kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,313
- 12,613
Hakuna ambae hatastaafu kazi, kesho kama sio wewe utakaestaafu basi atastaafu baba yako, shangazi, babu, mama mkubwa, dada, kaka, mama, baba mdogo, jirani nk. Hivyo, haki lazima itendeke hata kwa anaeachishwa au kuacha Kazi mwenyewe apewe chake.
Kitu cha msingi ni elimu ya kustaafu kazi itolewe kwenye mitaala yetu ya sekondari ili kila MTU bila kujali anafanya Kazi gani afahamu namna ya kushughulikia kustaafu kwake Kazi.
Kila mfanyakazi na kila kijana wa Leo lazima afahamu kuwa iko siku siku atazeeka na kushindwa kufanya hiki anachokifanya Leo kupata chakula, malazi, mavazi, matibabu na starehe, hivyo aanze kuanzia sasa kuwaza na kuchukua hatua juu ya namna atavyopata chakula, malazi, mavazi na matibabu yake siku akiacha Kazi kwa uzee au ugonjwa, au kuachishwa Kazi.
Kikokotoo kisiwe na mizengwe ndani yake, kikokotoo lazima kijikumbushe kuwa hata hii misharahara wanayopewa watumishi Leo ni midogo sana kuliko uhalisia, wanapunjwa sana sana sana. Hii sio mishahara bali ni posho tu wanapewa. Hivyo kikokotoo kilenge pia kurekebisha athari za mishahara mishahara midogo wanayolipwa watumishi.
Hivyo hakuna mtumishi awe waziri, mbunge, mkuu wa majeshi au mwalimu asiyetaka kikokotoo kinachompa ahueni pale atakapostaafu.