Kikosi cha wasomi [Doctors, engineers, na wengine] kuhutubia mkutano wa CHADEMA Reading, UK

That much is known, apparently.

Unaijua historia ya the original "Red Brigades"?

Kwa nini CHADEMA ikachagua jina lenye legacy ya damu kama "Red Brigades"?

CHADEMA inafuata falsafa za "Leninism-Marxism"? Inaamini katika violent politics na political assasinations? Inafanyia vetting hizi setup za hizi militias? Inasemaje kuhusu marufuku ya jeshi la polisi dhidi ya militias zote za vyama vya kisiasa kwa msingi kwamba hazipo kisheria (including Green Guards) ?

Unauliza maswali au tayari unatoa majibu.
Hudhuria mikutano yetu,jukwaani mara nyingi majibu haya huwa yanatolewa.

sorry nilijibu uliloitaji.hayo mengine ni mawazo yako (yenu watu kama Mwigulu....)naomba nisiyalete hapa maana chanzo cha mjadala si hayo uliyoyaleta.
 
Kufikiri kwamba kila mtu anaweza kuhudhuria mikutano yenu ni makosa. Kama huna majibu sema tu majibu sina. Kama unayo yatoe, hata hapa JF unaweza kupageuza pakawa mkutano wa CHADEMA.

Kuona mtu yeyote anayeuliza maswali critical ni "kama Mwigulu" ni kuwa shallow, kuto address issues na kukimbia maswali kirahisi. Vitu hivi tunavitegemea kutoka chama tawala ambacho mnataka kukitoa. Hatuvitegemeai kutoka chama mbadala kinachotaka kuja kubadilisha mambo. Mkiwa na majibu haya mnatutia shaka kama mna tofauti yoyote kubwa na CCM.

Kada mzuri wa chama haogopi challenge kwa visingizio.

Ningekuheshimu zaidi ungesema "Original Red Brigades siijui, ndo kwanza nasikia kwako kwamba kulikuwa na original Red Brigades, mie nimepelekwa pelekwa tu, labda tuulizane huku wanaojua tukupe jibu".

Lakini hizi habari za kutaka ku shut down relevant questions bila kutoa majibu ni a characteristic of totalitarian regimes and tyrants in monopolistic ruling parties.

Not hopeful oppositions.

Msivunje watu moyo kwa kukataa valid criticism, tutaona mnafront mageuzi bila kuonyesha kwamba mko serious.
 
Mkuu ili bandiko lako hakuna mtu yeyote wa UK atayekujibu...umemaliza kila kitu.
Ritz, ni vyema ukija au tuma mjumbe aje asikilize kuliko kushinda ukikandia vitu ambavyo wewe mwenyewe unaona kabisa ni vya manufaa kwa uma. Mie nazani kama ubalozi wangetumia zile pesa ambazo mdingi anatumia kwenye safari zake za kuhudhuria semina ya uzazi wa mpango
 
cdm endeleeni na wema wenu wa kugeuza umoja wa wachaga kuzikana na kuwa chama cha ukombozi huko ugaibuni,pia muweke wazi kuwa,wasomi wa kanda ya kaskazini wanaoishi huko ndio wameandaa.
 
cdm endeleeni na wema wenu wa kugeuza umoja wa wachaga kuzikana na kuwa chama cha ukombozi huko ugaibuni,pia muweke wazi kuwa,wasomi wa kanda ya kaskazini wanaoishi huko ndio wameandaa.
Aliyeandaa ni mhehe akisrikiana na mhaya, msafwa na mfipa
angalia majina ya viongozi wa chadema uk
 
Bora wafanye hivyo maana Serikali imekosa pesa ya kuendesha Barozi zetu, nyumba za ubalozi zimejaa buibui huku SYMBION inapewa M152 kwa siku
 
Hao wasomi wameleta faida gani Tanzania? Hawana tofauti na hao wa M4D(death).
Hawajatumiwa ila wakitumiwa mtaona faida yao then kwa ufupi kwa wale wakazi wa dodoma mtakumbuka umuhimu wao katika nyanja ya usafiri, Best na Norman yani Poazz kama POA
 
Mheshimiwa Mzee kazi.karibu sana kijiweni kwetu reading.naomba unipe ufafanuzi kidogo Mzee Aseri katanga si Msomi hana digrii kama wewe.lakini Computer 4 Africa hafanyi kazi ya kulipwa mshahara.ni kama Bodi member kukiwa na jambo alipwa posho ya kikao. kazi yake tuulize sisi watu wa Reading ni Care.anatunza wazee na kwake ni Slough mwendo wa dakika 12 toka Reading amefanya shift Moja na Katibu wa CCM Susan Mzee.unngeuliza kwanza.Aseri hana digrii ukinithibitishia hilo naomba Admin anifungie.

