Kikwete alisoma taarifa ya CAG?

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
Habari kuwa Kikwete anakubaliana na wabunge katika mjadala wa kuwawajibisha mawaziri kwa wizi wa pesa za wizara na idara mbalimabli haziwezi kupita bila kuuliza maswali ya msingi. Kwanza inabidi tujiulize, Kikwete aliisoma taarifa ya CAG? Swali hili ni muhimu kwa kuwa tunafahamu kuwa Kikwete amewahi kupewa mfano wa hundi wenye tarakimu ambazo haziendani na maneno yeye akatwaa hundi hiyo yenye makosa. Kama hakusoma hundi yenye ukurasa mmoja iweje taarifa kubwa ya CAG?

Pia ni rahisi kuamini kuwa taarifa ya Richmond ilijadiliwa bungeni bila yeye kuisoma. Ndiyo maana baada ya kujadiliwa na kumwondoa Lowasa alisikitika mbele ya wazee wa Dar kuwa ilikuwa ni ajali ya kisiasa.

Alienda mbali kuwa Chadema wanatuhumu wao, wanapeleleza wao na kuhukumu wao. Kama angeisoma ile taarifa kabla angeweza kumwokoa rafiki yake Lowasa. Halafu tunakumbuka sheria ya uchaguzi aliyoisaini ikiwa na makosa na baadaye kurekebishwa baada ya kusainiwa.


Kama Kikwete hakuweza kusona makosa kwenye ukurasa mmoja wa hundi na pia pia sheria ya gharama ya uchaguzi na taarifa ya Richmond kwa nini tuamini kuwa alisoma lundo la taarifa za CAG? Ni rahisi kuamini kuwa Kilwete hakusoma taarifa ya CAG na kwa hiyo hakujua kilichomo. Kama angejua angweza kuwaokoa mawaziri wake.

Lakini ilimpasa tu kukubaliana na wabunge kwa kuwa wananchi wengi walikasirishwa na wizi mkubwa unaofanywa na mawaziri. Kwa kuwa ni rahisi kuamini kuwa Kikwete hakuisoma ile taarifa ya CAG inayohitaji mkaguzi mwingine wa kuisoma, habari kuwa alipendezwa na mjadala ya wabunge ni ya kutiliwa mashaka makubwa

 
Rais yeye hasomi hiyo report maana anaweza asiielewe unless yeye ni professional accountant or financier...ile report anasomewa na kutafsiriwa na wasaidizi wake ambao wanaelewa kila kitu kilichoandikwa humo...

Unajua ufanisi mzuri wa Rais sio tu kwa decisions zake mwenyewe bali pia advisers wake pia wanachangia... Mi nahisi Mkuu wetu hana good advisers wale ambao wanaweza kukaa nae chini wakamweleza hali halisi ya nchi kiuchumi na kijamii inavyokwenda...
 
Siyo lazima aisome yeye, kuna walioisoma na kumpasha kilichomo. Hata cag mwenyewe anaweza kuwa chanzo kimojawapo cha habari juu ya kilichomo. Atasoma nyaraka ngapi? Kwa ma-rais makini huwa wanakuwa na watu makini wa kuwapasha nini kinajili katika sehemu kama mjengoni.
 
Kutoka moyoni mimi namwamini Kikwete kuliko Mkapa na Mwinyi, Hata mipango yake ya maendeleo ya taifa ni mizuri tu, Ila wateule wake wanamwangusha, Kama akina Msuya, Barongo, Chadiel Mgonja na wengineo walivyofanya enzi zile za mwalimu.

Kwa vile Kikwete ni very Democratic, anaogopa kuchukua maamuzi ya kidikteta kwa hiyo anashirikisha vyombo mbalimbali pamoja na wananchi ili wawazomee kwanza hao wezi, ili hatua stahiki zitakapochukuliwa kusiwepo na maneno kuwa wamepishana katika maslahi binafsi.
 
HAKUWA NA MUDA HUO,ALIKUWA ANAWAZA SAFARI YA BRAZILI KWA AKINA SHAKIRA NA MAXIMO.Kuna vitu vipo obvious na kwamba kila kitu rais asomewa ni hiari yake anaweza kusoma kwa nyakati fulani then akaita washauri wake wa brief lakini pia naye akiwa na tangible findings zake.Pia wakati briefing the CAG kwake anaweza kuona wapi kuna risk kubwa na CAG kumwabia ukweli wapi panahitaji maboresho zaidi.Tusimpambe hakusoma na kama alisoma hakuelewa na kama alielewa alipuuza kwa maslahi yake na pia aliamini ni UPEPO TU UTAPITA
 
...Kwa vile Kikwete ni very Democratic, anaogopa kuchukua maamuzi ya kidikteta.......

Very democratic?? inawezekana anashindwa kuchukua maamuzi kwa kuwa yeye ni DHAIFU kiutawala au amechagua RAFIKI zake au WASHIRIKA wake kwenye wizi na hawezi kuwafanya chochote kwa kuwa anafaidika moja kwa moja na matendo yao
 
Kikwete ni mvivu sana sidhani kama hata ana muda wa kujisomoe mwenyewe au hata kuwasomea wanae kitabu!!

Kwa jinsi alivyo, atakuwa alisomewa na kusimuliwa!!
 
mweeeee jamani tuwe wakweli...manamba yalivo magumu yale kwenye report ya CAG ataweza kusoma huyu mzee jamani au mnamtaka maneno
 
Ni mvivu na mtoro!!

Hebu pata picha ya mwanafunzi mvivu na mtoro shuleni, ndio utaelewa tuna rais wa namna gani!!
 
Nadhani ameisoma reportn nilimsikia kwenye Mei mosi akizungumzia mambo mengi ya kwenye report hiyo.
 
Kikwete ni mvivu sana sidhani kama hata ana muda wa kujisomoe mwenyewe au hata kuwasomea wanae kitabu!!

Kwa jinsi alivyo, atakuwa alisomewa na kusimuliwa!!

tena anasimuliwa huku anakula karanga au visheti na kahawa
 
Kwa kufuata maelezo uliyayasema hapo juu naweza kuamini kwamba hakuisoma au kama alisoma pia hakuielewa na mbali ya melezo yako hapo juu kuna uwezekano hajasoma kwa kutopata mda wa kukaa na kuisoma kwani yuko njiani mda wote kama siyo kudhuria misiba na kuzika ana ziara, ana safari za nje na za ndani.
 
Back
Top Bottom