zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,935
Baada ya Rais Kikwete kuunda upya mfumo wa ukaguzi wa mahesabu ya Serikali na baada ya kulazimisha ukaguzi huo uwe unafanywa kwa haraka zaidi, sio kama ilivyokuwa kwa uongozi wa kabla yake, na baada ya kufanya kila njia hesabu hizo ziwe zinajadiliwa kwa uwazi bungeni. Tunaona matunda yake.
Kikwete, unastahili kila sifa njema kwa kuwa mwenye kutoa na kufanya maamuzi kidemokrasia bila kuchukuwa hatua mkononi mwako (udikteta). Tunaona CAG ilivyofanya kazi, hakuna aliyetegemea kama itakuwa hivi.
Wapinzani, wameirukia hoja kama vile ni ubunifu wao, wanasahau kuwa wewe ndiye muasisi wa huu mfumo mpya na wewe ndiye uliyemteua Utoh.
Wanasahau pia kuwa wewe ndiye uliyeamuwa na kuanzisha mfumo wa hizi ripoti za mkaguzi mkuu zijadiliwe bungeni, hakuna aliyekuwa na moyo huo kabla yako. Mungu akuweke uendelee kuonesha njia.