Lusingu anafanya kazi ya kulinda madukani usomi wake unasaidia nini wakati yeye mwenyewe kashindwa kupata kazi professional,watu wa Redaing wanamjua alikuwa pamoja na Susan kwenye CCM.ziko picha zake akiwa na shati la kijani.najua wewe ni mgeni wa siasa ungeuliza kwanza.

labda iwe ndio siku hiyo ya mkutanano ndio awe anarudisha kadi ya CCM kwenu. na ilivumishwa sana hapa Reading kuwa alipokuwa amejiunga CCM alikuwa katokea chama cha DP.kutokana na kukosa uaminifu CCM wakamnyima uongozi akawa na kinyongo na Susan Mzee na wakawa hawasemi.

Lusingu John amekuwa katibu mkuu wa Jumuiya ya watanzania hakuna alichokifanya.amekuwa mwenyekiti wa watanzania UK hakuna hata jambo moja alilifanikisha hadi akaacha uenyekiti wa Tanzania Association kimya kimya kwa kuona aibu.

hakuwahi kuitisha mkutano wala kikao cha watu wowote kwa kipindi chote cha uongozi wake. ni watu wachache sana wanaojua kuwa ni Mwenyekiti wa Tanzania Association.

ukiniambia nimchangue Chris Lukosi na Lusingu basi nitampatia Chris Lukosi hata kama hana shule.

MFUKO WA MAZISHI.

Tunaomba msiwachangishe watu pesa. hadi hapo Chadema mnapofungua account ya Mazishi.

Chris Lukosi aliwachangisha watu wa Uingereza hasa watu walioko London wakachangia nguo za wahanga wa mafuriko Jangwani Tanzania Mwanzoni mwa mwaka huu.tulio mbali tukaona wako na naibu balozi ambaye leo wanamtukana kuwa hawajafanya chochote.

Mizigo ile Chris akitumia mgongo wa kampuni yake akasema kuwa itafikishwa Tanzania mwezi wa pili hadi leo ni september tunamaliza mwaka hatujaona mizigo ile kukabidhiwa na kwa kihelehele kwa Serengeti Freight kampuni ya kina Lukosi kama mizigo ile ingefika tungeona mapicha Mjengwa Blog,michuzi na kwa shingongo.naomba mkabidhi kwanza mizigo ya wahanga kabla ya kuja na gea ya mfuko wa mazishi.

kwanza hakuna Mtanzania aliwahi kufa akashindwa kusafirishwa Lusingu amewahi kufikwa na tatizo hilo tulimsaidia hadi hatua ya mwisho. tunahitaji mfuko wa maendeleo sio Mazishi.
Mgongano wa kimaslahi.

Lusingu ni mchungaji anafanya ibada zake hapa kila jumamosi ni Msabato nadhani ndio sababu mojawapo ya kuupeleka mkutano wa Chadema nje ya jumamosi ni mtu wa dini.

Kampuni ya serengeti Freight imejadiliwa sana humu jamii Forums,kabla ya Chris kuwa mwenyekiti.kampuni hii haitajwi vizuri na watanzania ni inasadikiwa ni kampuni ya Dili fulani fulani, yaani usafi wa chiris na kampuni yake una mashaka makubwa. na hao wanaitwa wasomi, wameifanyia vetting kamopuni hii kabla ya kufunga nao mkataba?

Tatizo la Pili.

