Habari wana jamvi,
Nimevutiwa na maelezo ya mtoa mada nikaona sio mbaya nikachangia pia.
Me pia ni mkulima wa vitunguu, nyanya kwa kutumia greenhouse, hoho, ufugaji wa nyuki kwa njia ya kisasa na matikitiki. Nnachoweza kusema hii sekta ya kilimo ni nzuri sana na bado ina nafasi kubwa sana ya kubadili maisha ya watanzania wengi.
Kwa sasa namiliki kampuni mbili ambazo zimejikita kwenye masuala ya kilimo na dhumuni haswa likiwa kusaidia vijana wenzangu pia kufanikiwa katika kilimo.
Kampuni ya kwanza na kampuni mama inaitwa Lumuma Investment ambayo inahusika na mambo yote kuanzia Greenhouse farming, Drip Tape Irrigation, pia tunazo variety tofauti za mbegu aina ya Hybrid F1.
Kampuni ya pili na kampuni dada inaitwa Central Park Bees Ltd, ambayo inajihusisha na ufugaji wa nyuki na uuzaji wa vifaa vya kisasa vya kufugi nyuki. Tembelea tovuti yetu
http://www.centralparkbees.co.tz uweze kujua zaidi faida za ufugaji wa nyuki kwani ni zaidi ya kupata asali. Kuna products nying utaweza kupata kutokana na nyuki ambazo dhamani hake ni kama Gold.
Napenda kuwahakikishia kuwa kilimo kinalipa, kwani binafsi toka nimemaliza chuo sijawahi kuomba ajira sehemu na nimekua na maisha ya furaha kutokana na kilimo.
Tunapatikana Makole, tukitazamana na msikiti wa Makole Dodoma mjini.
Wasiliana nami kwa simu namba: 0655003510 / 0689658811
Email:
josephkadendula@centralparkbees.co.tz
Ahsanteni sana.