Kikwete atangaza mikoa, wilaya mpya

Mimi binafsi sioni kwa nini watu wanafikiri kuongeza mikoa ndio kuleta maendeleo kivipi? Huku ni kuzidi kuongezeana umaskini kwangu mimi naona haikustahili iwe hivyo.... swala ni kuleta maendeleo kwanza kwa hii mikoa iliyopo na si kuongeza gharama. Huu ni ubinafsi wa baadhi ya viongozi wa hiyo mikoa mipya period...wenzenu wanaungana ninyi mnatengana hii nchi kweli imelewa lewa......
 
akuna maendeleo yanayoletwa kwa kuongeza mikoa mipya hata siku moja yote hii ni mbinu za ccm kushinda kwa kishindo hewa ya kupandikiza mapandikizi yao ili waendeleze madudu yao akuna lolote hapo
 
Hiyo mikoa na halmashauri inasaidiaga nini?
Mikoa na Halimashauri zinasaidia kupeleka madaraka karibu na wananchi. Hii husaidia kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi, huduma za kijamii, elimu, afya n.k. Wananchi hawawezi tena kuzifuata huduma hizo mbali maana kutakuwa mfano kwenye hiyo Mikoa mipya hospitali za wilaya na mkoa, Shule za sekondari n.k
 
akuna maendeleo yanayoletwa kwa kuongeza mikoa mipya hata siku moja yote hii ni mbinu za ccm kushinda kwa kishindo hewa ya kupandikiza mapandikizi yao ili waendeleze madudu yao akuna lolote hapo
Hii ni dhana ya Mtu binafsi na wale wote wasiopenda maendeleo na mafisadi. Kwa dhana halisi kuanzisha Mikoa na wilaya ni pamoja na kuwezeka mgawanyo wa madaraka kuanzia ngazi za chini na kupeleka huduma karibu na wananchi. Ila kwa kuwa pengine kutokana na ukumbwa wa nchi bora kungekuwa na majimbo badala ya kuongeza mikoa Ufatiliaji hasa wa fedha za umma unakuwa mdogo udanganyifu ni mwingi.
 
UJINGA WA VIONGOZI WETU..........MBONA hatangazi gharama kiasi gani zitaongezeka kutokana na kuongeza madudu hayo??????????????
halafu hawatoi takwimu zinazoonyesha maeneo amabayo yaligawiwa hivyo siku za nyuma na kuona kama kuna maendeleo zaidi ya awali.............
UBABAISHAJI UBABAISHAJI......ULAJI ULAJI...KUNA WATU WANATENGENEZEWA UKUU WA MIKOA/WILAYA/UKURUGENZI....SI MNAJUA HII NI NGWE YA MWISHO?????....KWA HIYO FULL KUTOA SHUKRANI KWA KUGAWA VYEO...SUBIRINI MUONE UTEUZI UTAKAVYOKUWA NA VIGHEZO VITAKAVYOTUMIKA....
KILICHOFANYIKA NI KUANDAA NAFASDI KWA AJILI YA WAWAPENDAO HAKUNA LOLOTE...TUTAKOMA NA KUWALIPIA KODI KILA MWEZI................
kikweteutabiri.jpg
Rais Jakaya Kikwete

Exuper Kachenje, Dodoma

RAIS Jakaya Kikwete ametangaza mikoa mitatu , wilaya, tarafa na halmashauri za wilaya mpya ili kuimarisha utawala bora.

Kwa sasa Tanzania bara ina mikoa 26 hivyo kwa tangazo hilo la kusudio la kuanzisha mikoa mipya mitatu itafikia 29.

Hata hivyo, Pinda alidokeza kuwa mazungumzo bado yanaendelea kuhusu uanzishwaji wa mkoa wa Mpanda na mkoa wa Arusha kupewa hadhi ya kuwa Jiji.

Wakati hayo yakiwa yanaelezwa taarifa zinaonyesha kuwa gharama ya kuanzisha mkoa mpya ni kati ya Sh4 mpaka 6 bilioni na kwa
wilaya mpya ni Sh1 bilioni.

Gharama hizo zinajumuisha ujenzi wa makao makuu, kulipia gharama za uendeshaji, kuweka miundombinu muhimu pamoja
na kuajiri watumishi.

Kusudio la kuanzishwa kwa mgao huo mpya ulitangazwa bungeni mjini Dodoma jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokuwa akihitimisha hotuba ya Makadirio ya Bajeti kwa Ofisi yake ambayo ni Sh2.6trilioni. Bajeti hiyo ilipitishwa jana jioni.

Kwa mujibu wa Pinda mikoa mipya itakuwa ni mkoa wa Njoluma, Simiu na Geita ambapo mkoa wa Njoluma utajumuisha maeneo ya Njombe, Ludewa na Makete.

Mkoa wa Simiu unagawanywa kutoka mkoa wa Shinyanga na Geita.

Kwa mujibu wa Pinda baadhi ya wilaya zinazokusudiwa kuanzishwa ni Butiama mkoani Mara, Mbogwe mkoani Rukwa, Nyang'wale, Ilemela na Ushetu mkoani Mwanza.

Nyingine ni Kwela na Bulele mkoani Rukwa, Kaliua, Ikungi mkoani Singida, Kalambo, Ushelu, Gairo mkoani Morogoro, Mkalama, Nyasa mkoani Ruvuma na Uvinza mkoani Kigoma.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, serikali pia inakusudia kuanzisha halmashauri za wilaya mpya ambazo ni Kaliua, Uvinza, Kakong'o, Kalambo na Mkalama.

Nyingine ni Nyasa, Nyang'wale, Kahama, Masasi na Lindi.

Hata hivyo, akitoa maelezo wakati wa kujadili vifungu vya bajeti ya Waziri Mkuu kabla ya kupitishwa, Waziri wa Nchi (Tamisemi)
Celina Kombani alisema mikoa na wilaya hizo hazikutengewa bajeti kwa mwaka 2010/2011 kwa kuwa mchakato wa kugawa mipaka yake bado unaendelea.

Alisema hatua ya kuanza kazi kwa mikoa na wilaya hizo zitapelekwa kwa rais ambapo pia wananchi watashirikishwa kabla ya kutolewa kwa notisi kwenye gazeti la serikali.

Kikwete atangaza mikoa, wilaya mpya
 
yani mnagawa iringa yetu??
afu iyo wilaya mpya ya ilemela mwanza?
mbona ilemela mwanza ni wilaya na ipo siku nyingi tu?

kwa lipi hasa izi mikoa?afu haya majina yao uwa wanainchi wanashilikishwa kuyabuni au ndo watawala?na maana zake ni nini hasa "SIMIU"??????????????????????
 
Back
Top Bottom