Kikwete apingwa

Dk. Bana ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Taasisi ya Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (Redet), alisema kuwa jambo analoweza kulifanya Rais kwa sasa katika kupambana na vita hiyo ni kutoa motisha kwa wale watakaowafichua watuhumiwa.

Alibainisha kuwa serikali inaweza kujipanga ikatoa motisha ya kati ya sh milioni tatu hadi tano kwa kila atakayetoa taarifa za wauza dawa za kulevya na wala rushwa ambazo zitathibitika kuwa za kweli.

"Kwenye jamii hawa watu wanaoitwa whistleblower's (wapiga vilimbi) wapo, hivyo wakipewa motisha watawataja wauza dawa hizo na wala rushwa ilimradi tuhuma hizo zithibitike ni za kweli," alisema

Dr Bana siku hizi naona uwezo wake wa kufikiri critically na kuja na solution zenye tija umepungua sana...yaani siku hizi kila akiombwa comment on sensitive issues anaongea bla bla blaaah hata msela wa Manzese stand tu pale ana pointi bora zaidi!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
"List of Shame"iliyotolewa pale Mwembe yanga na Rais wangu tangu mwaka 2007 amechukua
hatua gani? Si aanze kujishughulikia mwenyewe kwanza Watanzania tumemchoka!!!!!!!
 
Aah kumbe ni taarifa ya tanzania daima??
Itakua ni mwendelezo wa zile mbio zao za 2015...!!
Kila la kheriii,,,
 
Kuna magazi mawili siyapendi kwa sababu habari zake lazima ziegemee upande fulani. Hayo mageziti ni 'TANZANIA DAIMA' na 'UHURU'
 
Mkuu Riwa huyu jamaa namfananisha na Pascal Mayalla aka Pasco ambaye haishi kukurupuka na kuanzisha threads azake zisizo na mashiko hapa jamvini. Huyu jamaa kusema kweli anasikitisha na kustaajabisha sana...Kweli njaa mbaya sana!!!

Dr Bana siku hizi naona uwezo wake wa kufikiri critically na kuja na solution zenye tija umepungua sana...yaani siku hizi kila akiombwa comment on sensitive issues anaongea bla bla blaaah hata msela wa Manzese stand tu pale ana pointi bora zaidi!

Mkuu Pasco Mayalla

Pole sana nilikuwa sijakujibu muda mrefu maana naona kila siku anaangaika kwa ajili ya Zitto
Mimi ni CCM damu lakini nakuhakikishia kuwa Zitto anatumika wewe subiri true colour will show.......
Kama ilivyokuwa kwako baada ya kugundulika kuwa wewe ni mwanaCCM mwenzetu ukawa unasema
wewe ni independent advicer mara Political Analysist lakini yote kwa yote hakuna chochote na wewe your
true colour show at the end

Last:.................... Pasco Njaa Mbaya tujenge taifa letu tuache siasa za majungu................
 
Last edited by a moderator:
Mbona nape aliwataja lowasa, rostamu, andre chenge lkn haohao ndio wanaopeta ndani ya ccm....yaani kikwete kuwa rais basi anaona watz wote ni maboya tu.....siamini km kikwete yuko serious na maisha ya watz
 
Kikwete ni tatizo, hata hao mnaowaita washauri wake hamna lolote. Huwa anashauriwa halafu yeye anatumia ubabe.
 
Gazeti la Mwananchi leo.

Waarabu wamechukua hekta 2300 kwa kugawa unga kilo 2 kwa kila kaya katika Bonde la rufiji.

Eti wanakuja kulima miwa.

Kwani hao wanakaya si wangepewa heka mbili mbili wakalima miwa halafu wakauzia kiwanda kama mtibwa.

Kweli watanzania tumeuzwa.

Halafu hao hao waliopewa unga wataenda kuwa vibarua katika hayo mashamba.

What a shame to vasco da gama , pathetic leader
 
Unafiki mbaya sana, wa kupinga rushwa nani vile....................Thubutu...............
 
Huyu ni mwana ukome alishagoma kusikia jamaa huyu ni balaa sijui alitokea wapi jamani kwa nini sisi watanzania tumekumbwa na hili balaa la kuwa na huyu mtu hapa Tanzania. Nafikiri sasa tumuombe Mungu atusaidie maana hili janga sasa linakotupeleka siko
 
Huko ni kutafuta mahali kwa kujificha. akitajiwa atawafanya nini?? aliwahi kupelekewa orodha ndefu ya wauza madawa ya kulevya na mafisadi papa mbona mpaka leo hawajafanywa chochote??
 
Back
Top Bottom