Kikwete aijaza jeuri Takukuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete aijaza jeuri Takukuru

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Prodigal Son, Feb 26, 2010.

 1. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  RAIS Jakaya Kikwete amesema watakaojihusisha au kutuhumiwa kwa vitendo vya rushwa kwenye mchakato wa uchaguzi ndani ya vyama vya siasa na wakati wa uchaguzi mkuu ujao, watachukuliwa hatua kali za kisheria.

  Alisema hayo jana jijini hapa, wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini(Takukuru) uliofanyika kwenye Chuo cha Benki Kuu.

  Rais ambaye alitoa hotuba yake akiwa amekaa, alisema asingependa kuona watu au kikundi cha watu, kiongozi au mtu binafsi akijihusisha na rushwa kwenye uchaguzi mkuu ujao ndani ya chama ama vyama vyenyewe.

  Aliitaka Takukuru kuhakikisha inawachukulia hatua watu hao ili kwenda sambamba na utekelezaji wa sheria ya uchaguzi ambayo muswada wake ulipitishwa bungeni hivi karibuni.

  “Ningependa kuona hakuna mtu anayejihusisha au kutuhumiwa kwa rushwa katika uchaguzi au wakati wa mchakato wa uchaguzi ndani ya vyama akaachwa bila kushughulikiwa.

  "Ninyi Takukuru ndio mnaotazamiwa kufanya kazi ya kukazia utekelezaji wa sheria hii mpya, na niwahakikishieni kuwa nitafanya kila linalowezekana ili muweze kufanikisha kazi ya kudhibiti rushwa katika uchaguzi nchini na msimwogope mtu,” alisema huku akishangiliwa.

  Alisema hivi sasa baadhi ya viongozi wa siasa ambao wengi wao ni wawakilishi wa wananchi, wameanza kupitapita majimboni kabla ya wakati muafaka kwa kisingizio cha kutoa misaada kwa wananchi na kuhoji walikuwa wapi.

  “Nimeambiwa wahongaji (viongozi) hivi sasa wanajipitisha kwa wananchi kwenye matawi wakitoa misaada huku wakijenga majengo, hivi hawa walikuwa wapi hadi wajitokeze wakati huu, hawa si wanataka kuwahadaa wananchi ili wachaguliwe?”

  Alihoji na kuongeza kuwa asingependa kuona mtu anayetaka kuingia kwenye uongozi akienda kwa wananchi kuwahadaa kwa fedha.

  Aliitaka Takukuru ianze mchakato wa kujipanga wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, ili waanze kudhibiti viongozi wanaotumia fedha, huku akisisitiza kuwa sheria iliyopitishwa hivi karibuni inaruhusu udhibiti wa rushwa kabla na wakati wa kura za maoni ndani ya vyama vya siasa na wakati wa uchaguzi.

  Alisema nia na madhumuni ni kuona kuwa wakati Serikali ya Awamu ya Nne itakapokuwa imemaliza awamu yake ya uongozi, iwe imejenga misingi imara ya utawala bora, demokrasia na maadili ya viongozi itakayojikita kwenye sheria za nchi, ili hatimaye uwepo utamaduni wa kudumu wa kuendesha shughuli za siasa bila mazingira ya rushwa.

  Alitumia fursa hiyo pia kuwaasa waandishi wa habari nchini wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi, ambapo alisema baadhi yao hujenga mazingira yanayowaaminisha watoa habari kuwa nao wanajihusisha kwenye vitendo vya rushwa.

  “Bahati mbaya sana waandishi wa habari nao wanaomba rushwa, mnakatisha tamaa jamii, ingawa ukiwasema hadharani waandishi wa habari wanakasirika sana, utakuta mwandishi anamwambia mtu unaona hii habari ni mbaya sasa niitoe?” Alisema.

  Aliihakikishia Taasisi hiyo misaada ya hali na mali ikiwa ni pamoja na vitendea kazi vya kisasa, lakini akaonya kuwa sharti watumishi wake wafanye kazi kwa umakini wa hali ya juu wakizingatia weledi wa taaluma zao.

  Aliitaka Takukuru kufanikisha azma ya kupambana na rushwa nchini, na kujihusisha kwa karibu sekta binafsi kwa maelezo kuwa wapo wakuu wa kampuni katika sekta hizo, wanaojihusisha na rushwa.

  Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, alisema katika kipindi cha Januari hadi Februari mwaka huu, Kurugenzi ya Uchunguzi iliongeza kasi ya kusimamia uchunguzi na uendeshaji mashitaka na kuvuka malengo kwa kuchunguza kesi kubwa tano kwa makao makuu na moja kwa kila mwezi kwa kila mkoa.

  Alisema Takukuru imeliokolea Taifa Sh 7,587,968,099.32 kupitia uchunguzi unaoendelea wa rushwa na ukaguzi wa fedha za miradi ya maendeleo uliofanyika kwenye halmashauri zote nchini.

