Kikwete aambiwa abebe mizigo yake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete aambiwa abebe mizigo yake!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Japhari Shabani (RIP), Aug 22, 2011.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Aug 22, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  • WABUNGE WADAI MSEKWA NI GAMBA JINGINE CCM

  na Salehe Mohamed, Dodoma

  MAKADA na wabunge kadhaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanatilia shaka uwezo na dhamira za baadhi ya mawaziri katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, na sasa wamemtaka awaondoe kama anataka kunusuru chama na serikali yake.

  Wanasema Rais Kikwete asipofanya mabadiliko sasa, hataungwa mkono na wananchi, wakiwamo baadhi ya wana CCM wenye nguvu na ushawishi wanaoitakia mema nchi hii.

  Makada hao wanakiri kwamba serikali imepoteza heshima mbele ya jamii kutokana na kukithiri kwa vitendo vya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na kukosa uamuzi mgumu kwenye ufumbuzi wa matatizo ya wananchi, likiwamo tatizo la mgawo wa umeme.

  Wanadai sasa hivi Bunge ndilo limebaki kuwa mkombozi wao maana linajadili yale yaliyoishinda serikali, na hata kuiagiza ifanye na kurekebisha makosa ya wazi.

  Na baada ya wabunge wa CCM kuona serikali imelala usingizi, na chama kinachoongozwa na mwenyekiti ambaye ndiye rais, kinashabikia udhaifu a serikali, wameshtuka na kuanza kuishambulia serikali, hasa baada ya kuona wabunge wa upinzani wanatoa hoja zinazogusa maisha ya wananchi wa kawaida.

  Miongoni mwa wabunge ambao wameamua kuungana na wapinzani katika kutetea masilahi ya wananchi ni Deo Filikunjombe (Ludewa), Beatrice Shelukindo (Kilindi), Christopher ole Sendeka (Simanjiro), Dk. Khamis Kigwangalah (Nzega) na Kaika Telele (Ngorongoro).

  Wabunge hawa, kwa nyakati tofauti, wamewashambulia viongozi wao kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo na hivyo kusababisha matatizo kwa wananchi.

  Hata hivyo, duru za siasa zinadai kwamba inawezekana mashambulizi ya wabunge hawa wa CCM ni kiinimacho cha kudhoofisha nguvu ya wapinzani, kama ilivyokuwa kwa waliojiita wapambanaji wa ufisadi, ambao miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu uliopita walitumika kupoka ajenda ya ufisadi kutoka kwa wapinzani, hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili CCM iweze kuaminiwa tena na umma.

  Telele na Sendeka walimshambulia Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, kwa kutoa vibali vya ujenzi wa hoteli yenye hadhi ya nyota tano katika hifadhi ya Bonde la Ngorongoro ambalo haliruhusiwi kwa shughuli za kibinadamu.

  Shelukindo naye alimshambulia Waziri wa Maliasili na Utalii kwa kumteua Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa, katika kamati ya kusimamia ugawaji wa vitalu vya uwindaji wakati hana sifa zinazostahili.

  Mbunge huyo pia katika vikao vya wabunge wa chama hicho, alimshambulia Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kwa kufanya ukabila kwenye Idara ya Wanyamapori.

  Mashambulizi ya wabunge hawa yameonekana kuwashtua baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao mara kadhaa wamekuwa wakilinda udhaifu wa watendaji wa chama na serikali kwa lengo la kuogopa kuharibu taswira ya chama.

  Kutajwa kwa Msekwa katika uuzaji wa maeneo akitumia jina la Rais Jakaya Kikwete kumezua maswali miongoni mwa makada wa chama hicho juu ya uhalali wa dhana ya kujivua gamba inayopigiwa chapuo hivi sasa.

  Hoja inayojengwa na makada hao ni kuwa kama Msekwa anashiriki katika vitendo vya ufisadi atakuwa na mamlaka gani ya kuwahoji makada wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo hivyo?

