DRC: Wanajeshi walinda amani wa Tanzania wajeruhiwa katika mapigano na M23

Suzy Elias

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
1,067
6,192
M 23 imewajeruhi wanajeshi wetu huko Kivu ya Kaskazini.

Ifahamike m23 ni wahuni wanaoungwa mkono na Serikali ya Kigali na ikumbukwe wahuni hao m23 kipindi cha Kikwete tuliwatwanga hali iliyopelekea mgogoro mkubwa wa kidipromasia baina ya Serikali ya Kikwete na Serikali ya Kigali.

Sasa baada ya Serikali ya Samia kuingia madarakani wahuni hao wamerejea kwa nguvu pengine wakiamini Samia hawezi kuwafanya lolote.Tusikubali aslani!

Tuwashughulikie hao wahuni kabla hawajaleta mgogoro mkubwa ndani ya Kanda yetu na Serikali ya Kigali ionywe wazi iache kuwakumbatia hao chawa wao.

Tusimchekee Kagame kwa sababu si mtu mwema hata kidogo.

Mzee Kikwete hakuwa mjinga ku deal naye kibabe huyo mwana- hizaya mpenda vya bure.

=====

Wanajeshi walinda amani wa Tanzania wajeruhiwa katika mapigano na M23 DRC​

Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, FARDC, limetangaza kuwa wanajeshi watatu wa Tanzania wanaohudumu katika kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Mataifa MONUSCO wamejeruhiwa wakati wapiganaji wa M23 waliposhambulia ngome yao iliyopo Rutshuru.

MONUSCO imethibitisha kuwa wanajeshi wake watatu wamejeruhiwa na kupelekwa kutibiwa katika hospitali ya mjini Goma uliopo mashariki. Katika tangazo hilo jeshi la serikali ya Congo limesema mmoja wa wanajeshi hao amejeruhiwa vibaya.

MONUSCO inasema kuwa wanajeshi hao wamejeruhiwa katika shambulio lililofanyw na wapiganaji wa M23 katika ngome yao iliyopo ivukatika eneo la Shangi -Rutshuru.

Kundi la M23 linasema kuwa majeshi ya FARDC na na MONUSCO ndio waliofanyanya mashambulio kwanza dhidi yao katika ngome yao iliyopo katika eneo la Jomba Jumatatu.

Hii inakuja wakati mapigano yakiendelea kwa siku ya nne mfulurizo kati ya pande hizo yaliyoibuka baada ya mapigano hayo kusitishwa kwa muda wa wiki mmoja- mapigano yanayoendelea katika eneo la Rutshuru katika Kivu ya Kaskazini.

MONUSCO ilitangaza kuwa imo katika mapigano ikisaidia upande wa jeshi la Congo FARDC linalopigana na wapiganaji wa M23.

Tanzania ina wanajeshi zaidi ya 800 katika jeshi la MONUSCO kilichopo Mashariki mwa DRC.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatano usiku, jeshi la DRC, FARDC linaishutumu Rwanda kutuma kikosi chake maalum cha wanajeshi 500 kuwasaidia wapiganaji wa M23, likisema kuwa walikuja wakiwa wamevalia mavazi yenye rangi ya kijani kibichi na nyeusi.

Serikali ya Rwanda kwa imekuw aikikana mara kwa marakuwa inawasaidia M23, ikisisitiza kuwa tatizo lao liko ndani ya nchi yao wenyewe ya DRC.

Kikundi cha M23 Jumatano pia kilitoa tangazo kikiishutumu serikali kwa ‘’kuchagua njia ya vita’’, kwa vikosi vyake kushirikiana na wanajeshi wa MONUSCO na wapiganaji wa kundi linaloshutumiwa na Rwanda kufanya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 la FDLR kuwashambulia.

Tangazo hil la M23linasema: “Kuchagua vita kwa serikali ya Congo badala ya kuchagua mazungumzo ya amani, ni tatizo katika kurejesha amani katika mashariki mwa DRC”.

Wakati huo huo, jeshi la DRC- FARDC limetangaza kuwa maazimio yakikao cha wakuu wa majeshi kilichofanyika Goma ya kubuni kikosi maalumu cha kupigana na makundi ya wanamgambomashariki mwa Congo.

Yatawasilishwa mbele ya kikao cha wataalamu wa masuala ya kijeshi na wakuu majeshiitakayofanyika kati ya tarehe 15 na 19 mwezi huu mjini Nairobi Kenya, kabla ya kuidhinishwa na maraisi wa Kanda.

Chanzo: BBC
 
Sio rahisi, Rwanda wana intelligence madhubuti na iliyoenea sana East Africa. Kuingia kwenye vita ya moja kwa moja na Rwanda na kutarajia kuwapiga kirahisi ni kujidanganya. Usiongopewe na udogo wa eneo lao.
Hizo ni stori chief. Huyu jamaa wazungu wanamtumia ili aifanye congo isitulie wazid kuiba. Huyu jamaa anatakiwa apate funzo rasmi
 
Sio rahisi, Rwanda wana intelligence madhubuti na iliyoenea sana East Africa. Kuingia kwenye vita ya moja kwa moja na Rwanda na kutarajia kuwapiga kirahisi ni kujidanganya. Usiongopewe na udogo wa eneo lao.
Duh kaka unaishi shimoni? yaani Dula mbabe akampige Tyson! Rwanda ni kama Singida ipigane na Tanzania nzima!
Hujui nguvu za kijeshi za JWTZ

JWTZ sio jeshi la kitoto bado hawajaamua tu. Ukitaka kujua ubabe wa JWTZ Kagame atume waasi wake wapige mpakani na Tanzania halafu jamaa wakija waasi wakimbilie Rwanda!!

Uganda wanajua joto la JWTZ!
 
Back
Top Bottom