  Mkutano huo wa siku tatu unaowakutanisha viongozi na wakuu wa idara wa taasisi hiyo wapatao 169 una lengo la kufanya tathmini ya utendaji wa mwaka mzima ili kuainisha changamoto zinazoikabili taasisi hiyo na kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana nayo.


  Chanzao: Habari LEO
   
 2. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  Sawa mzee,

  nahisi wapo kwa ajili ya ruswa ndogondogo TU, ma big fish hawaguswi,
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,776
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Kila siku wimbo huu huu sijui lini watatoa album!
   
 4. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,299
  Likes Received: 547
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono; JK naye anaharibu kuliko nilivyokuwa namtegemea. TAKUKURU ndio watu gani na KAMATI YA MWINYI ndio kitu gani? Kamati ya Mwinyi imeshika mafisadi na JK hajaipa meno, badala yake anakwenda kuwapa meno TAKUKURU...yani mwenye mbuyu hana meno na kibogoyo anakuwa tajiri wa mbuyu....tuna kaazi kweli na JK wetu.
   
 5. D

  Donrich Senior Member

  #5
  Feb 26, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kama Takukuru wameshindwa kudhibiti rushwa kwenye Richmond,EPA,Kiwira,to name just some,itakuwa vigumu sana kudhibiti rushwa katika uchaguzi ujao,labda kama watatumwa kuwalenga watu fulani fulani wasiotakiwa kwenye system...halafu Mzee naona amesahau kabisa kwamba magazeti na waandishi wa habari ndo waliomsaidia kuingia Magogoni,..labda wameshamjenga kisiasa vya kutosha so he dont need them anymore...lets wait and see...
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Feb 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  nimeipenda hii.. thanks!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Feb 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  sipendi tena sitaki taasisi ambayo imeundwa kisheria na ambayo inadaiwa iko huru inapewa maelekezo ya kufanya kana kwamba utendaji kazi wake unategemea hisani ya Rais!
   
 8. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 11,010
  Likes Received: 3,272
  Trophy Points: 280
  Aanguke sahihi sasa muswada uwe sheria. Au anasubiri kwanza agombee ndio iwe sheria?
   
 9. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Lakini jamani, tungoje tuone mchezo wa uchaguzi utaendaje, hapa kuna mawili, either hii tiasaidia kidogo kuingiza genuine people into the system ama ni tukio! Either way its a step, whether backwards or forwards remains to be seen. In my opinion, CCM is reacting to cleanse itself of the systematic loopholes that allow unscrupulous people tp flow into its ranks and thus get a strangle hold on the party which I think has alarmed the leadership into foretelling a KANU style death. CCM is acting to save itself but in the process we might get some genuine representation. Unajua watu wanalaumu bure saa nyingine, JF hakuna objectivity kabisaa saa nyingine ama kimakini zaidi karibia mara zote... Mama Kilango juzi kati kidogo apigwe mawe Same Mashariki, pamoja na programu zote zakimaendeleo alizowapelekea kisa alinfanya mkutano na hakutoa posho. Ndio watanzania wenyewe hawa... So all you people who think you have the moral high ground need to reassess... Demokrasia haiendani na "demos" ambayo iko nyuma kielimu (and I dont mean formal education alone) watu wanapenda kunhongwa.. ndio society yenyewe and since leaders mostly reflect society.. Our corrupt democracy reflects a corrupt society (nchi ya kitu kidogo na takrima) kwahiyo hapa Rais hajakosea ata kidogo... Acheni majungu yasiyo ya msingi.. Mimi nachukia sana kuona watu wanakosa uungwana.. Mnyonge mnyongeni lakini hakiyake mpeni.. Hongera kwa hili JK. Bora hao ma big fish waendelee kuongelea kwenye bahari ya fwedha za taifa hili kuliko nione wabunge, madiwani sijui mpaka wajumbe wanaogeleanao.. Kwakuwa wataishi watakufa wataisha... watabakia a new generation of leaders ambao hawajazoea utaratibu huo. SO its a step.. japokuwa safari ni ndefu na vita inaendelea.. Ukimdai mtu shilingi miatano akakupa 100, pokea alafu endelea kumdai.. JF= Uchambuzi - Objective thinking.

  Kinyambiss 2020
   
 10. W

  WildCard JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,494
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Muswada wenyewe umetoholewa kiasi kwamba hata atakapousaini hautakuwa na maana tena. Akina Chenge walihakikisha vinawekwa vipengere vya kijinga kiasi kwamba hata wa kumkamata kahonga ni kazi ngumu kwelikweli
   
 11. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 25,431
  Likes Received: 26,299
  Trophy Points: 280
  Alikuwa anazungumzia TAKUKURU ipi? hii ya Bwana Hosea? kama ndio yenyewe basi huo ni wimbo tuu.
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,831
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nina wasiwasi labda Takukuru ilianzishwa kwa ajili ya watu wadogo...
   