  Hata hivyo, baadhi ya wabunge waliozungumza na gazeti hili wameweka wazi kuwa kulinda maovu hayo ni kukiua chama chao na wabunge wake ambao hivi sasa wameamua kutetea masilahi ya majimbo yao bila woga.

  Baadhi yao wamebainisha kuwa kama serikali itashindwa kuwasikiliza, wao wataachana nayo, na wataendelea kutetea majimbo yao.

  "Hivi sasa kilichopo ni kutetea wananchi wetu kwenye majimbo tuliyotokea, tukifanya mchezo wananchi watapoteza imani kwetu kama walivyofanya kwenye chama," alisema mbunge mmoja kwa sharti la kutotajwa jina.

  Wachambuzi wa masuala ya siasa wanabainisha kuwa miongoni mwa mambo yanayoifanya CCM kupoteza mvuto kwa jamii ni kupanda kwa mafuta, tuhuma za ufisadi, maisha magumu na mgawo wa umeme.

  Mmoja wa viongozi serikalini amelidokeza Tanzania Daima Jumapili kuwa baadhi ya mawaziri wanashindwa kuwajibika kikamilifu kiasi cha kushindwa kuwawajibisha watendaji wasiotekeleza majukumu yao.

  "Tunaisubiri NEC (Halmashauri Kuu ya CCM) itakayokutana mwezi ujao kama itafanya maamuzi ya kukinusuru chama chetu. Isiporekebisha mambo hali itakuwa mbaya zaidi. Si umeona bungeni mambo yanavyotuwia magumu?" alisema.

  Kada mmoja wa siku nyingi kutoka Kanda ya Ziwa alisema, "Kama rais hataki kutuondolea hii mizigo yake, tunaweza kumlazimisha na yeye akafunga virago akaondoka nayo."

  Alidai kwamba ingawa JK katika siku za hivi karibuni ameleta dhana ya kujivua gamba kama njia ya kukihalalisha chama mbele ya umma, kitendo cha rais kushindwa kuchukua hatua mapema dhidi ya wale anaowadhania kuwa ni magamba kimemfanya aonekane kiongozi dhaifu.

  Alisema hata utekelezaji wa dhana hiyo ukifanyika vibaya unaweza kumdhuru rais mwenyewe kwa sababu amewapa watu wengi muda wa kufanya tafakuri ya kutosha, na wamegundua kwamba magamba ndani ya CCM ni zaidi ya hao ambao wamekuwa wakitajwa.

  Alienda mbali hata kudai kwamba uchambuzi wa kina ukifanywa, hata mwenyekiti mwenyewe anaweza kujikuta ni gamba ndani ya chama, jambo ambalo litakiletea chama madhara makubwa kuliko ilivyodhaniwa.

  Alisema wabunge wameshtuka kwa sababu wamegundua rais anawatumia kujiimarisha kisiasa wakati akijua yeye anastaafu miaka minne ijayo, na baadhi yao watakuwa bado wanahitaji kujijenga kisiasa kwa malengo ya siku zijazo.


  "Kwa sababu hiyo, tutafika mahali tutampuuza kwa masilahi ya watu wetu, chama chetu na nchi yetu. Haaminiki tena, maana kama ameweza kuchonganishwa na watu waliomtafutia urais, itakuwaje sisi tusio karibu naye?"


  Source: Tanzania Daima
   
 2. mKaLI_mOkO

  mKaLI_mOkO Member

  #2
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  JK mwenyewe ni gamba kama ana uzalendo wa kweli ajivue.....hata mwaka hajafikisha awamu hii nchi ishamshinda hii.
   
 3. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mhhhhhh
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Crap ze crap ze upupu
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  tatizo liko kwa mwenyekit wa chama na ambaye anajiita Raisi huyu ndo kikwazo anapaswa kuondolewa
   
 6. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Kama ulishindwa kumuondoa kwa kura 2010, sasa hivi utamuondoa kwa vigezo gani?
   
 7. HT

  HT JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  which serikali are they talking about!? Do we have any govt? Where is it?
   
