Nimemsifu Mkulu kwa maamuzi magumu aliyoyachukua kuwakinga 'wanyonge' dhidi ya uonevu wa utashi wa kisiasa. Maamuzi ya Mkulu yamenikumbusha mtihani kama huo aliokabiliwa nao Pilato. Pilato alikuwa na mamlaka ya kumwacha huru Yesu Kristo na alikuwa na nafasi hiyo moja tu. Lakini kutokana na kelele za Wayahudi Pilato alilazimika kumwachia huru Baraba alikyekuwa mhalifu wa hali ya juu.
Pilato alitoa hukumu yake kwa kusikiliza kelele za watu. Kikwete ametoa haki kwa kuangalia hali halisi. Iwapo angesikiliza kelele za wabunge, wanasiasa na wanaharakati wengine leo hii kuna wanyonge wangeonewa kwa kuonekana kuwa wanyang'anyi. Iwapo kweli IPTL ilistahili kulipwa pesa zake, kwa nini isilipwe? Iwapo watu wako na sympath kwa wamachinga pale wanaponyang'anywa haki zao, ni vema pia kuwa na thympathy kwa watu wengine hata kama wametuzidi kipato na uwezo wa mali.
Mtu unapokuwa rais, inabidi kutoa maamuzi kulingana na haki, na sio kwa ushabiki wa kisiasa. Nampongeza JK kwa kufaulu mtihani huu mgumu uliomshinda Pilato...
[/B] [/B]JK jana kasema ukweli kabisa. Watanzania tuache unafiki. Bado sijaona makosa ya Maswi na Muhongo
Mitanzania sisi mipumbavu! Hivi kila kitu lazima kupiga dessa? Maneno mengi uliyoyatumia yamesemwa Jana na Prof. Kitila Mkumbo wakati akihojiwa na bi. Sulmu Kassimu kwenye dira ya dunia! Tafuta maneno yako! Pamoja na kupiga simbi bado umetoa hoja ya kijinga sana!
Naomba nikuulize mkuu gsu ....Maazimio ya Bunge yalifanyika under the Premise kwamba zile fedha ni za Umma.
Kikwete amethibitisha sio za Umma.
Sasa;
- Kwa nini anamchunguza Muhongo? Kwa nini ameagiza Maswi ashughulikiwe?
- Kwa nini amekubali Werema Kujiuzulu?
- Kwa nini asiwaombe radhi stanbic bank kwa damage waliyoipata?
- Kwa nini apoteze fedha zingine kwa ajili ya kutekeleza maazimio ya bunge ambayo yalikua na basis kwamba fedha ni za umma?
Unatoa mifano haifanani Yesu ninani ktk mfano wako
Ni kweli kabisa mkuu katika nchi hii kama ukipata viongozi kama Maswi na Muhongo ambao wanazuia watu kufanya uzembe au wakemea maovu basi lazima watokee watu wenye nia mbaya na nchi yetu wakitaka kuwakatisha tamaa.Ukiangalia taarifa ya CAG yote huoni sehemu ya kuwahukumu hawa watu, kama Maswi kaomba ushauri kwa mwanasheria Mkuu wa serikali mara nyingi kabla ya kufanya maamuzi na ndiyo taratibu za kazi zinavyoelezea, walitaka afanye nini cha ziada ili muone mtu anafanya kazi kwa kujituma?Unajua siku zote mti wenye matunda ndio hupigwa mawe!Kwenye ukweli jamani kuweni wakweli bila kujali chuki binafsi.
Akiondoka Prof Muhongo na Katibu Maswe wizara inarudi tena kwa madalali wa ndani wa kisiasa na wafanyabiashara wazawa.Tukikupima akili hatupati hata 2 mM (Two microMuhongo)!
Mbona hamjiulizi zimelipwa ngapi kwa IPTL kabla ya account hii ya escrow haijafunguliwa? Ilikuwa ni kazi ya Maswe Kukokotoa au TANESCO inao wataalam wake?Kama kweli Maswi ni mchapaka kazi na mzalendo kama unavyotaka tuamini. Kwanini alishindwa kukokotoa hesabu upya ili kufahamu pesa ya TANESCO ni kiasi gani na pesa ya IPTL ni kiasia gani kama mahakama ilivyo amua?
