan, ni kwa vipi wingi wa mikoa utaleta maendeleo. Wakati wa mkoloni tulikuwa na majimbo machache na maendeleo yalikuwepo. Magari ya serikali Land Rover kama lile la the gods must be crazy lakini wakuu walizunguka kila kona ya province na Kila district. Hivi Sasa kila wilaya in VX V8 lakini zinaishia mijini tu.

  Ona mfano wa Kenya wana Mikoa sio zaidi ya kumi lakini kazi inakwenda uchumi unakua. Buchanan ukiangalia sana ni kuongezeka kwa kasma ya matumizi na gharana za kujenga hizo wilaya na mikoa at the expense of the projects. Hii ni zuga tuu uchaguzi umekaribia sasa tunapewa block satisfaction ooh huoni sisi ni wilaya, ohh sasa mkoa wakati hakuna maendeleo yoyote.
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Mpaka sasa sielewi ni vigezo gani vinazingatiwa kuanzisha mkoa na wilaya mpya.Kama ni ukubwa wa eneo basi wilaya ya Handeni mkoani Tanga ingestahili kugawanywa kwasasabu ina eneo kubwa sana.
   
 10. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Yote hii ni kuongeza viti maalumu na wabunge wa kuchaguliwa of new establshed majimbos bungeni.

  It's financed by tax payers money. just disapearing.

  Kilio cha samaki machozi huenda na maji masikini.

  Who's to advocate for poor majority??????
   
 11. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  anaongeza majimbo ya ccm tu hana lolote, lipi jema fedha za kuanzishia mikoa mipya na wilaya zingesaidia kuwasogezea huduma na shule vijijini mfano kule masasi, nangurukulu, nakang'ole, nakakunguruwe, n.k
   
 12. M

  Mkora JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu si walau waonekane wamefanya kitu
   
 13. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Yale yale tu hakuna jipya hapo ni kutengenezeana ulaji wa wakuu wa wilaya na mikoa wapya
   
 14. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  waafrika bwana!!..... vinchi vidogovidogo.... tumikoa twiiingiii tudogotudogo.... tuwilaya twiiiingiii, tudogotudogo, tutarafa, tukata, tuvijii nk.... twiiiiingiiii tudogotudogo..... ila hata uwe professor huwezi kuielewa falsafa yetu ya utaifa na maendeleo.....

  ccm bwana..... ila rafiki yangu mwanakijiji watamuua mwaka huu kwa kuwachambua, manake hajamaliza ya ccj wamefanya vitu vyao kwa mgombea binafsi na sasa mikoa na wilaya..... haya mkoa wa njokuma huoooo.... shimiyu..... na geita..... na mpanda iko mbioni... kabla jk hatamaliza kipindi cha lala salama ataleta na mkoa wa "vyuo vikuu"!!!!


  hahahah,.....
   
 15. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Tunaacha mambo makubwa ya maana tunafikiria vijambo vidogo vidogo tuuuu! Hata kila nyumba ikiwa mkoa bure tu!
  Hii ya sasa hawajaimudu kuitimizia mahitaji yake hata kwa 50%, inaanzishwa mingine. Baada ya uchaguzi itaanzishwa mikoa ya mpanda, chalinze, masasi, hata na monduli labda
   
 16. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  katika mgawanyo huo naona mkoa wa Morogoro umesahaulika kabisa. Badala ya kuongeza wilaya Mkoa wa Morogoro ulitakiwa kuganywa ili kuleta maendeleo. Kuanzia mto ruaha ungekuwa mkoa wa ulanga - kilombero ukiwa na wilaya za kidatu, ifakara, mlimba, lupiro na ulanga. Hiyo ingeleta tija. Mie nashangaa mawaziri na wabunge na watu maarufu kutoka wilaya za kilombero na ulanga mbona huwa wanakuwa bogus sana, wanashindwa kupigania mambo ya msingi ya wilaya hizo? ...... fanya utafiti: mawaziri na wabunge na watu maarufu toka katika maeneo hayo wamefanya nini ....
   
 17. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hivi kuanzisha mkoa mpya kuna tija au kunaongeza matumizi? ebu tembelea Babati makao makuu ya mkoa wa Manyara, hakuna hata hadhi ya kuwa Mkoa, tunajidhalilisha sana hasa tunapotembelewa na Wageni, eti unamwambia mgeni hapa ni mkoani, hebu tuige nchi za wenzetu, hata Arusha hapastahili kuitwa mkoa achilia mbali Jiji. tungeimarisha kile tulichonacho kiwe na hadhi kwanza kabla ya kurukia maeneo mengine, miundombinu ya mikoa mingi ni hovyo.
   
 18. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tuchambue:

  • Kwa sasa hizo sehemu inazalisha kiasi gani?

  • Je, zitazalisha kiasi gani kama tutaziingiza katika daraja la Mikoa na WIlaya?

  • Ulinganifu wa kimatumizi uko vipi na utakuwa vipi baada ya kuzibadilisha kwenda katika daraja lingine la mkoa na wilaya?

  • Kwa kuwa hii si mara ya kwanza kwa hili kufanyika, tungependa kupata tathimini ya mafanikio kwa mabadiliko tuliyo kwishafanya hapo awali (e.g, Kuanzishwa kwa Mvomero, Babati, Manyara n.k) kabla hatuna fanya uamuzi mwingine.

  If all these will not hold the positive significance, then the argument is simple and clear, it is just ".........divide and rule.....!?
   
 19. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...YOu just have to Laugh at WaBongo's Priorities! 'Watoto 21' ulionao wanakupa tabu kuwalea na umeshindwa kuwatimizia mahitaji ya lazima, you go and add another Three!!!:eek:
   
 20. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Hii inapigia mstari ile kauli ya Kikwete kwamba hajui kwanini watu wetu ni maskini.

  Ukweli ni kwamba serikali yetu haina think tanks wenye kujua what it takes kuiendeleza nchi, na ndio maana wanatapatapa na kutaka kufanya kila kitu and ending up doing NOTHING. Hatua tuliyofikia ilitakiwa tupitia hatua ya mpito na ku-priotise na kwenda direct kwene nyanja zinazogusa watu wengi wa chini na kati. Hakuna tena muda wa siasa, kupiga domo au kutaka kufanya kila kitu.
   
Loading...