Chris Lukosi anafanya mambo yake kiengeji mno bila organisation, ukitizama matangazo yao ya serengeti mengi yanamakosa yanathibitisha kuwa kampuni inaongozwa na watu ambao labda wamekwenda shule hawakuelimika vya kutosha.
kama lilivyo tangazo hili la Mkutano wa Reading,siamini kama limeandikwa na mtu aliyepita shule vizuri ukitazama lugha ya kebehi kama ubalozi umeshindwa.mtu makini angesema kuwa tunafanya hili na lile na sio kuanza kuoneshea vidole wengine.jamani tuko Ulaya,juzi Mancini wa Man.City anawasifu wachezaji wa timu yake pinzani kuwa RVP na Rooney hawakamati.watu huwa wanasema mambo yao.ukimuona mwanamke mzuri mwambie utamfanyia nini sio kuwasema wengine.

sasa litakuja Tatizo kubwa chris atangangania yeye ndio mwenyekiti na hao wanaitwa wasomi watataka kuja na muundo wao wa utawala hapo ndio mgongano utakapoibuka.Lusingu hatakubali kuongozwa na mtu asiyesoma na yule asiyesoma atasema wewe una PhD lakini Mlinzi na mimi sijasoma ndio nina kampuni yangu ya kutuma vifurushi Africa, usomi wako umekusaidia nini?

kwanza LEMA ananijua mimi, sidhani kama mafahari hawa wawili wataiva.
nasubiri mkutano.

Benard Chisumo,
Inaelekea una chuki binafsi na watu/mtu fulani. Karibu kwenye mkutano.
 
Chilisosi,
Unasumbuka bure na hayo matawi hapo UK kinachofanyika ni mchongo fulani nyie pamoja na Lema, sio kutangaza Chadema ninavyoijua Uingereza, Watanzania wengi wamejiripua na wengine kesi zao za ukimbizi zipo mahakamani hawataki kabisa mambo ya siasa za Tanzania, kama wapemba wa Uingereza wameitosa CUF mtaweza nyie na ndio wapo wengi...uwa nacheka sana nikifika Uingereza kuna Wachagga, Wasukuma, Wahaya, wamejiripua raia Wasomalia.
Naona jamaa zako wameandaa ubwabwa, vipi utakuwepo?
 
Benard Chisumo,
Inaelekea una chuki binafsi na watu/mtu fulani. Karibu kwenye mkutano.
Mzee ungejibu hoja mbali mbali ya muhimu ile mizigo ya wahanga wa mafuriko mliyokusanya iko wapi? tupeni mahesabu hayo kabla ya kuja na jambo jipya gea ya kuzikana.
kwanini mzianze na kuwatembea jela watanzania walioingizwa jela na dili za kampuni fulani ya kutuma mizigo ya watanzania iko UK? mnazisaidia vipi familia zao? mimi sina muda hadi nije kukukusikiliza? umetudanganya kuwa Aseri na digrii wakati unajua unasema uongo.
 
Aliyeandaa ni mhehe akisrikiana na mhaya, msafwa na mfipa
angalia majina ya viongozi wa chadema uk
uchaguzi ulifanyika lini? wewe ulipata kura ngapi wakati walioshiriki ufunguzi wa tawi waliokuwa kumi na nafasi ya katibu mkuu hakuna.umerudisha kadi hapo hapo unakuwa kiongozi.katiba ya chadema huijui.utaweza vipi kuwa kiongozi? mkuu mizigo ya wahanga wa mafuriko ya jangwani vipi?
 
Kwa nini uweke "wasomi"?
Bila shaka ni kwa sababu wengi walioko huko ughaibuni ni wasomi wa namna moja au nyingine. Tunafahamu idadi kubwa ni wanaofanya masomo ya juu huko, wapo pia wanaofanya kazi wakiwemo wataalamu kama madaktari, wahandisi, na wanasayansi ambao baada ya kubanwa pumzi hapa waliamua kufanya kazi na kuishi kule.
 
MKUTANO WA CHADEMA READING

TAWI LA UK

Mkutano utafanyika siku ya Tarehe 26/08/2012 kuanzia saa saba mchana mpaka saa kumi na mbili jioni, siku ya Bank Holiday. .Risc Reading International Solidarity Centre, 35-39 London Street, Reading, RG1 4PS .
BAADHI YA WATOA MADA MBALI MBALI WATAKAONGEA SIKU HIYO NI;
DR, LUSINGU
DR, ALEX
ASERI KATANGA (Chairman computers for AFRICA)
Engineer PRUDENCE
LIBERATUS MUSIBA (Msc, Project planning & Management)
NA WENGINE WENGI
Watanzania wote na wadau mbali mbali mnakaribishwa
MFUKO WA KUFA NA KUZIKANA UTAANZISHWA SIKU HIYO KWA AJILI YA WATANZANIA WOTE WAISHIO UK. MFUKO UTASAIDIA KUSAFIRISHA MAREHEMU PAMOJA NA MFIWA MPAKA NYUMBANI. KITU AMBACHO UBALOZI WETU UMESHINDWA KUKIFANYA

