Tathmini yangu kwa kuhusu uwezo wa Benchika katika kuleta mabadiliko ndani ya kikosi cha Simba

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
439
1,756
Kuna mwaka fulani Simba ilimchoka marehemu Aggrey Siang'a baada ya kuiletea mafanikio makubwa Simba, Siang'a alikuwa anatisha, Simba ilikuwa ikitoa vipigo vya mabao 5 kila anayesogea mbele, akina emmanuel Gabriel walikuwa wanamtesa sana kipa wa yanga wakati huo Peter Manyika, lakini baadae mbinu za Siang'a zilifeli, Simba ikamuondoa ikamrudisha Patrick Phiri ambaye alishindwa kuibadilisha timu akaondolewa ndani ya muda mfupi.Kipindi hicho Simba ilikuwa na migogoro ya chini kwa chini kama ilivyo sasa ingawa haisemwi.

Hali ile naifananisha na sasa hivi, tumemfukuza Robertinho na hasa pale tulipopigwa mabao 5 na mtani ikawa ndio sababu, Leo amepewa timu Benchika lakini mambo ni yale yale tu.

Kwanini mambo ni yale yale?

1.Simba haichezi mpira mzuri, ile Simba ya Mgunda au ile tunayoifahamu haijabadilika bado.

2.Pira linalochezwa na Simba halina furaha kabisa.
3.Wachezaji bado wamefungwa nyota zao, wanapambana lakini wamewekewa kitanzi, wazito kishenzi
4.Benchika hajui wakati gani amuingize nani, mechi inaweza kuwa ngumu lakini ukakuta anamuingiza mchezaji ambaye hana impact yoyote
5.Upangaji wake wa kikosi nao sio mzuri mfano Kanoute, ngoma na Babacar kucheza pamoja sio sawa
6.Timu isipofanyiwa dua ya kufa mtu itaendelea kutema wachezaji hadi siku ya kiama, mwakani Yanga wanamchukua Baleke
 
Back
Top Bottom