Kikwete akae na Kagame wazungumze wayamalize...

Kikwete akae na Kagame wazungumze wayamalize...

Mkuu vitu vingine pima hata wewe kabla hujaleta jukwaani wakae wayamalize yepi.

Kunakosa gani ambalo jk kafanya mpaka akae na kagame kagame anauwa watu na kupora mali za congo halafu ukae nini.

Mkuu acha kabisa kuleta hoja za namna hiyo kagame mjinga sana hamna hoja hata moja itayofanya jk na kagame kukutana.
kagame mikono yake inanuka damu ni muuaji daraja la kwanza halafu leo ukae naye ba! Bwana wewe.
Simiyu Yetu Ametoa mapendekezo mazuri tu na ametumia uhuru wake kama mwana jamvi. Mara nyingine katika maisha ni vema kushuka (soma Waebrania 12:14 - "Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu ambao hakuna atakaye muona Bwana asipokuwa nao").

Ufike wakati JK aonyeshe maturity kwa kuitisha mkutano kati yake na Kagame ili wayamalize. Ni vizuri akawa wa kwanza kuinitiate peace talk; si kwamba anaenda kumuomba radhi Kagame kwani hajafanya kosa lolote. Mimi binafsi nafurahia ukimya wa JK katika hili; ukimya huu unampa yeye edge ktk ulimwengu wa diplomasia!
 
Back
Top Bottom