 13. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Alisema nia na madhumuni ni kuona kuwa wakati Serikali ya Awamu ya Nne itakapokuwa imemaliza awamu yake ya uongozi, iwe imejenga misingi imara ya utawala bora, demokrasia na maadili ya viongozi itakayojikita kwenye sheria za nchi, ili hatimaye uwepo utamaduni wa kudumu wa kuendesha shughuli za siasa bila mazingira ya rushwa.  ....fanya basi iwe kweli mheshimiwa. Dalili za kaya kuelekea kwenye ABYSS NA KUIFANYA NCHI IFANANE na zile ambazo wananchi wake wamegeuzwa kuwa MACHOKORAA zinazidi kujitokeza kila kukicha. Watu wamechoka na upambe wa maneno, tangu enzi zile za simulizi za maendeleo ya miaka mitano hadi enzi hizi za ILANI. Porojo tupu. Zamani zile ukwapuaji style yake siyo kama zama hizi. Mijitu mishirika inakwapua peupee na wengine tunaishia kusoma udaku wa sanaa pale Kisutu. Mara fyagio la chuma na sasa haya ya huko Mwanza. Mistari na Beti murua. Hivi yule Vithlani burungutu lake ni hadithi tu?

  At this stage, strict adherence to maintaining the rule of LAW AND ORDER, hayo hayo ya GOOD GOVERNANCE ndo suluhu na SIYO POROJO za hayo!
   
 14. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Ndio twajua huipendi nasi pia hatuipendi ila tatizo kama rais kamchagua mtu wake bila hata chombo kimoja cha juu au muhili mmjo kama bunge kupitisha ilo pendekezo la rais twategemea nini si maudhi ya kila siku na hao viongozi wa icho chombo si kujikweza kila siku kwa rais we chek tu jamaaa katoka huko majuuu moja kwa moja mwanza kaenda pale capri point chuo cha bank kufungua kikao mwasemaje sasa

   
 15. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  but in the process we might get some genuine representation.
  Hongera kwa hili JK. Bora hao ma big fish waendelee kuongelea kwenye bahari ya fwedha za taifa hili kuliko nione wabunge, madiwani sijui mpaka wajumbe wanaogeleanao
  Acheni majungu yasiyo ya msingi..
  Its pretty disappointing reading your perspective. It lead me to conclude that you mind is so cheap kiasi kwamba una amini kiulaiini. Chochote uambiwacho utaamini na utapondo atakaepinga eti sababu wewe ni shabiki.
  Genuine representation kutoka wapi? Hawa ministers ans MPs wa CCM? Come on. Wake up.Lowassa, Rostam, Masha, Msabaha, Karamagi, Sofia nk. watapitishwa, na hao utawaita genuine representatives?
  Eti hongera JK! Tumekua promised mangapi? Magapi yametimizwa? Kaka, inaonekana ulikua unaishi marekani na hujui what has been happening at home. Tuulize. Tutakupasha. This is sheer brind following. No objectivity what so ever.
  Majungu? Haya. Tuache time to tell!
   
 16. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Amesoma alama za nyakati na sasa anajua nini watu wanahitaji kusikikia ila warekebishe sheria ya uchaguzi iwe na flat level kwa watu wote
   
 17. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii habari si imeshatolewa hapa na Mongoiwe kwa kicha cha ''Kikwete azungumzia sheria ya uchaguzi'' AU?
   
 18. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #18
  Feb 26, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 680
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  Kwanza takukuru wanataki au wa waanze kumkamata yeye kikwete. kwa sababu alishaanza kitambo kupigiwa kampeni kuwa asipigwa na mtu yeyote kwa ccm. hata maandamano yalikwishafanyika. sasa takukuru wanasubiri nini? au ndo mambo ya msiba ni kwa jirani yako tu? kwako aaaah.
   
 19. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2010
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Wakuu,

  Tunaweza tusikubaliane na hii sheria kwa asilimia 100 lakini mimi naamini itasaidia hasa kwa vijana ambao hawana mapesa ya kumwaga au hawana nia ya kumwaga mapesa dakika za mwisho.

  Vurugu zilizoanza kutokea huko majimboni, ingelikuwa ni hatari tupu mwaka huu.

  Habari ambazo wengine tunazipata toka huko majimboni zinaonyesha wazi hii sheria imewatisha wengi wenye nia ya kugombea na hilo ni jambo jema. Takukuru nao wameshaanza kujipanga ipasavyo.

  Wacha tusubiri na kuona mwisho wake ila huenda ni habari njema kwa wengi hata kama sheria hii haitaweza kuwanasa wale samaki wakubwa ila huku chini kwa sisi magege kunaweza kuwa na fair playing ground ya aina fulani.

  Huenda hii sheria ikawa na maana kubwa kwenye kura za maoni za CCM kuliko kwenye uchaguzi mkuu.
   
 20. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu,

  Maadamu hayo maoni yametoka kwako, nimepata matumaini kuliko hata hizo porojo za Mhe Raisi. Nimekusikia mkuu, ngoja tusubiri tuone mwisho wake.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...