Haya yote ni serikali kushindwa kutawala chini ya CCM, na kukimbilia kikombe ili kutuliza vuguvugu la mabadiliko, hakika tujiandae kuona rangi ambazo hata hatujawahi kuziona.
Serikali yoyote iliyopoteza mwelekeo siku zote huwa inakumbatia hoja nyepesi nyepesi, kama ilivyotokea kwa Mobutu ambaye alishia kuwashinikiza wana muziki wa kizaire wamwimbie kwenye nyimbo zake, mwishowe akazikwa na watu wachache katika maziko yasiyo kuwa na heshima.
Kama CCM na viongozi wake wanasoma alama za nyakati vizuri wajiandae kuelekea huko, pona yao ni kujichuna ngozi na kutoa nyama ibaki mifupa walioikataa ya azimio la arusha.
Nje ya hapo ni kuporomoshwa kwa kishindo kikuu na chama kusambaratika mpaka baada ya miaka hamsini mingine.