 8. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  msema kweli sikuzote huonekana mtu mbaya sana lakini huu ndio ukweli wala hakuna mjandala tuangalie mbele natuone nini kilicho kifikisha ccm hapo na kinaelekea wapi? naamini kama ccm wasipolrekebika huu kweli ni mwisho na hiyo mizingo ndio itadondoka nayo na kuelekea shimo amabako kamwe hawatatoka
   
 9. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  He has nothing significant to lose, kapata 2nd term yake sasa hivi anaimalizia japo kwa kelele nyingi. Tatizo litakuwa kwa hao atakaowaachia chama dhaifu kisichoisha visasi.
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Dhana ya gamba si alitaka kuitumia ili ajisafishe na kukisafisha chama angali akijua yeye mwenye ni miongoni acha nae aone utamu wa gamba
   
 11. President Elect

  President Elect JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 693
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mh. Rais JK, yuko mbali sana na wananchi wake. Ni jambo jema kwa makada wa CCM kumshauri mwenyekiti wao na kumsogeza karibu na wananchi.

  Wana-CCM wakimwachia JK alizamishe jahazi lao, na wao watazama naye!
   
 12. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ....Marehemu Horace Kolimba aliwaambia chama kimepoteza muelekeo wakamuona majinuuuuni. Nadhani alishaona uozo mapema na sasa serikali nayo chali....Hasara tupu!!
   
 13. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Mama wa magamba atawezaje wavua watoto wake magamba!!!gamba ni gamba!ukitaka kuvua magamba anza na gamba kubwa ndo umalizie na madogo!damn ccm
   
 14. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Mgogoro uko hapo kwenye red.

  Watamshauri nini ambacho hajawahi kushauriwa..?

  Kwani wahenga waliposema "sikio la kufa.........." walimaanisha nini?
   
 15. olele

  olele JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 814
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 80
  Source: Tanzania Daima
  source hiyo inaandika habari za upande mmoja, siwezi comment
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,247
  Trophy Points: 280
  mimi mpaka kesho ninashangaa ya kuwa tulipigwa changa la moto kuwa kamati kuu ni gamba na ndiyo maana ikajiuzulu sasa yawaje JK, Msekwa, Meghji, na wengineo wengi kutoka Zanzibar na akina Makinda wao waonekane siyo gamba? Wababe hawa wao wanaendelea kutesa tu..................ukishangaa la musa utaona la firauni............lol

  Hili zoezi la kujivua gamba laoneka ni la kiubaguzi lazima Mwenyekiti abebe msalaba wake kwa kushindwa kuliongoza hili taifa kupitia serikali yake hawezi kuwa ni kiongozi wa kulaumu walio chini yake tu...................where is leadership in blaming others for blunders of judgment that happened while you were in-charge...................
   
 17. S

  Sanchez Member

  #17
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwani nani kakuambia alipata urais kwa kura nyingi!Usalama wa taifa ndiyo walio muweka madarakani na siyo kura za wananchi.stupid
   
 18. t

  the mkerewe JF-Expert Member

  #18
  Aug 22, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Last uchaguzi Mubaraka alishinda kwa 93 %
   
 19. T

  Tetere Enjiwa JF-Expert Member

  #19
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tumia hekima kidogo tu, nyie ndio mtakao mponza mwenzenu kwa ajili ya kulinda maslahi yenu ya muda mfupi. Mtamsaidia sana kama mtamwambia ukweli. Ukitumia kigezo cha kura hata gadaffi, mubaraka, nk. walishinda kwa kura tena zaidi ya 90% acha hii ya kwenu ya 61%. Mshaurini kwa hekima acheni usanii kwenye mambo ya msingi mtajiponza nyie na mnayejipendekeza kwake. Mambo sasa ni magumu huo ndio ukweli mchungu tafuteni suluhisho.
   
 20. gmosha48

  gmosha48 JF-Expert Member

  #20
  Aug 22, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,960
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Kamuulize Gadafi, Ben Ali na Mubaraka.
   
Loading...