Ms Judith
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 2,563
- 918
Neville Meena na Mussa Juma, Samunge
................
Kikombe cha babu
Dawa yote wanayokunywa wagonjwa wanaofika katika Kijiji cha Samunge lazima ipitie katika mkono wa Mchungaji Mwasapila.
Mkono wa mtumishi huyu wa Mungu huwa umeshikilia kikombe maarufu kama "kikombe cha babu", ambacho hukitumia kuchota dawa kutoka kwenye ndoo ambazo huletwa na wahudumu. Anachiokifanya ni kujaza vikombe vingine ambavyo hutumiwa na watu kunywa dawa hiyo.
Wakati wote utamwona Mchungaji Mwasapila akiwa na kikombe hiki mkononi mwake, huwa hakiachi popote anapokwenda labda kama si wakati wa kutoa dawa. Hapa ina maana kwamba hata kama akienda kupata chakula cha mchana au chai ya saa nne, babu huondoka na kikombe chake.
Wakati akieleza kuhusu kikombe hiki, Mchungaji Mwasapila alikuwa na uso wa tabasamu kwa mbali, hii inaashiria kwamba kikombe chake kina thamani kubwa katika utoaji wa dawa au tiba kwa wengine tunavyoweza kutamka.
Anasema kwa kuzingatia kazi zake za ufundi uashi, wakati fulani alilazimika kuwepo Mjini Loliondo ambako alikuwa akijenga nyumba ya watawa wa Kanisa Katoliki.
Anasema baada ya kukamilisha ujenzi huo uliochukua siku kadhaa, alirejea nyumbani kwake, Samunge ambako alikuta kikombe ndani ya nyumba yake kikiwa kikizagaa.
"Niliwauliza wale vijana niliowaacha pale nyumbani... Jamani hiki kikombe ni cha nani? lakini kila mmoja alisema hajui na wala hawakufahamu jinsi kilivyoingia ndani ya nyumba yangu."
Anasema walijaribu kuwauliza hata majirani iwapo kuna mtu ambaye kwa namna moja au nyingine alikuwa amesahau kikombe kile, lakini hakuna aliyejitokeza hivyo kukiacha ndani bila matumizi na kwamba kilikuwa kipo kipo tu ndani ya nyumba hiyo.
Kwa mujibu wa Mwasapila, baada ya muda mrefu kupita (hakumbuki ni muda gani), alilazimika kumuuliza Mungu kipimo cha dawa aliyoonyeshwa kuitoa kwa watu na hapo ndipo alipoonyeshwa kikombe hicho ambacho anasema wakati wote kilikuwa kikizagaa ndani ya nyumba yake.
"Mara moja nilinyanyuka nikaenda kukichukua kikombe, na hapa ndipo nilipojua thamani yake, Mungu alisema kikombe ndicho kipimo sahihi na mtu anatakiwa kunywa kimoja tu na watoto ni nusu yake", anasema.
source: http://mwananchi.co.tz/biashara/-/10635-usiyoyafahamu-kuhusu-mchungaji-mwasapilaItaendelea wiki ijayo….

haya wapendwa,
hii hapa homework mpya, kumbe babu alikiokota kikombe chake? na anatembea nacho kila anpoenda!
Mungu gani anayetenda hivi? anayenunua vikombe na kupelekea watumishi wake?
niende wapi kuukimbia uso wako?
nikipanda mbinguni, wewe uko!
nikifanya kuzimu kitanda changu wewe uko,
nikisema giza litanifunika,
giza na mwanga kwako ni sawasawa!