AAH Ukiwa kwenye payroll yake huoni baya. Sasa sisi wa kambo ndio kibano. JK Afanye mambo mawili tu nitamwona wa pekee moja atengue mikataba ya umeme pili ampeleke slaa mahakamani kwa kumchafua.[/QUOTE
Today they are crawling out of the woodwork. The Kikwete acolytes.
Na wewe ulimwagwa na nani? Mbowe au Josephine?
Umpe sifa kwan wewe nan? Sifa zako zina umuhim gan? Ukimsifia ataongezeka nn? Usipomsifia atapungukiwa nn? Wanaomsifia wanatosha sifa zako peleka kwa yule mshkaj wako!
Ndiyo anastahili sifa maana ni mpenda sifa mno. Ndio maana kila wakati anasubiri mpaka mwisho aone upepo unakwendaje ndipo anarukia jambo ili tu yeye ndiye apate sifa. Mwisho wa siku atahakikisha wengine wote wanachafuka na kubaki yeye tu msafi. Mimi namsifia tu kwa staili yake ya uongozi inayoiangamiza CCM.
Mwanzo nilikuchukulia juu juu, lkn sasa naona upuuzi wako haupaswi kupuuzwa. Msijitie ubingwa wa kumkosoa Nyerere, nakuhakikishia kuwa hata kama ni hali ngumu, basi ilitokana na hali halisi na sio uzembe. Hakukuwa na wasomi wala teknolojia tulionayo leo na exploitation ya resources zetu haikuwa ya kiasi hiki.
Huu unaoturudisha nyuma kwa sasa ni uzembe. Wasomi kibao lkn serikali legelege. Na hili la kusema enzi za Nyerere tulikuwa hatuna ruksa ya kusema nao ni upuuzi. Ulitaka useme nini?
Halafu sisi tulioko mjini story za Nyerere kuchoma Benki Kuu kwetu ni upuuzi
Baada ya Rais Kikwete kuunda upya mfumo wa ukaguzi wa mahesabu ya Serikali na baada ya kulazimisha ukaguzi huo uwe unafanywa kwa haraka zaidi, sio kama ilivyokuwa kwa uongozi wa kabla yake, na baada ya kufanya kila njia hesabu hizo ziwe zinajadiliwa kwa uwazi bungeni. Tunaona matunda yake.
Kikwete, unastahili kila sifa njema kwa kuwa mwenye kutoa na kufanya maamuzi kidemokrasia bila kuchukuwa hatua mkononi mwako (udikteta). Tunaona CAG ilivyofanya kazi, hakuna aliyetegemea kama itakuwa hivi.
Wapinzani, wameirukia hoja kama vile ni ubunifu wao, wanasahau kuwa wewe ndiye muasisi wa huu mfumo mpya na wewe ndiye uliyemteua Utoh.
Wanasahau pia kuwa wewe ndiye uliyeamuwa na kuanzisha mfumo wa hizi ripoti za mkaguzi mkuu zijadiliwe bungeni, hakuna aliyekuwa na moyo huo kabla yako. Mungu akuweke uendelee kuonesha njia.
Kwani uliposema tumsifie ni yeye anayefanya hesabu za CAG?
Sasa tusifie nini basi? Tusifie mfumo au matokeo ya jumla ya kazi? Kweli wewe kilaza. Kwa hiyo ukiwa unasahihisha mitihani, yule aliyepiga mistari vizuuuuri ktk karatasi la majibu ndio shujaa wako hata kama baada ya hiyo mistari hakuandika jibu lolote?! Duh, kweli kikwete ana washauri
Mijitu mingine ina mawazo mgando kweli, haya nieleze mifumo ya kikwete imesaidia nini katika kuzuia ubadhilifu wa mali za umma? mifumo mingi imewekwa kwa mashinikizo ya nchi wahisani baada ya kugundua pesa zao za misaada hawaoni matumizi yake kwenye maendeleo ya nchi. zamani kipindi cha nyerere mtu alikuwa akigundulika anamakosa anachukuliwa hatua kama unabisha kawaulize wakina mwinyi uone walichofanywa na mwalimu. leo unamsifia bosi wa magamba ya ruswa, ufisadi na unyonyaji unaakili kweli au unafikiri kwa kutumia ******. bila shaka ww utakuwa mke wa bosi wa magamba.
Baada ya Rais Kikwete kuunda upya mfumo wa ukaguzi wa mahesabu ya Serikali na baada ya kulazimisha ukaguzi huo uwe unafanywa kwa haraka zaidi, sio kama ilivyokuwa kwa uongozi wa kabla yake, na baada ya kufanya kila njia hesabu hizo ziwe zinajadiliwa kwa uwazi bungeni. Tunaona matunda yake.
Kikwete, unastahili kila sifa njema kwa kuwa mwenye kutoa na kufanya maamuzi kidemokrasia bila kuchukuwa hatua mkononi mwako (udikteta). Tunaona CAG ilivyofanya kazi, hakuna aliyetegemea kama itakuwa hivi.
Wapinzani, wameirukia hoja kama vile ni ubunifu wao, wanasahau kuwa wewe ndiye muasisi wa huu mfumo mpya na wewe ndiye uliyemteua Utoh.
Wanasahau pia kuwa wewe ndiye uliyeamuwa na kuanzisha mfumo wa hizi ripoti za mkaguzi mkuu zijadiliwe bungeni, hakuna aliyekuwa na moyo huo kabla yako. Mungu akuweke uendelee kuonesha njia.
Ukweli kwa hili suala anastahili pongezi. Amewapa meno na uwezo watu wa CAG kukagua kwa uwazi kila wizara na kuruhusu ripoti zao zisomwe na kujadiliwa bungeni kama ilivyokuwa kwenye kikao cha bunge lililopita. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.