Kikosi cha Simba 2012: Wako wapi na wanafanya nini kwa sasa?

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,219
22,286
Mwenye kujua walipo wachezaji wa Simba 2012 walioifunga Yanga 5 - 0 ashushe data hapa kwa heshima ya hawa Legends walioipa Yanga adhabu isiyovumilika.

Wapo wapi na wanafanya nini kwa sasa?
 
Mtu akiishiwa Pesa anakumbuka madeni yote! Kweli fungu la kukosa ni mzigo mzito! Simba sasa dhofulhali mashabiki hawana tena cha kujifariji zaidi ya kukumbuka mechi za long fuc,,, ago za kuifunga Yanga! Poleni sana watani njooni tu kwa Mkapa j2 mshangilie waarabu mtapunguza stress!

Huyu Rage the Great kolo pekee mwenye akili Simba nzima sasa ni wakati muafaka akiwa mzima wa afya tumtafute tumpe Maua yake 🌹🌷🥀💐🔥 na tuhakikishe sanamu lake limejengwa na kuwekwa juu ya Ghorofa la Simba pale Kolokoloni Msimbazi Maana Makolo wote waliobaki including my son and wife kukiwa na mawingu tu madishi yao yanayumba! Kufa kiume Kila mechi inauma sana!!

Yani Mbumbumbu kolowizard watu wa ajabu sana si tunaongelea historia Tanzania kucheza fainali CAF huku watu wenye akili wanapigana vikumbo kununua tickets kibao kumbe kuna wengine wako kwenye mashimo kama kina Gods must be crazy!
 
Golini: Juma K Juma, sasa ni kocha wa Magolikipa Stars

Mbavu ya kulia: Nassoro Chollo, mara ya mwisho alikuwa Stand United

Mbavu ya kushoto: Omar Maftah atakuwa kwao huko.

Beki kati: Baba Esta (Kapombe), yupo Simba bado
:Kelvin Yondani, yupo Geita Gold

Kiungo Mkabaji: Patrick Mafisango (RIP), ameshageuka mbolea.

Winga wa Kulia: Uhuru Suleiman, sijui alipo.

Winga wa kushoto: Emanuel Okwi, yupo Al Ittihad

Kiungo mchezeshaji: Mwinyi Kazimoto, sijamsikia hivi karibuni.

Kiungo Mshambuliaji: Haruna Moshi Boban, naye sifahamu alipo. Itakuwa kastaafu.

Mshambuliaji: Sunzu Felix, alienda kwao Zambia. Sijui timu gani.

Mtani tulimtandika Mkono, mpaka Golikipa alifunga. Dharau kabisa.
 
Hiyo central defender ya Simba ilikuwa moto

Kelvin yondani
Juma nyoso
Shomari kapombe
 
Golini: Juma K Juma, sasa ni kocha wa Magolikipa Stars

Mbavu ya kulia: Nassoro Chollo, mara ya mwisho alikuwa Stand United

Mbavu ya kushoto: Omar Maftah atakuwa kwao huko.

Beki kati: Baba Esta (Kapombe), yupo Simba bado
:Kelvin Yondani, yupo Geita Gold

Kiungo Mkabaji: Patrick Mafisango (RIP), ameshageuka mbolea.

Winga wa Kulia: Uhuru Suleiman, sijui alipo.

Winga wa kushoto: Emanuel Okwi, yupo Al Ittihad

Kiungo mchezeshaji: Mwinyi Kazimoto, sijamsikia hivi karibuni.

Kiungo Mshambuliaji: Haruna Moshi Boban, naye sifahamu alipo. Itakuwa kastaafu.

Mshambuliaji: Sunzu Felix, alienda kwao Zambia. Sijui timu gani.

Mtani tulimtandika Mkono, mpaka Golikipa alifunga. Dharau kabisa.
Huyu kapombe sahivi naambiwa nimemzidi umri.
 
KIKOSI Cha Simba 2012 kilichukua UBINGWA bila KUPOTEZA Mechi hata Moja.

YANGA ALIPIGWA 5-0.

simba.jpg
 
simba.jpg

Kutoka kushoto.

1. Emanuel Okwi.
2. JUMA KASEJA.
3.shomari kapombe.
4. Amiri maftaha.
5. Mwingi kazimoto.
6.Nassor chollo.
7.uhuru Suleiman mwambungu.
8.CALVIN YONDAN.
9.Harun moshi
10.mafisango RIP.
11.Felix sunzu
 
Back
Top Bottom