Kikwete Afaulu Mtihani Uliomshinda Pilato!

Kikwete Afaulu Mtihani Uliomshinda Pilato!

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,636
Reaction score
2,734
Nimemsifu Mkulu kwa maamuzi magumu aliyoyachukua kuwakinga 'wanyonge' dhidi ya uonevu wa utashi wa kisiasa. Maamuzi ya Mkulu yamenikumbusha mtihani kama huo aliokabiliwa nao Pilato. Pilato alikuwa na mamlaka ya kumwacha huru Yesu Kristo na alikuwa na nafasi hiyo moja tu. Lakini kutokana na kelele za Wayahudi Pilato alilazimika kumwachia huru Baraba alikyekuwa mhalifu wa hali ya juu.
Pilato alitoa hukumu yake kwa kusikiliza kelele za watu. Kikwete ametoa haki kwa kuangalia hali halisi. Iwapo angesikiliza kelele za wabunge, wanasiasa na wanaharakati wengine leo hii kuna wanyonge wangeonewa kwa kuonekana kuwa wanyang'anyi. Iwapo kweli IPTL ilistahili kulipwa pesa zake, kwa nini isilipwe? Iwapo watu wako na sympath kwa wamachinga pale wanaponyang'anywa haki zao, ni vema pia kuwa na thympathy kwa watu wengine hata kama wametuzidi kipato na uwezo wa mali.

Mtu unapokuwa rais, inabidi kutoa maamuzi kulingana na haki, na sio kwa ushabiki wa kisiasa. Nampongeza JK kwa kufaulu mtihani huu mgumu uliomshinda Pilato...
 
JK jana kasema ukweli kabisa. Watanzania tuache unafiki. Bado sijaona makosa ya Maswi na Muhongo
 
mkuu umeandika vema sana jk ni kiongozi makini sana kwenye hii dunia amefanya alichotakiwa kufanya kama kiongozi wa nchi hajasikiliza ushabiki wa kisiasa kama wengi walivyotaka.
 
mkuu umeandika vema sana jk ni kiongozi makini sana kwenye hii dunia amefanya alichotakiwa kufanya kama kiongozi wa nchi hajasikiliza ushabiki wa kisiasa kama wengi walivyotaka.
Tena umakini wa JK hakuna kichwa hata kimoja ndani ya UKAWA
 
JK jana kasema ukweli kabisa. Watanzania tuache unafiki. Bado sijaona makosa ya Maswi na Muhongo

kabisa kabisa kosa la muhongo na maswi hatulioni mahala lilipo ni chuki za mafisadi tu ndiyo zilikuwa zinashinikiza.
 
upeo wa jk siyo wa kutiliwa shaka anatenda haki sana kwenye jamii hata kwa watu mmoja mmoja hajui kumuonea mtu.
 
Nimemsifu Mkulu kwa maamuzi magumu aliyoyachukua kuwakinga 'wanyonge' dhidi ya uonevu wa utashi wa kisiasa. Maamuzi ya Mkulu yamenikumbusha mtihani kama huo aliokabiliwa nao Pilato. Pilato alikuwa na mamlaka ya kumwacha huru Yesu Kristo na alikuwa na nafasi hiyo moja tu. Lakini kutokana na kelele za Wayahudi Pilato alilazimika kumwachia huru Baraba alikyekuwa mhalifu wa hali ya juu.
Pilato alitoa hukumu yake kwa kusikiliza kelele za watu. Kikwete ametoa haki kwa kuangalia hali halisi. Iwapo angesikiliza kelele za wabunge, wanasiasa na wanaharakati wengine leo hii kuna wanyonge wangeonewa kwa kuonekana kuwa wanyang'anyi. Iwapo kweli IPTL ilistahili kulipwa pesa zake, kwa nini isilipwe? Iwapo watu wako na sympath kwa wamachinga pale wanaponyang'anywa haki zao, ni vema pia kuwa na thympathy kwa watu wengine hata kama wametuzidi kipato na uwezo wa mali.

Mtu unapokuwa rais, inabidi kutoa maamuzi kulingana na haki, na sio kwa ushabiki wa kisiasa. Nampongeza JK kwa kufaulu mtihani huu mgumu uliomshinda Pilato...

Tuchukulie kwamba tunakubaliana na wewe kwamba IPTL wamelipwa pesa yao.

Sasa unamchunguza Muhongo na Maswi kwa kipi tena

Na werema arudishwe kazini sasa.

Watanzania bana....mambo ya msingi sasa tumeacha tunashangilia tu Tibaijuka
 
Hivyo ndivyo kiongozi anatakiwa kuwa.Hongera sana Rais. Kitu nilichojifunza kupitia sakata hili nimegundua pia watanzania wengi pia hawajui elimu ya kodi na ndiyo kitu ambacho wabunge wengi walikuwa wanajichanganya.Kwa mfano nikimlipa mtu fedha baada ya kupokea huduma fulani malipo huambatana na VAT yeye ndiye anayetakiwa kuwalipa TRA na kama hatalipa basi TRA wao ndio wanatakiwa kumuwajibisha aliyelipwa kwa kukwepa kodi.Pia kwa sheria za nchi hii unavyomlipa mtu kwa kupata huduma fulani huwa hatutakiwi kuikata VAT kabisa au kuwataarifu TRA kwamba nimelipa VAT kwa njia ya simu.Kama ni kampuni husika huhitajika ku file VAT Return kama kawaida.Pia kama kampuni haijasajiliwa kwenye VAT basi huo ni uzembe wa TRA kwa kuruhusu watu kufanya biashara kubwa bila kuwa Registered wakati sheria inasema kama mfanyabiashara atakuwa na turnover kuanzia 40 milioni kwa mwaka na awe anauza bidhaa zenye VAT basi anastahili kusajiliwa.