SISI SOTE NI NDUGU, TATIZO NI CCM

ni wakati wa kusimama na kusema tumechoka

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA HAWA WAFUATAO
MWENYEKITI: Chris Lukosi 07903828119

Au tutumie email kupitia chademauk@gmail.com

Peooooople's Power

Chris
Jumapili sio Bank Holiday.ni jumatatu tarehe 27 ndio bank holiday.sasa hao wasomi wako wameshindwa kukueleza kuwa jumapili sio bank holiday.kwani huna diary mwenyekiti wetu?
umedanganya kuwa aseri ana digrii.
pia phD za lusingu za kubeba maboksi Tesco na Sainsbary's yaani phd yake imeshindwa kumsadia kupata kazi ya kitalaam.
mngeanza kumsadia yeye.kabla ya kutaka kutuibia na mfuko wa mazishi.jamani nyie misheni town acheni utapeli.
 
Bila shaka ni kwa sababu wengi walioko huko ughaibuni ni wasomi wa namna moja au nyingine. Tunafahamu idadi kubwa ni wanaofanya masomo ya juu huko, wapo pia wanaofanya kazi wakiwemo wataalamu kama madaktari, wahandisi, na wanasayansi ambao baada ya kubanwa pumzi hapa waliamua kufanya kazi na kuishi kule.
asili ya chadema sio usomi.Mbowe si msomi.hata hawa ni wabeba maboksi kama chris.
nadhani kipindi hiki chris lukosi ungetumia kujifunza katiba ya chadema na muundo wa chama.hata salam za chadema huzijui.nakuliza Brown Ngululupi ni nani katika chadema?
swali la pili nitajie ni nani aliyeandika katiba ya chadema kwa mara ya kwanza?
najua hujui kitu nakupa wiki kujibu maswali haya.hutaweza hata umuulize Lema.misheni town mwenzio.
 
Nyinyi mnaojiita wasomi mnafanya nini UK?, kama mimi nimgekuwa na Elimu kama yenu nisingebaki huko Uk. ningerudi kujenga nchi yangu, Mnahimizana kutoa michango ya misiba, kazi mnafanya UK, maiti inazikwa Tanzania, sasa hapo mmmetusaidia nini wanyonge?
 
asili ya chadema sio usomi.Mbowe si msomi.hata hawa ni wabeba maboksi kama chris.
nadhani kipindi hiki chris lukosi ungetumia kujifunza katiba ya chadema na muundo wa chama.hata salam za chadema huzijui.nakuliza Brown Ngululupi ni nani katika chadema?
swali la pili nitajie ni nani aliyeandika katiba ya chadema kwa mara ya kwanza?
najua hujui kitu nakupa wiki kujibu maswali haya.hutaweza hata umuulize Lema.misheni town mwenzio.
Pole naona unalalamika mpaka povu kukutiririka, naona mambo ndiyo baado kabisa maana ngoma bado mbichi. Aliyeiandika Katiba ya CHADEMA wa nini na unamtafuta ili mumfanyeje? Mum-Ulimboka? Aibu tupu! Suala la muhimu ni kama Katiba hiyo ni nzuri au mbaya; hata kama ikiwa iliandikwa na mtu mmoja, 28 au hata milioni moja. Kwa taarifa yako Katiba ya CHADEMA ina mvuto, ni nzuri na ilwahi kusifiwa na watu mashuhuri kama Hayati Mwalimu Nyerere. Suala ni nani aliiandika si muhimu tena kwa watanzania wenye mapenzi mema na nchi yao na waliojaa hamasa ya kuikomboa nchi yao toka kwenye makucha ya wakoloni hatari wa CCM. Ndiyo maana mnashindwa kuwanyamazisha hata kwa risasi za moto. Subirini nchi ikombolewe muikimbie maana mtatakiwa kujibu kila nukta ya uhaini mlioitendea nchi yetu hii na watu wake.
 
Kamanda umeandika ujumbe mzito sana
 
Back
Top Bottom