Naye Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, alisema si rahisi kuwarudisha mawaziri darasani ila wanachopaswa kufanya ni kubadili fikra, ili kwenda na wakati na kuachana na tabia za urasimu.
Rais Kikwete alisema ujamaa ndio umesababisha watumishi wengi wa serikali kuona ubepari kama uadui hivyo hata mtu anayetaka kuja kuwekeza anasumbuliwa hadi anaamua kuondoka.
" Kweli ujamaa ndio umetufanya tuone ubepari ni dhambi hivyo mwekezaji akija anaangaliwa kama vile mwizi, na hilo linafanya wawekezaji wengine kuamua kwenda kutafuta sehemu zingine za kuwekeza, sisi serikalini tumeligundua hilo na ndo maana tumeanza mkakati wa kuajiri vijana wengi zaidi wenye fikra mpya katika nafasi mbalimbali," alisema Rais Kikwete.
"Bado kuna tatizo la watumishi kubadili fikra ili watekeleze maono yetu, hilo tunapambana nalo kweli kweli ili twende na dunia ya sasa, ila kuwarudisha darasani hapana," alisema Rais Kikwete na kusababisha kicheko.
..kwa kweli inachanganya mwenyekiti wa chama kinachofuata itikadi ya UJAMAA na KuJITEGEMEA anapotoa kauli kama hizi.
..hivi inawezekana tukawa na chama tawala cha kijamaa lakini serikali yake ikawa ya kibepari?
Azimio Jipya said:Mkuu nitafurahia kama ungegusia source! Aliyasemea wapi haya maeneno!!
AridityIndex said:Na kwa taarifa yenu kwa kila Mtanzania aliyefanikiwa kiuchumi kupitia private sector atakubaliana na haya isipokuwa wale mnaonufakaika na system zisizo wazi na ukiritimba, maana wao akili yao inaishia kuomba mgao eti kwa vile mtu amekuja kuchukua cheque yake.
hapa kikwete kwa mara ya kwanza kaongea point yenye akili sana. Wachangiaji wa mwanzo hili lililosemwa na kikwete lina ukweli midingi maofisini humo wakiritimba hata kwa wawekezaji wa ndani yaani private sector na wao ni kama paka na panya. Sijuwi kitaisha lini hiki kizaji cha mwalimu nyerere?.
Na kwa taarifa yenu kwa kila mtanzania aliyefanikiwa kiuchumi kupitia private sector atakubaliana na haya isipokuwa wale mnaonufakaika na system zisizo wazi na ukiritimba, maana wao akili yao inaishia kuomba mgao eti kwa vile mtu amekuja kuchukua cheque yake.
Waberoya said:Kikwete has a point! Lakini amesema kama vile siyo Rais! amesema kama vile anapiga porojo
Rais mzuri ni yule anayejua tatizo na kulitatua tatizo, Mkapa alijua watanzania wavivu na akaleta uchapa kazi kwa kupunguza fedha kwenye mzunguko.
Watanzania hawataki kuhuburiwa matatizo yao! wanataka solution , you are the best if not only candidate to solve our problems.
Issues za ujamaa na matatizo yake zimejadiliwa sana humu, ni debatable, ni controversy, kuna nchi nyingi zimeendelea kwa ujamaa, na ziko nchi zenye ubepari leo hii wanatamani ujamaa!
Kikwete pole, haukujua ikulu kuna nini na unatakiwa ufanye nini umebaki kuwa comedian like any other comedian, umebaki kulalamika kama wanaharakati!
Heshima yako ni kujiuzulu tu, wenye akili watakusifia , kwenda na zigo la magogoni mpaka 2015 you may die on the way or you may end up crazy!
Kiranga,Maandishi hayaonyeshi kwamba hii ni direct quote (hakuna quotation marks)
Na zaidi ya hapo hakuna source.
Vitu viwili hivi vingeongeza credibility ya habari.
What made you say that?....got any uthibitisho?Waberoya,
..wakati wa awamu ya pili ya Mzee Mwinyi kulianza kujingeka utamaduni na mazingira ambayo hayakuwa conducive kwa wafanyabiashara waaminifu kufanya shughuli zao.
..tatizo alilolikuta Mkapa ni tabia ya kupenda ujanja-ujanja, biashara za kitapeli, na ukwepaji kodi.
..alichofanya Mkapa ni kuanza kusimamia ukusanyaji kodi, na kuchukua hatua za kudhibiti mfumuko wa bei na mzunguko wa fedha.
..morale na maadili ya watumishi wa umma iko chini, sasa JK anaanza kulaumu Ujamaa. mimi nimeishi wakati wa Ujamaa na watumishi walikuwa wanafanya kazi kwa kujituma kwelikweli. mambo yalianza kuharibika baada ya hali ya uchumi kuwa ngumu na wafanyakazi kuanza kushindwa kumudu maisha.
Moja ya tatizo ni hili: leo sikukuu, kesho hakuna kazi, Jumapili hakuna kazi, Jumatatu ni siku ya mapumziko, Jumanne nayo ni siku ya mapumziko. Sasa niambieni, kwa hali tuliyonayo sisi tunaweza kweli kumudu kutokufanya kazi siku zote hizi?
Kwa hiyo hapo utaona kwamba moja ya matatizo yetu ni kuendekeza starehe na uvivu.
Mkuu una uhakika na ilo la Siku ya Jumanne kuwa ni siku ya mapumziko?Moja ya tatizo ni hili: leo sikukuu, kesho hakuna kazi, Jumapili hakuna kazi, Jumatatu ni siku ya mapumziko, Jumanne nayo ni siku ya mapumziko. Sasa niambieni, kwa hali tuliyonayo sisi tunaweza kweli kumudu kutokufanya kazi siku zote hizi?
Kwa hiyo hapo utaona kwamba moja ya matatizo yetu ni kuendekeza starehe na uvivu.