Unaweza kuyaorodhesha baadhi ya hayo mambo yaliyo na kina zaidi ya vyama?
Ewaaa,
Zaidi ya kuwa na vyama tu - ambavyo vinaweza kuwa vyama vinavyoendeshwa shaghalabaghala- kuna umuhimu wa kuwa na vyama vinavyoendeshwa kwa itikadi.
Sasa hivi napata tabu kuelewa itikadi ya CHADEMA kwa sababu inatuma message kwamba ina endorse "Leninism-Marxist" kwa kuliita jeshi lake (lililopigwa marufuku) "Red Brigade" (angalia hizo links hapo ). Naanza kupata maswali kwamba, je, CHADEMA inaelekea kule marehemu Kolimba alikokuita kukosa "dira na muelekeo"?
Pia, kwa mtu anayefahamu historia ya "Red Brigade" atajua ni kikundi cha "Leninist-Marxists" waliokuwa wana advocate violence katika politics, even by political assasination.
Napata tabu kuamini kwamba wakuu wa CHADEMA hawaijui historia hii, kuna watu wana upevu mkubwa mule.
Sasa wao kuchapa hizi fulana na kuanzisha jeshi la "Red Brigade" ina maana wana endorse violence in politics na political assasinations?
Ndio maana naona mambo kama itikadi ni muhimu, kwa sababu bila itikadi utakuwa all over the place, mara una "Red Brigade" kama "Leninist-Marxist" mara una utandawazi wa kibepari etc.
Kwa hiyo kuna vyama vyenye kuongozwa na itikadi.
Halafu kuna uongozi wa principles tu. Kwamba cahama kikubwa kama CHADEMA ku endorse jina lililokuwa associated na violence is not a good look.
Halafu kuna seriousness. Kwamba chama kama CAHDEMA kuruhusu jina kama hili kuwa associated na chama chao maana yao nini? Wanataka wananchi wanaoelewa "Red Brigade" ni nini tupate picha gani? Kwamba CHADEMA kinajiandaa na some sort of armed struggle au vipi?
Halafu kuna mambo kama ku focus kwenye mambo yenye mantiki kwa nchi bila kufungwa na vyama. Naona hapa kuna ushabiki kiasi kwamba mtu aki criticize CHADEMA, hata kama ni criticism inayoweza kukijenga chama kwa kukifanya kiwe focused zaidi, anaitwa magamba, hata mtu kama anajulikana hafagilii chama chochote kama mimi, by track record.
Hatuwezi kukataa ukabila halafu tuje kufungwa na makabila mapya ya vyama, bila kuelewa itikadi za vyama na kuwa na uhakika kwamba vitatupa kitu tofauti na CCM.
Hatuwezi kutatua matatizo na kushinda vishawishi vya rushwa vinavyoitatiza CCM kama hatujengi utamaduni wa kuheshimu institutions, utamaduni wa kuwa critical kwenye process na kuacha kuheshimu vyama kama dini, kiasi cha kum label yeyote anaye criticize chama chako kama "magamba" au "magwanda".
Mambo ni mengi, hayo ni kwa kuanzia tu chap chap.