Kikwete apingwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete apingwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 17, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,171
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFFFFF"]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Kikwete apingwa
  • Ashauriwa kudhibiti mfumo badala ya kutajana

  na Edson Kamukara
  Tanzania Daima

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete, kuwataka wananchi kuacha kulalamikia rushwa bila kuwataja majina waombaji na watoaji ili wachukuliwe hatua, baadhi ya wasomi wamepinga kauli yake wakidai si njia ya kumaliza tatizo hilo.

  Wakizungumza na Tanzania Daima jana, wasomi hao walisema kuwa Rais Kikwete kama alikuwa na dhamira ya dhati katika mapambano ya vita hivyo, alipaswa kueleza hatua zilizochukuliwa kwa orodha ya wala rushwa na wauza dawa za kulevya alizodai anazo.

  Akihitimisha kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru sanjari na kumbukumbu za miaka 13 ya kifo cha hatati Mwalimu Julius Nyerere juzi mkoani Shinyanga, Rais aliwataka wananchi kuwafichua wale wanaojihusisha na vitendo hivyo kwa vile wanaishi nao kwenye jamii.

  Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashir Ally, aliliambia gezeti hili kwa njia ya simu kuwa Rais Kikwete anapaswa kujiuliza ni kwa nini watu hawaitikii wito huo ambao unatolewa miaka nenda rudi.

  "Watu wanajua kuwa wakithubutu kutaja majina ya wahusika watakiona cha moto. Lakini Rais anataka kufanya jambo la ajabu maana angetupa mfano wa nchi hata moja iliyokomesha rushwa kwa watu kutajana majina," alisema.
  Bashir alifafanua kuwa hoja si kutaja majina ya watoa au wapokea rushwa bali kudhibiti mfumo wa rushwa usio wa haki, hivyo kushangaa kwamba Rais anawezaje kusema rushwa inamkera katika mazingira ya sasa.

  "Kama unaruhusu mfumo wa watu kununua kura, elimu, afya na huduma nyingine za msingi utasemaje unakerwa na rushwa. Anza kukerwa na mfumo wa matabaka ya wenyenacho na wasiyonacho, watoto wa viongozi kupenyezwa kimizengwe madarakani.

  "Ukidhibiti mfumo unaochochea rushwa hizo utakuwa umetokomeza rushwa. Lakini hilo limeshindikana kwa vile wauza elimu, dawa feki, dawa za kulevya na mengineyo ni marafiki wa watawala na hawaguswi," alisema.

  Msomi huyo alishauri kuwa kwa jinsi mfumo wa rushwa ilivyo sasa na kasi ndogo aliyoionyesha Rais Kikwete katika vita hiyo, ni bora kazi hiyo awaachie wengine wanaokuja wapambane.

  Naye mhadhiri mwingine wa chuo hicho wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Dk. Benson Bana, alisema kauli ya Rais Kikwete anaiona kama ya kisiasa kutokana na kazi aliyokuwa akiifanya kuwa ya siasa.

  Alisema kama hoja ni majina, listi ya watuhumiwa wa rushwa imekuwa ikitajwa na watu mbalimbali, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa watuhumiwa.

  "Kama Rais mwenyewe alishasema anayo orodha ya wauza dawa na wala rushwa, alipaswa kuwaeleza wananchi kwanza ameifanyiaje kazi, kisha ndipo awahamasishe kuwataja watuhumiwa wengine," alisema.

  Dk. Bana ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Taasisi ya Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (Redet), alisema kuwa jambo analoweza kulifanya Rais kwa sasa katika kupambana na vita hiyo ni kutoa motisha kwa wale watakaowafichua watuhumiwa.

  Alibainisha kuwa serikali inaweza kujipanga ikatoa motisha ya kati ya sh milioni tatu hadi tano kwa kila atakayetoa taarifa za wauza dawa za kulevya na wala rushwa ambazo zitathibitika kuwa za kweli.

