Kikeke ambana Maalim Seif

Kikeke ambana Maalim Seif

Averos

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2010
Posts
994
Reaction score
703


Leo wakati akimhoji Maalimu Seif juu ya uchaguzi wa Zanzibar, Salim Kikeke mtangazaji wa BBC, aliishia kupigishana makelele na Maalimu Seif kwani kila mmoja alikuwa anaongea kwa sauti.

Huu ndio utaratibu wa kuhoji watu Salim?
 
Muda huu maalim seif yupo kikaangoni BBC chini ya salim kikeke,.Amembana kwa nini hakuhamasisha wafuasi wake kupiga kura kwa maranyingine ikiwa yeye alishashinda kwenye uchaguzi wa awali.Kwa mara nyingine tena maalim anachemka kuhusu kususia uchaguzi.Kazi kwenu mnao muabudu.Dk 3 za maswali toka kwa Kikeke maalim jasho limemtoka.
 
Habari,

Naangalia BBC Swahili hapa Star TV ghafla napandwa na hasira kuona Salimu Kikeke akimuhoji Maalimu Seif kwa dharau na kumuingilia kila Maalimu Sief akijaribu kujibu maswali anayoulizwa.

Kifupi Kikeke ameonyesha kuwa upande mwingine wa siasa mbal na Maalimu Seif.
Sijui ndo msimamo wa BBC Swahili au??
Wajuzi tujulishane
 
Nimefurahishwa sana Salimu Kikeke alivyomuhoji Seif
Kwasababu Seif hakuwa na hoja za msingi kwanini hwakushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar
 
alichokua anafanya Salim ni ku argue katka kila sababu aliokua anatoa Maalim na hzo ni mbinu za wana habar
 
Mtu kapewa dakika 3 za kujieleza snataka aanze kuhubiri, kipindi kile hakina muda wa mjadala zaid ya ndio na hapana kwa sababu ya msingi na sio historia
 
sishangai watu humu wakimponda salim kikeke maana wakati ule kuna mtu alisema anaonewa na mwandishi wa hii bbc swahili kwa hiyo ni mwendelezo tu wa kile kinachoitwa kuonewa.
lakini kiukweli kutokuelewana kulianzia kwa maalim seif kukimbia swali badala yakujibu swali,na salim alikuwa anajaribu kama sio kulazimisha mhe.maalim seif kurudi kule salim anapopataka.
 
Back
Top Bottom