Na badala yake wakaamua kulipa pesa yote ya Tegeta Escrow kwa IPTL, bila kukokotoa hesabu upya kama walivyoamuliwa na mahakama ya ICSD?
Kama kweli huyo Maswi hakuwa na masilahi binafsi ya hiyo pesa, kwanini hakumkingia kifua lawyer wa Tanesco aliyefanya due deligency na kutoa report kwamba kampuni ya PAP ni ya kitapeli, matokeo yake wakamfukuza kazi huyo lawyer.
Maswi na Muhongo watanusurika na hili sakata ka Escrow kwasababu moja tu, mtu anayetakiwa kuwawajibisha naye ni muhusika mkuu wa sakata la Escrow
Tafakari, chukua hatua
Mama Tibaijuka kaondolewa kwa kutozingatia ITIFAKI tu. Rais alishasema atalitolea maelezo suala hili. Sasa huyu mama aliitisha press conference ya nini?kwa hiyo anna pekee ndo alikosa kwenye hili??? anna si ni mwanamke iwapo Ruge ni bwana yake mlitaka aseme wazi hakuna tena haki ya privacy??
Tena umakini wa JK hakuna kichwa hata kimoja ndani ya UKAWA
Ponsio Pilato hukuwa na kigugumizi, aliuliza swali makusudi kwa wayahudi nimwachie nani sabato YESU kristo Mnazareti au Baraba? Alichokuwa anaamini Pilato ni kwamba wayahudi wataamua aachiwe Yesu kwani BARABA alikuwa mnyanga`anyi alikuwa anawasumbua sana kwenye jamii kama vile sisi tunavyowachoma vibaka,kwa hiyo hiyo ilikuwa trick ya wazi kabisa ya kumwokoa yesu. Kikwete jana hakufanya hivyo hakuuliza mtu, watu walikuwa wanangojea atoe maamuzi na siyo mambo yake ya kijing`atang`ta.
Mtoa mada mfano wako ni tofauti Pilato alishindwa kumwachia Yesu moja kwa moja kwa maana wayahudi walisema akimwachia Yesu atakuwa siyo rafiki wa kAISARI, maana yake Kaisari angemfukuza kazi Pilato na yeye Pilato cheo kile alikuwa anakitaka. Sasa Kikwete alikuwa na kigugumizi cha nini kumfukuza Tibaijuka kwani yeye alikuwa anaogopa kufukuzwa kazi na nani, Pilato aliogopa kufukuzwa kazi na Kaisari . je! huyo Kikwete wako alikuwa anaogopa kufukuzwa kazi na nani? Kama angemlinda Tibaijuka?
Mambo ya bibilia tuachieni sisi wa roma
Ninampongeza sana Rais wangu kwa kuamua kufanya maamuzi kwa kufuata taratibu, ikumbukwe kuna siku alishawahi kusema wakati anahojiwa na radio sauti ya amerika, kuwa katika vitu vinavyomuuma sana, ni pale alipofanya maamuzi juu ya mtu fulani halafu hapo baadae akagundua kuwa uamuzi alioufanya ulikuwa ni wa kumuyonea mtu kwa sababu jambo(Tuhuma) lilokuwa limemfanya afanye maamuzi halikuwa la kweli. lakini pia ikumbukwe, utaratibu wa kuwafanya wabunge wawe ni wachunguzi wa tuhuma mbalimbali, utaratibu huo sio sahihi, taaluma ya uchunguzi inasomewa, sasa mtu amepitishwa na jimbo lake huko atokako kwa sababu tu ni maarufu huko, au alikuwa daktari, anafika bungeni anapewa kamati ya kuchunguza tuhuma za wizi wapesa. hana taalumaa ya uchunguzi na pia hana taaluma ya uhasibu na kibaya zaidi huenda anajua nikimkomoa huyu, basi akiachishwa nafasi yake huenda nikapewa mimi na kuwa waziri wa Afya. Hebu tuwaache wabunge waisimamie serikali na waache kufanya kazi za mhimili mwingine za kuchunguza mambo ya wizi.
Ipo siku utamtambua tu yesu kuwa ni nani kwenye hii dunia jifanye umechanyikiwa tu.Unatoa mifano haifanani Yesu ninani ktk mfano wako