  "Kwenye jamii hawa watu wanaoitwa whistleblower's (wapiga vilimbi) wapo, hivyo wakipewa motisha watawataja wauza dawa hizo na wala rushwa ilimradi tuhuma hizo zithibitike ni za kweli," alisema.  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Atajiwe majina mara ngapi? mh Slaa wa CDM aliyaanika wazi majina ya mafisadi JK akiwa mmoja wao-alichukua hatua gani?
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Anataka kugombanisha watu Kama alivyopandikiza chuki za kidini 2010
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,171
  Trophy Points: 280
  DHAIFU anazidi kudhihirisha UDHAIFU wake

   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  huyu hana lolote...ngoja nijiandae kuangalia debate hapa (obama vs romney)
   
 6. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mkuu si unajua mganga hajigangi?
   
 7. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  haya naanza kumtaja yeye alihongwa suti tano na dola milioni moja -wiki liks!
   
 8. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Aseme majina ya wauza madawa aliyafanyia kazi? Au ajayaona mpaka leo kwa sababu ya utembezi?
   
 9. t

  thatha JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Tatizo ushabiki unafanya watu wanashindwa hata kukumbuka mambo, wapo watu wengi tu waliochukuliwa hatua baada ya Rais kupewa majina ya wala rushwa hata leo baadhi ya kesi ziko mahakamani.
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mjaha sana tu humu JF. Jukwaa la utani, majungu, wivu na chuki. Hivi hakuna yeyote mwenye kuanzisha jukwaa lenye mweleko wa kisomi?
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Yeye mwenyewe anatoa rushwa ya vyeo.......na mifano ipo mimngi tu.......ukiwemo wa yule GAMBO
   
 12. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  wapi uliona kikwete akikanusha tuhuma za wiki leaks kuwa alihongwa suti tano na dola million moja walkati akiwa kwenye harakati za kugombea urais??aliyemhonga in turn si ndio kapewa The kilimanjaro hotel na kama sio kelele za kimataifa pia alikaibia kujenga hoteli kule serengeti kwenye njia ya wanyama??
   
 13. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hata wakitajwa anafanya nini? Mpiga domo tu huyo hana jipya!
   
 14. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,047
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu jamaa huwa ana nini kichwani mwake? Yeye mwnyewe ameshasikika mara kadhaa akisema hadharani kuwa serikali ina majina ya wala rushwa, wauza 'unga' n.k lakini mpaka leo hajawahi kuthubutu kumtaja hata mmoja wao.
  Leo hii yeye pamoja na cheo chake na nguvu zake zote za dola alizo nazo kashindwa kuthubutu kuwataja watu, anawarushia mzigo huo watu wa chini na dhaifu ambao hawana nguvu wala ulinzi wowote.
  Yeye huwa anajisikia kuongea ongea tu na inaonyesha kabisa kupitia kauli zake kuwa huwa hapwendi kabisa kujipa muda wa kutafakari mambo, pia si msikilizaji mzuri bali anapenda kuonge bila kujali kuwa kuna watu wanamsikiliza.
   
 15. Monyiaichi

  Monyiaichi JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 1,825
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  hivi huwa mwizi anaonewa wivu?
   
 16. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu Bak! Huyu hapa anakula bata download (1).jpg
   
 17. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  BAK huyu jamaa kashindikana!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sina hakika kama rais ana ujasiri wa kuchukua hatua kali dhidi ya mafisadi, wauza madawa ya kulevya, wala rushwa ambao ni watawala au wana nguvu za fedha na Wahujumu uchumi wengine. Ni hakika ana ujasiri wa kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya Walalahoi watakaojihusisha na vitendo viovu nilivyovitaja hapo juu. Lakini pia bila kujali nafasi au pesa yeyote anayegusa maslahi ya chama au maslahi binafsi ya watawala ni lazima ashughulikiwe iwe ni kwa kufuata sheria au kutofuata. Hii ni hatari.
   
 19. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hosea si ameishamtaja kuwa anapinga rushwa jukwaani!
   
 20. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #20
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  amechukua kwa ulimboka na mwangosi msimuonee rais wetu japo ni dhaifu.
   
Loading...