Kumbuka:Kama wewe ni mwana siasa lakini unataka kupata umaarufu kwa kukwamisha wanasiasa wenzako kwa uongo basi hufai kuwa kiongozi kwa maana wewe ni mdhambi, Pia kama wewe ni tajiri halafu utajiri wako unachangia wanyonge kuwa wanyonge zaidi na makampuni mengine kuwa dhaifu basi wewe ni mdhambi na hautufai.
 
Ponsio Pilato hukuwa na kigugumizi, aliuliza swali makusudi kwa wayahudi nimwachie nani sabato YESU kristo Mnazareti au Baraba? Alichokuwa anaamini Pilato ni kwamba wayahudi wataamua aachiwe Yesu kwani BARABA alikuwa mnyanga`anyi alikuwa anawasumbua sana kwenye jamii kama vile sisi tunavyowachoma vibaka,kwa hiyo hiyo ilikuwa trick ya wazi kabisa ya kumwokoa yesu. Kikwete jana hakufanya hivyo hakuuliza mtu, watu walikuwa wanangojea atoe maamuzi na siyo mambo yake ya kijing`atang`ta.

Mtoa mada mfano wako ni tofauti Pilato alishindwa kumwachia Yesu moja kwa moja kwa maana wayahudi walisema akimwachia Yesu atakuwa siyo rafiki wa kAISARI, maana yake Kaisari angemfukuza kazi Pilato na yeye Pilato cheo kile alikuwa anakitaka. Sasa Kikwete alikuwa na kigugumizi cha nini kumfukuza Tibaijuka kwani yeye alikuwa anaogopa kufukuzwa kazi na nani, Pilato aliogopa kufukuzwa kazi na Kaisari . je! huyo Kikwete wako alikuwa anaogopa kufukuzwa kazi na nani? Kama angemlinda Tibaijuka?

Mambo ya bibilia tuachieni sisi wa roma
 
kabisa kabisa kosa la muhongo na maswi hatulioni mahala lilipo ni chuki za mafisadi tu ndiyo zilikuwa zinashinikiza.

Naomba nikuulize mkuu gsu ....Maazimio ya Bunge yalifanyika under the Premise kwamba zile fedha ni za Umma.

Kikwete amethibitisha sio za Umma.

Sasa;

  1. Kwa nini anamchunguza Muhongo? Kwa nini ameagiza Maswi ashughulikiwe?
  2. Kwa nini amekubali Werema Kujiuzulu?
  3. Kwa nini asiwaombe radhi stanbic bank kwa damage waliyoipata?
  4. Kwa nini apoteze fedha zingine kwa ajili ya kutekeleza maazimio ya bunge ambayo yalikua na basis kwamba fedha ni za umma?
 
Last edited by a moderator:
JK jana kasema ukweli kabisa. Watanzania tuache unafiki. Bado sijaona makosa ya Maswi na Muhongo

Ni kweli kabisa mkuu katika nchi hii kama ukipata viongozi kama Maswi na Muhongo ambao wanazuia watu kufanya uzembe au wakemea maovu basi lazima watokee watu wenye nia mbaya na nchi yetu wakitaka kuwakatisha tamaa.Ukiangalia taarifa ya CAG yote huoni sehemu ya kuwahukumu hawa watu, kama Maswi kaomba ushauri kwa mwanasheria Mkuu wa serikali mara nyingi kabla ya kufanya maamuzi na ndiyo taratibu za kazi zinavyoelezea, walitaka afanye nini cha ziada ili muone mtu anafanya kazi kwa kujituma?Unajua siku zote mti wenye matunda ndio hupigwa mawe!Kwenye ukweli jamani kuweni wakweli bila kujali chuki binafsi.
 
Naomba nikuulize mkuu gsu ....Maazimio ya Bunge yalifanyika under the Premise kwamba zile fedha ni za Umma.

Kikwete amethibitisha sio za Umma.

Sasa;

  1. Kwa nini anamchunguza Muhongo? Kwa nini ameagiza Maswi ashughulikiwe?
  2. Kwa nini amekubali Werema Kujiuzulu?
  3. Kwa nini asiwaombe radhi stanbic bank kwa damage waliyoipata?
  4. Kwa nini apoteze fedha zingine kwa ajili ya kutekeleza maazimio ya bunge ambayo yalikua na basis kwamba fedha ni za umma?
wewe ni mburura kwelikweli,maadili ya utumishi wa umma , mtumishi wa umma apokee siyo zaidi 50000 kama zawadi na haijalishi umepokea kutoka pesa za Umma au la?
 
Last edited by a moderator:
JK jana kasema ukweli kabisa. Watanzania tuache unafiki. Bado sijaona makosa ya Maswi na Muhongo

Wewe hujaona makosa yeye kasema ana wachunguza na ameagiza wahusika wawachunguze

Ameshindwa kueleza ni kwa nini Pesa zitoke na huku anasema mgogoro haujawa resolved
 
Back
Top Bottom